NGUVU DHIDI YA MATUKIO YA KICHAWI

Na Askofu mkuu Dr Josephat Gwajima, ufufuo na uzima
Mahali penye upofu shetani huwa na nguvu nyingi zaidi na hujitahidi kwa kila namna kusababisha matukio tofauti yaonekane ni mzunguko wa kibinadamu, amefanya watu waamini kwamba unaposema matukio haya ni ya kishetani dunia yote ikuone umechanganyikiwa na umepotea ndio maana watu wa baiolojia wana majina ya matukio haya, watu wa Sayansi wana Majina ya kuyaita matukio haya, watu wa historia wana majina ya kuyaita matukio haya.
2 Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
Fikra za watu zimepofushwa na shetani. Dunia imezungukwa na matukio mabaya ya afaya, familia, uchumi, siasa lakini pamoja hayo yote silaha kubwa ukiipata dhidi ya shetani ni kuanza kuona mtiririko wa matuko haya yanayotokea duniani sio mpoango wa Mungu.
Ayubu1:1 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana. Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.”
Tumemwona Ayubu alikuwa mtu anayemcha Mungu alikuwa ni tajiri mkubwa amebarikiwa na Mungu kwa mali na watu wengi nyumbani kwake. Kila siku nyumbani kwa Ayubu kulikuwa na siku kuu sababu alikuwa ana watoto saba na kila siku kulikuwa na sherehe kwa kila mmoja wao.
Siku moja Mungu aliongea na shetani kwamba anamwona Ayubu anavyompenda japo ana mali na utajiri mwingi na kumweshimu, lakini shetani alimjibu Mungu kwamba Ayubu anamheshimu na kumcha kwasababu umemzunguka na kumbariki ndipo Mungu akamrushu shetani aguse utajiri wa Ayubu na mali zake.
Wakati maongezi hayo yanaendelea kati ya Mungu na shetani Ayubu alikuwa hafahamu lolote linaloendelea. Ndipo shetani alimgusa akaharibu kila kitu cha Ayubu na watoto wake wote wakafa lakini Ayubu hakumkana Mungu kwa namna yeyote ile. Ndipo Mungu akamwambia shetani unaona umegusa kila kitu chake lakini bado ananipenda lakini shetani hakukubali akamwambia Mungu bado anakupenda kwasababu ya Afya yake aliyo nayo ndipo Mungu akamruhusu shetani aguse Afya ya Ayubu kwa kumwekea majipu mwili mzima.
Mungu anaweza akaruhusu upatwe na matatizo kwenye maisha yako ili umjue yeye ujifunze Neno lake, anakuita ujue kupigana anataka ufikie kwenye hatima yako kwa namna ya juu zaidi, Mungu huruhusu mabaya yakupate haimaanishi hakupendi hapana anataka ujifunze vita, si kwamba uhuzunike bali anataka uimarike utimize kusudi lililopangwa kwenye maisha yako.
Watu wanaweza wakawa hawataki usome lakini Mungu anakuona umesoma hata kama hujui kusoma, watu hawataki uoe au uolewe lakini Bwana anakuona una familia yako inayomcha Mungu. Umejaribiwa na umeshinda. Wengine wanaweza wakakuona mgonjwa au umepatwa na matatizo wakasema umemtenda Mungu dhambi na Mungu amekuacha wewe usife moyo Mungu anakufahamu tangu asili kuwa umeshinda.
Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
Ayubu alipigwa majipu mwili mzima mpaka mke wake akamshauri amwache Mungu ili afe na yeye aolewe baadaye. Inawezekana wewe uko kwenye hali ambayo watu wanaokuzunguka wanakuona kama mzigo kwao japo ni mwaminifu na unamcha Mungu, wanakudharau wewe simama imara usiwasikilize waache wazomee sababu ni saa yao ya kuzomea, waache waseme sababu ni saa yao ya kusema usiogope maneno yao songa mbele.
Hana alikuwa anachekwa na Penina sababu alikuwa hajapata mtoto lakini alipomtumaini Mungu alikuja kupata mtoto aitwaye Samweli ambaye aliisaidia Israeli yote kama Nabii wa Mungu.
Mara nyingi matukio ya kichawi yanahusiana na familia. Mfano mzuri ni tukio la kwanza la kishetani lilitokea kwenye familia ya Mungu.

Ufunuo 12: 7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”
Ilitokea mbinguni mtoto anabishana na Baba yake na Baba yake akaamua kumwambia ondoka lakini mtoto alikataa akasema siondoki tupigane, leo hii unashangaa kunini kuwa na ugomvi kwenye familia baina na shangazi na mama mdogo, baba na mtoto n.k ilianzia mbinguni, Tukio lingine Miriamu na Musa "Hesabu 12" Watu hawaogopi kwamba mtu anaongea na Mungu kila siku kwaajili yao badala yake wanagombana nae kama mtu wa kawaida, Ukiangalia tangu hesabu moja mpaka kumi na mbili Musa alikuwa akisema ni Mungu amesema. Tukio lignine ni la Daudi na mwanaye Absalom. Matukio ya kichawi yapo na yanaletwa na watu wa karibu wale wanao kuzunguka.
“Kwa jina la Yesu nashinda matukio yote ya kichawi yaliyoandaliwa kwenye maisha yangu na mtu yeyote wakati wowote kwa Damu ya Yesu.”
Ayubu japo alifikia hatua mpaka mke wake akajitenga naye lakini alisimama imara akimwamini Mungu na Biblia inasema ngozi yake ikawa laini kama ya motto mdogo (Nitakuondolea aibu yako) Mungu akambariki watoto saba wakiume na watatu wa kike baadaye Mungu akamzidishia mali nyingi zaidi ya alivyokuwa mwanzo.
Mungu anasema hatakuacha wala hatakupungukia kabisa, Mungu anazijua idadi ya nywele zako simama imara songa mbele.
Yeremia 30:17 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.”
Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.”
Mtume Paulo anasema hakuna atakaye mtenga na Upendo wa Mungu na hakuna wa kumtaabisha sababu amebeba chapa za Yesu.
Wagalatia 6:17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu”
Ukiangalia Eliya alisimamisha Mvua miaka mitatu na lakini ingekuwa leo watu wangetoa maelezo ya kigeografia, Yoshua alisimamisha dunia ili jua lisizame mpaka ashinde vita lakini ingekuwa leo wangetoa maelezo ya kisayansi.
NAMNA YA KUKABILIANA NA MATUKIO YA KICHAWI.
1. Lazima uelewe ni tukio la kichawi, kama usipolielewa utalichukulia ni la kisayansi, kiasili, nk. Jiulize kama shetani aliweza kumtupia Ayubu upele, atashindwaje kukutupia wewe kansa, atashindwaje kukutupia magonjwa ndani ya mwili wako? Tatizo ambalo mtu anakutana nalo anajarbu kuliunganisha na asili ya kisayansi, kiafya, kiuchumi, hapo huwezi kulitatua hilo tatizo.
“ Kwa jina la Yesu Mungu naomba nionyeshe kujatambua matukio ya kichawi kwa jina la Yesu”
2. Tumia maandiko kwenye kila hali inayokukumba. Kwanini utumie maandiko? -sababu Neno ni Mungu.
Yohana 1: 1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”
Mfano:-
Hesabu 23: 23 “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”

Ukisema maneno haya inamaanisha “silogwi wala silogeki”,
Biblia inasema maandiko ni upanga wa roho, silaha nyingine ni wokovu tulio nao ni kama helment ili ukianguka usiumie, ngao ya imani ni kama ukiona unataka kufa unasema Zaburi 118:17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.”, lakini ukiwa na ngao lakini huna silaha za kupigana inakuwa haina maana. Silaha zetu ni Neno la Mungu.
2 Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
Waefeso 6:11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.”
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”
Wayahudi kwa asili hawakubali kujilinda wao wanaamini kupigana na hawakubali kupigania nyumbani kwao wakiona mtu anawasema vibaya au hawapendi hata kama hajajitokeza hadharani huwa wanamfuatilia hukohuko alipo na kumpiga. Lazima ujue unatakiwa kuwashambulia adui zako hata kabla hawajaja kukuloga, usisubiri kuweka malaika wakulinde wewe anza kuwapoga wakala wote ufalme wa giza wewe fanya vita kwa jina la Bwana wa Majeshi utashangaa wakianza hata wakiwaza kukujia wanashindwa mpaka watakuita wewe mchawi kumbe umewazidi maarifa kwa nguvu za Mungu na umewashinda. Usimpe ibilisi nafasi.
Upanga huu wa Neno la Mungu haukatiki mfano “ukisema imeandikwa nimepita kutoka mautini nimeingia uzimani” wale wanaowaza kukushambulia uingie mautini wakijaribu wanafyekwa na upanga ulioutumia.
Wewe ni muumbaj pamoja na Mungu jetengeneze kiroho na kimwili kwa jina la Yesu, ni vizuri kutumia Upanga.
Isaya 54: 17 "Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana."
Nguvu kubwa juu ya matukio ya kichawi ni Neno la Mungu. Kuna silaha mbalimbali ambazo hazitafanikiwa na kumbuka wewe ni rungu la Bwana silaha za Bwana za vita unaweza kumpiga adui yako mahali popote bila kuagiza Malaika au Mungu ashuke kutoka mbinguni aje awapige adui zako kwa jina la Yesu.
Yeremia 51:20 “Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”
Usiogope sababu wewe mwenyewe ni silaha za Mungu za vita. Ukitaka kuwa na maisha mazuri usiogope hata uoga wenyewe sababu wewe ni silaha za Bwana. Neno la Mungu ni silaha ya Mungu. Ukisema katika jina la Yesu mimi ni silaha za Bwana za vita kwenye ulimwengu wa roho wewe umeshakuwa silaha.
Fanya vita na adui zako kule kule walipo haribu mawazo yao juu yako, haribu viwanda vyao vya uharibifu haribu walinzi wao na askari wao juu yako kwa jina la Yesu, Mungu akikuangalia kutoka mbinguni anakuona kama rungu lake na silaha zake za vita, unaweza ukawa silaha yeyote ile dhidi ya adui zako kwenye ulimwengu wa roho kwa jina la Yesu. Amen

Somo hili litarushwa tena Rudisha Radio Online kwa kubonyeza link ifuatayo SIKILIZA RUDISHA RADIO ONLINE MUDA WOWOTE SAA 24 KWA KUBONYEZA LINK HII YA BLUE: www.mixlr.com/rudisha-radio

Comments