KANISA LA TAG LAMCHAGUA ASKOFU WAKE MKUU.

 Askofu Dk Barnabas Mtokambali

Dr Barnabas Mtokambali  achaguliwa tena kuwa Askofu mkuu wa TAG
Makamu wake ni Rev Dr Magnus Mhiche mchungaji wa Mbagala spiritual centre
Na katibu mkuu ni Ron Swai mchungaji wa Dar es Salaam Calvary Temple DCT  


 Askofu Dk Barnabas Mtokambali, amechaguliwa kwa awamu nyingine tena kuongoza kanisa hilo, kwa miaka minne. Dk. Mtokambali aliibuka mshindi katika kura za maoni kwa kupata jumla ya kura 2250, kati ya kura 2403 zilizopigwa, akifuatiwa na askofu Lawrence kametta aliyepata kura 128.
Ushindi huo wa 2/3 sawa na asilimia 75 ya kura zote, ulimfanya msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Mmishenari Gregory Beggs kumtangaza Dk. Mtokambali kuwa Askofu mkuu kwa awamu hiyo ya tano.

Mkutano huo pia ulifanya uchaguzi kwa upande wa makanu, ambapo askofu Dk.agnus Mhiche naye kwa mara nyingine ya tatu amechaguliwa kuwa makamu askofu Mkuu, baada ya vuta nikuvute kati ya Askofu Lawrence kametta, iliyosababisha uchaguzi kurudiwa mara tatu mfululizo.

Kwa ufande wa katibu, Mchungaji Ron Swai naye amerejea kwenye nafasi yake baada ya kuteuliwa na wapinzani wawili na kuwabwaga kwenye kura za awali na kutangazwa kuwa katibu mkuu kwa awamu nyingine tena.

Kuchaguliwa kwa viongozi hao imewarejesha wote waliokuwepo kwenye nafasi hizo bila kufanyika mabadiliko yoyote. Hata hivyo katika mkutano huo ulifanyika uchaguzi wa viongozi waajimbo, sehemu na kamati zao.


Dr Barnabas Mtokambali ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Bethel Revival Temple, Mtaa wa Mwembe Songo, Morogoro Mjini, Katika mkoa wa Morogoro, Tanzania

Kwa mara ya Kwanza Dr. Barnabas Mtokambali alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa TAG kwa kipindi cha miaka 4 Alichaguliwa kwa mara ya Kwanza august 2008

Kwa awamu nyingine ya pili Dr Barnabas Mtokambali alichaguliwa kuwa askofu wa TAG kwa kipindi cha miaka minne (2013-2016) 
Askofu Mkuu wa TAG Dk Barnabas Mtokambali(Katikati) akiwa na Makamu Askofu Mkuu Dk.Agnus Mhiche(Kulia) na Katibu mkuu  Mchungaji Ron Swai mara baada ya kuchaguliwa.

Comments