MASHIMO YA KICHAWI

 Na Askofu Dr Josephat Gwajima


Historia ya mashimo Kwenye Biblia zamani ukisoma kwenye Agano la kale mtu alipokuwa anafanya makosa akihukumiwa alikuwa anatupwa kwenye mashimo marefu hushushwa kwa kamba kukaa huko kama jela kifungoni.
Kulikuwa na aina mbalimbali za mashimo kama mashimo yenye wanyama, lengo lilikuwa kama mtu akihukumiwa kifungo cha kifo na Pia kama Mfalme amechukizwa na mtu fulani basi mtu huyo anatupiwa ndani ya shimo hasa shimo la Simba kama Danieli alivyotupiwa.
Aina ya pili ya shimo wakati wa Agano la kale lilikuwa ni aina ya shimo lenye moto ambalo lilikuwa linawashwa moto mwingi na watu waliohukumiwa mfano Danieli na akina Shadrak, Meshak na Abednego walitumbukizwa kwenye shimo lenye moto. Hukumu yao ilikuwa ni kutokana na mambo ya kisiasa ambao wao walionekana wametoka Israeli wakaingia kwenye nchi ya watu na kuanza kupanda kwenda juu kwa kasi sana kwenye uongozi huku wenyeji wakikosa kibali mbele ya Mfalme ndipo wakatengenezewa jambo la kuwakamata kwa Mungu wao ndipo wakatakaa kuinama kwa mungu mwingine ambaye siye Jehova ndipo walipohukumiwa kwenye shimo la moto lakini Mungu aliwaokoa na moto ule haukuwateketeza wala harufu yake haikubaki kwenye miili yao.
Shimo lingine lilikuwa ni shimo lenye maji ambayo yanafika shingoni ambapo mtu aliyehukumiwa ni Yeremia, hapo Yeremia hakuhukumiwa hukumu ya kifo lakini aliwekwa kwenye shimo lenye maji yanayofikia shingoni na ilikuwa mtu akichoka kusimama akiamua kupumzika kwamba achuchumae basi anazama hivyo lazima asimame na chakula anapewa ale juu ya maji.

Yeremia 38: 6 “Naam, nabii Yeremia akasema, Amina, Bwana na atende hivi; Bwana ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya Bwana na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa.”
Aina nyingine ya shimo la agano la kale ni shimo lisilo na kitu ambalo ni refu mtu alikuwa akiwekwa ndani yake anakufa sababu ya kukosa hewa na njaa. Pia kulikuwa na mashimo ya maji ambayo watu walikuwa wanachimba kwaajili ya kunywa maji na kama mtu akishindwa kuyafunika vizuri basi mtu alikuwa anaweza kutumbukia na kuzama. Aina nyingine ni mashimo kwaajili ya vita hayakuwa marefu sana lakini wayahudi walikuwa wanayatumia kwaajili ya vita.
Mashimo haya ilikuwa mtu akiingia kwenye shimo kulikuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kumtoa isipokuwa Mfalme. Mfano mfalme nebkadneza aliamua kumpeleka Danieli shimoni sababu alionekana ameasi, Biblia inasema mfalme usiku hakulala alikuwa anahangaika na asubuhi akaenda kwenye lile shimo na kumwita Danieli shimoni naye akaitikia na kusema Mungu amemtuma malaika wake nami nimeonekana sina hatia, Mfalme ndiye aliye mpeleka danieli shimoni na ndiye aliyemtoa shimoni.
Tunaona kumbe kuna malaika wa kufunga makano ya watu waliojiandaa kukutafuna kiuchumi, kiafya, kimasono, kibiashara, kikazi, na sisi tunaye malaika wa kuwafunga midomo watesi wetu.
Ili kuwatoa walio shimoni ni lazima apatikane Mfalme wa kuwatoa maana kuna aina nne za upako. Kuna upako wa kikoma ambao zamani kwenye agano la kale ili mtu mwenye ukoma achangamane na watu alikuwa anapakwa mafuta ili yamsadie aweze kujiunga na wenzake, pia kuna upako aina nyingine ya mtu kumiminiwa mafuta ya kumfanya awe mfalme(Raisi), kuna upako wa kinabii ambapo mtu anamiminiwa mafuta ya kumfanya awe nabii/mchungaji lakini kuna Upako wa Kifalme ambao mtu mwenye huo Upako ndiye anayeweza kuwatoa wale walio kwenye mashimo na mtu mwenye upako huu wa kifalme ndiye mwenye uwezo wa kusema neno lolote na likawa.

Baada ya Danieli kutolewa shimoni wakaitwa baraza la mawaziri wote kwenye kikao ili nao wajaribiwe apatikane mwenye haki, kikao kile kikawa cha tofauti na vikao vilivyowahi kutokea wakaitwa mawaziri wote pamoja na familia zao na watoto wao na wajukuu wao nao waingie shimoni mule. Biblia inasema wote walitupwa mle shimoni na Simba waliwakamata kabla hawajafika chini.
Pia wakati kina shadrak, meshak na Abednego walipotupwa kwenye shimo la moto, walionekana wapo wanne badala ya watatu kama walivyotupwa. Ukiwa ndani ya jaribu usiogope wewe tembeatembea ndani ya jaribu hilo na baadae utatoka ukiwa hauna hata harufu ya jaribu hilo.
Anayechimba shimo atatumbukia mwenyewe, anayetega mtego utamnasa mwenyewe, anayewasha moto utamchoma, Mungu anaokoa na hukumbuki kama ulikua na tatizo, mwenyewe kwa jina la Yesu.
Mtu anayekuchimbia shimo anakuwa anauhakika kwamba hutazaa tena, hutafanikiwa tena, hutasoma tena, hutaolewa tena, hutasafiri tena lakini hawajui kwamba maandiko yanasema usifurahi ewe adui yangu niangukapo chini nitasimama tena.
Mithali 26:27 “Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.”
Mtu wa Mungu Yusufu alikuwa mtoto wa Yakobo, Yakobo alikuwa na watoto kumi walikwua watoto wa Lea na wawili walikwua watoto wa Raheli Yusufu na ndugu yake walikwua watoto wa mwisho.
Yusufu alienda kuwatembelea ndugu zake wakubwa kuwaangalia wanaendeleaje ndipo walipomwona wakasema yule mwota ndoto anakuja na Yusufu akatoa wazo wamtupe shimoni ili aje amtoe shimoni, baadae wakaja wakataka wamuuwe lakini Yuda yuleyule akashauri wamuuze, (kwenye ukoo wa Yuda huyu ndiye alipotoka Yesu) “Mfalme ndiye anayetoa watu shimoni na ishu ya mashimo ni ishu ya wafalme pekee ndio wenye mamlaka.
Kwenye mashimo walikuwa wanatupwa watu waliokuwa hai na sio wafu.
Hesabu 16: 30 “Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.”
Mithali 1: 12 “Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.”
HISTORIA YA MASHIMO KATIKA ULIMWENGU MPYA.
Hayo mashimo tuliyosema yalikuwa ni mashimo ya kimwili lakini kuna mashimo ya rohoni. Mashimo haya yanamajina mbalimbali.
1. Hayawezi yakaonekana kwa macho.
2. Kwasababu shimo lenyewe ni roho kamili. Lina akili, linaweza kukimbia, ukiingia ndani huwezi kutoka, linageuka na kuwa giza. N.k

HISTORIA YA MASHIMO YA ROHONI.
Historia ya mashimo imeanza na shetani mwenyewe. Mashimo haya yanaitwa mashimo ya wachawi au ya kishetani sababu shetani mwenyewe ndiye anayeyamiliki.
2 Petro 2: 4 “Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu”
Malaika waliokosa ni mashetani waliomwasi Mungu ambao wametupwa shimoni.
Ufunuo 12: 7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”
Kumbe shimo lipo katika nchi na baharini shimoni, ndiomaana ya lile andiko la kisha nikamwona mnyama anatoka katika nchi, na bahari. Mashimo haya yana majina mengi.
1. Nyumba ya utumwa
2. Kuzimu
3. Moyo wa nchi
4. Shimo lisilokuwa na kina

Ndani ya moyo ndipo kunatoka vitu vyote vinavyotokea juu ya nchi.
Ufunuo 9: 1 “Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. 11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.”

*Neno Apolioni maana yake ni mharibifu.
Ukona ndoa imeharibika, taifa limeharibika, familia imeharibika fahamu uharibifu huo umetoka kwenye shimo la kuzimu ambamo humo ndipo kunapotoka uharibifu wote unaoendelea duniani.
Unatakiwa utofautishe kati ya ulimwengu na nchi.
Nchi ni uumbaji kama milima, bahari na ardhi. Ulimwengu ni sytem za kidunia kama system za elimu, fedha, uchumi, michezo, serikali n.k zote hizi zipo chini ya mkuu wa ulimwengu huu(ibilisi) na hizi zipo kwaajili ya kumtengenezea njia kuitawala dunia.
Isaya 24: 17 “Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.”
Zaburi 30:3 “Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.”
Isaya 14:15 “Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.”
Isaya 38:18 “Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.”
Kuna mnyama atokaye baharini na kuna mnyama atokaye katika nchi, na kuna kuzimu ya angani mbingu ya kwanza na ya pili. Kuna aina ya kwanza ya haya mashimo ya rohoni ambayo ndiyo yanayoongoza utawalwa wa mpinga kristo (kiongozi wa dini kuwafanya watu wawe vipofu) watu wengi wanapofushwa na mambo ya kidini. Watu huongea mambo ili kupofusha watu wawavune.”
Mathayo 15:14 “Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.”
Luka 6:39 “Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?”
Kuna aina nyingine ya mashimo madogo madogo ambayo nayo ni kuzimu yanaitwa mashimo ya wachawi, mashimo haya ndio yale ambayo utayafahamu pale unapomrudisha mtu anakuambia alikuwa ndani ya kabati au ndani ya dari maana yake aliuwa kwenye mashimo hayo.
Tofauti kati ya mashimo haya na mashimo ya kuzimu, ni kwamba haya yanayoendelea juu duniani yamedhihirishwa chini kuzimu na ukiyafyeka juu chini yanapotea, watu wote wanaotaka umaarufu wa siasa, kukua kiuchumi, biashara n.k yameasisiswa chini na ukishughulikia chini kuzimu na uharibifu wake, duniani kunakuwa shwari.
Wakati umeamua kushughulikia kwa kuomba kwa damu ya Yesu unaweza ukawa kama unakimbiza upepo huoni kama unatatua tatizo lako lakini pale unapoamua kufyeka yaliyotengenezwa kutoka chini kwa kusema katika jina la Yesu nafyeka naharibu nateketeza, naangamiza, navunja naponda kwa damu ya Yesu basi ni muda mfupi tu kutakuwa shwari kwenye tatizo lililokukumba.
Ni mfalme pekee ndiye anayeweza kuwatoa shimoni wale walioibiwa na kutumbukizwa humo, Yesu alipokuwa msalabani alikwenda mpaka kuzimu akamkanyaga kichwa Joka na andiko likatimia kwamba uzao wa mwanamke utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino. Kumponda kisigino maana yake ni kwamba Yesu alipigwa, alizomewa, alitaabishwa lakini hakufa kwasababu kisigino hukiwezi kuua bali aliutoa uhai wake akaenda kuzimu kuwatoa wale waliokufa watakatifu na kumponda kichwa Joka na akautwaa uhai wake siku ya tatu.Kwa maana hiyo mfalme Yesu ndiye anayeweza kutoa vyote vilivyoibiwa shimoni sababu alishafika huko.
Musa hakuwapeleka wana wa kwenye nchi ya ahadi sababu hakuwahi kufika ndio maana aliishia Jangwani, Yoshua ndiye aliye wapeleka wana wa Israeli sababu yeye alifika kule alipotumwa na Musa kwenda kuipeleleza nchi.
Yesu alikuwa mbinguni akaja duniani akaenda kuzimu akarudi duniani akakaa siku 40 akaenda mbinguni na ndiomaana anasema mimi ndimi njia ya kweli na Uzima mtu haendi kwa Baba wa Mbinguni bila kupitia mimi, pia anasema mnamwamini Mungu niaminini na mimi, nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi nami nakwenda kuwaandalia makao kisha nitakuja kuwachukua na pale mlipo na mimi nipo.
Sasa basi wachawi wao hufanya biashara ya roho na miili ya wanadamu kupitia mashimo haya. Kuna mashimo madogomadogo ambayo yanamuunganiko na lile shimo kuu la joka. Watu wengi wanaotaka kufanikiwa huenda mpaka shimoni ili wapate umaarufu sehemu wanayoitaka kwa kuuza nafsi zao kwa shetani.
Ayubu 33: 18 “Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. 22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi. 28 Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga. “
Zaburi 35:7 “Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.”
NAFSI NI NINI?
Nafsi ya mtu ina vitu kama vine.
1. Nia - (idara ya mawazo, mipango, hukumu, na Elimu ya mtu). Nia ya mtu inaweza kwenda shimoni na mtu akawa hana nia nzuri ya kuishi duniani.

2. Ndani ya nafsi ya mtu kuna utashi (mfano:- nataka kuwa daktari, nataka kuwa mtu fulani). Kama nafsi ya mtu imeibiwa basi mtu huyo unaweza kumuuliza unataka kuwa nani akakuambia vyovyote tu, mtu kama huyu ameibiwa nafsi yake ndio maana hajui kesho yake itakuaje.
3. Hisia ( kujisikia furaha, maumivu, kucheka, kufurahi, huzuni, amani,). Mtu kama nafsi yake haina furaha wala amani basi nafsi yake imeibiwa.
4. Moyo “sio wa nyama” moyo wa kujituma, kusoma, juhudi n.k.
Wachawi wanaweza kumwibia mtu nia yake na mtu akawa anasoma haelewi sababu akili yake inatumika mahali, unakuta mtu anajitahidi kusoma lakini hawezi. Nia ya mtu inaweza kuchukuliwa ukakuta mtu hana hisia ya maisha yake ya baadaye yatakuwaje unakuta mtu hana nia ya kuishi anaamua kujiua sababu nia yake imeibiwa. Unaweza kuwaona watu wepesi kukata tama sababu nia zao zimeibiwa. Neon nia maana yake ni Mapenzi, mapenzi yake yatimie, pale unapotaka kuwa mchungaji, kuwa daktari, kujenga kanisa la maelfu, kuwa waziri au raisi, ukiwa na nia ya namna hiyo sawasawa na mapenzi ya Mungu basi utafanikiwa.
Chochote kile kinachotokea mwilini kimeanzia rohoni. Macho, moyo, mikono, tumbo, miguu, kichwa cha mwilini vyote hivi vinatiwa nguvu na macho , moyo, mikono, tumbo, miguu, kichwa vyaa rohoni. Unapoona macho yanauma maana yake kuna macho ya rohoni yamechukuliwa. kama rohoni wakikamata akili mwilini akili zinakuwa hazipo usijidanganye kwamba kuna watu wenye akili sana na wengine hawana, kila mtu ana akili. Kama wameibiwa moyo au akili au tumbo wanakuwekea jini ili usife lakini roho yako inakuwepo.
Mtu wa rohoni akiibiwa moyo basi moyo wa mwilini unaanza kuharibika, alivyo mtu wan je ndivyo alivyo mtu wa ndani, hivyo basi akili za mtu wa ndani zikiibiwa basi akili za nje hazifanyi kazi, wachawi wakimwangalia mtu hawamwoni kwa jinsi anavyoonekana nje bali wanaona mtu wa ndani na mikono yake na moyo wake na akili zake na miguu yake na tumbo lake. Ukirudisha mtu wa ndani hata kama alikuwa hawezi kutembea ukirudisha miguu ya ndani basi miguu ya nje itasimama na kurudi. Kilichokufanya usikubalike kinatumika mahali na watu ili wao wakubalike ndio maana unajikuta mtu hukubaliki sababu umeibiwa.
Kwa kadiri unavyodumu kwenye dhambi ndivyo shetani anavyozidi kuendelea kutumia vitu vyako kama mikono, akili, tumbo, moyo, macho n.k. unapokuwa umeibiwa akili na moyo wako wa kiroho shetani anakufanya ubaki kwenye dhambi ili yeye aendelee kuvitumia kwenye ufalme wake ili mwisho wa siku ubaki bila kitu.
Isaya 42:22 “Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha”
Kwa jina la Yesu ninakataa moyo wangu kutumika, akili zangu kutumika kwa damu ya mwanakondoo aliyekuja akakaa kama nafsi ninakataa toka ndani yangu, nafsi yangu njoo kwa jina la Yesu, akili zangu njoo kwa jina la Yesu, moyo wangu ulioibiwa ukawekwa kwenye mashimo ya kichawi naamuru njoo kwa jina la Yesu….
Rudusha chochote kile ambacho unafikiri kimeibiwa kwako rudisha na utashangaa mipango inaanza, nia njema inaanza, rudisha vyote kwa damu ya Yesu na vyote vitarudi.

Comments