USIKUBALI KUWA WAKALA WA SHETANI.

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.
Bwana Yesu asifiwe?
Wakala (agenti) ni mtumwa wa kutekeleza jambo fulani kwa niaba ya bwana wake kwa lengo fulani.
Kwa jina lingine wakala anaitwa mjumbe; na lazima alitekeleze alilotumwa kulitekeleza na bwana wake.
Kuna mawakala wa MUNGU na mawakala wa shetani ambao wanafanya kazi nuruni na gizani mtawalia.
Wakala anaweza kutumwa kupeleka; kupokea ujumbe fulani au akawa ametumwa ayatekeleze yote mawili kwa wakati mmoja.
Mawakala wa shetani hutumwa makanisani kuyasoma makanisa;kisha kuleta hali ya kuwaangusha/kuvuruga/kutawanya kama maombi mengi na utakatifu hazijazingatiwa katika Kanisa lile.
Kuna watu wengi wanaotumika kama mawakala wa shetani ila wao hawajijui kuwa wanatumika.
Kuna anayetumika kuyaangusha makanisa kwa uasherati ila hata leo bado hajajitambua.
Kuna tajiri anayetumika kuyaangusha makanisa kupitia mali yake ya kipepo na hata kufikia leo bado hana habari kuwa anatumika.
Mawakala hawadumu kwa Kanisa moja; ila huwa ni waamiji leo hapa; kesho pale kesho kutwa huko.
Wao huwa hawajijui ila nguvu ya kutumiwa na mashetani ina uwezo wa kuwaamisha kwa kisababu kidogo tu au bila sababu.
Wakala akishatimiza kusudi lake la kuangusha/ au akishindwa (kwa sababu ya maombi na utakatifu wa lile Kanisa); yeye hukimbia kulitafuta lingine ajaribu bahati.
Mawakala wengine hutumiwa na ibada ya illuminati; wachawi; majini na mizimu ya kifamilia ili kumjaribu mchungaji wa Kanisa lile au kudhoofisha uongozi; vikundi vya makanisa na kulemaza shughuli zote Kanisani.
Inabidi wewe kiongozi uwe imara kwa wokovu na utakatifu wa Bwana Yesu ili kuwashinda watumwa hawa.
Agent ana uwezo wa kukukamata kupitia kukusalimia kwa mkono; kukushirikisha vyakula na baadhi ya bidhaa; mavazi kama mtego wa kukunasa.
Huwezi kumlaumu agenti kwa maana yeye hajui; huwa anakamatwa fikra zake na shetani ili atumikishwe.
Dada/ndugu fulani anaweza kutiwa roho ya uasherati ili Kanisa lolote aingialo aweze kuwaangusha waume/wake wote.
Sio rahisi kumtambua agenti ila tu uwe mtu wa rohoni na maombi mengi ; kwani watu hawa huwa na mvuto wa juu sana.
Ukipata mtu ambaye anatumika kama agenti; mtu huyu hajaokoka na akikwambia ameombewa wokovu ujue bado hakukombolewa kutoka kwa utumishi wa giza.
Nitaliandaa somo hili siku moja nilifundishe zaidi; Ubarikiwe na kama haujaokoka; okoka sasa.

Comments