MAGOTI YAMEKUPOKEA, MAZIWA UMENYONYA, MUNGU ANAKUSUDI NA WEWE!.

Na Mwl Nickson Mabena
" *Mbona hayo magoti kunipokea*? Au *hayo maziwa, hata nikanyonya*?" AYUBU 3:12
Bwana Yesu asifiwe sana Mtu wa Mungu popote ulipo,
Nimesikia sana moyoni mwangu nikuletee ujumbe huu,
Hivi karibuni wakati napitia kitabu cha Ayubu, na kutafakari baadhi ya Maandiko yaliyomo,
Nilipofika kwenye Andiko hilo (Ayubu 3:12), nikapata Ujumbe ndani yangu, na nikapata msisitizo wa kuandika japo somo fupi kwa ajili ya watu wake,
Ayubu baada ya kukutwa na wakati mgumu sana kwenye maisha yake,
Alipoondokewa na Mifugo yake yote kwa haraka, alipofiwa na watoto wake wote kwa mara moja,
Alipoanza kuishi maisha magumu ambayo hakuwahi kuyaishi kabla,
Ndipo alipoanza kuangea maneno ambayo ukiyatafakari vizuri, utagundua yanatoka kwenye kinywa cha mtu aliyefika mwisho wa akili zake!!.
Alianza kwa kuilaani siku aliyozaliwa,
"Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake". AYUBU 3:1
Akaendelea kuzungumza sana maneno magumu sana,
Akawa anasema ni afadhali angekufa tangu tumboni mwa mama yake, kuliko kuzaliwa, alafu akutane na mambo magumu kama yale,
Akasema, "Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?" AYUBU 3:11,
Umeyaona maneno hayo??,
Ni maneno ya Mtu anayejuta kwa yaliyonpata, na kuona kama muelekeo wa maisha yake haupo tena,
Ngoja nikuulize,
Je! Wewe umefika kwenye wakati mgumu hata kujutia kwa nini umetaliwa?,

Sidhani kama umefikia kwenye hatua hiyo,
Una mambo magumu, lakini sio ya kiwango cha kutamani ungefia mimbani!!.
Kuoa au kuolewa tu ndio vinakufanya kukata tamaa kiasi hicho?,
Kutokua na elimu tu ya kutosha ndio vinakufanya unachanganyikiwa kiasi hicho,
Kitokua na kazi tu ndio vikufanye ulalamike hivyo?,
Nisikilize Mtu wa Mungu,
Ayubu akaendelea kusema, MBONA HAYO MAGOTI KUNIPOKEA?, AU HAYO MAZIWA HATA NIKANYONYA?? (AYUBU 3:12,)
Ya Kwako madogo sana,
Mimi nakwambia, MAGOTI YALIKUPOKEA WAKATI UNAZALIWA KWA SABABU, MUNGU ANAMAKUSUDI NA WEWE,
MAZIWA UKANYONYA KWA SABABU MUNGU ANAKUSUDI NA WEWE,
Usijalaumu kiasi hicho, usiwalaumu watu kiasi hicho,
Mwamini Yesu akuokoe, akupe tumaini Jipya!.
Kama umeokoka, una Mtaji mkubwa sana,
MAGOTI HAYAJAKUPOKEA KWA BAHATI MBAYA,
Vinginevyo, ungefia tumboni, au ungetupwa na mama yako,
Kuzaliwa NJE YA NDOA sio sababu, MWAMINI YESU LEO, AKUPE FUTURE YA MAISHA YAKO..
Mimi nimetumwa nikwambia sentensi ifuatayo, kwamba
MAGOTI YAMEKUPOKEA, MAZIWA UMEYANYONYA, MUNGU ANAKUSUDI NA WEWE!!.
Mimi nimemaliza,
Naitwa,
Mwlm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments