Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. |
BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze ujumbe wa Neno la MUNGU.
Kutoka 20:17 '' Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.''
Usimtamani mke wa jirani yako.
Usimtamani mume wa jirani yako.
Kutamani kitu ni kuwa na hamu ya kupata kitu hicho.
Kutamani ni kuwa na tamaa ya kitu ili ukipate.
Kutamani ni kutaka kitu ambacho sio mali yako.
Mke au Mume wa jirani yako ni mwanamke yeyote au mwanaume yeyote nje ya mkeo mmoja au mumeo mmoja.
Mke au Mume wa jirani yako sio wako, hivyo hatakiwi kukuhusu kwa lolote kwa chochote kwa habari ya mapenzi.
Ni dhambi kumtamani mke wa jirani yako.
Leo kuna baadhi ya wanaume hutamani kuwa na mahusiano na wake za watu, hiyo ni dhambi mbaya.
Leo wamama wengi hutamani kuwa na mahusiano na waume za watu, hiyo ni dhambi mbaya.
Ni hatari sana sana kuwa na uhusiano na mke wa mtu au mume wa mtu.
Kwanini Biblia imesema ''Usimtamani mke wa jirani yako?''
Ni kwa sababu wote wanaotamani wake za watu au waume za watu ni kwa lengo moja tu yaani kuwapata kimapenzi.
Ukimtamani Mwanamke kwa lengo la kuzini naye hapo unakuwa umeshatenda dhambi tayari rohoni mwako.
Biblia iko wazi sana ikisema;
'' lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. -Mathayo 5:28''
Ni dhambi kumtamani mke wa mtu ili uzini naye.
Ni dhambi kumtamani mume wa Mtu ili utake kuzini naye.
Watu wengileo ni vilema kwa sababu ya kutembea na wake za watu au waume za watu.
Wapo watu wengi tu ambao uhai wao ulikatishwa kwa sababu ya kuiba wake za watu au waume za watu.
Ni heri kila mtu akawa na mke wake mwenyewe au mume wake mwenyewe, ili kama anasumbuliwa na tamaa basi ahakikishe anamtamani mkewe au mumewe kila siku.
1 Kor 7:2-4 '' Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. ''.
Mke wa mtu ni sumu mbaya na sumu hiyo inaweza kukatisha maisha yako.
Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukupeleka jehanamu kama hutatubu.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya kilema.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya ufie gerezani.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya ufe kiroho.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya ukose mbingu.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya udhalilike kwa kutembezwa uchi mitaani.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya ufe.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya upate magonjwa.
Mke au Mume wa mtu ni sumu na sumu hiyo inaweza kukufanya uiache familia yako ingali inakuhitaji sana.
Warumi 13:9 '' Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.''
Ukimpenda jirani yako huwezi kumchukulia mkewe au mumewe.
Ukimpenda ndugu yako huwezi kutembea na mkewe au mumewe.
Ukimpenda mfanya kazi mwenzako huwezi kulala na mkewe au mumewe.
Kile usichopenda wewe utendewe hakika huwezi kuwatendea wengine.
Mika 2:1-2 ''Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao. Nao hutamani mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.''
Ole wake anayekususia mabaya.
Ole wake anayekusudia kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu.
Inawezekana kabisa kuna mke au mume wa mtu amefyatuka akili ndio maana ni yeye aayekutaka wewe. Ndugu, Napenda ujue kwamba wewe una akili timamu hivyo mkatalie maana madhara makubwa ya dhambi hiyo yanaweza kukupata wewe. Maana unaweza ukafa au ukawa kilema kwa sababu tu ya mwanamke huyo mke wa mtu asiyejitambua.
Naomba tukio la mke wa mtu kukutaka wewe kimapenzi lione tu kama ni roho ya mauti inayokufuatilia hivyo ikemee sana maana ikikupata itakuua kiroho au inakuua kimwili kabisa.
Mithali 6:27-29 '' Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe? Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue? Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia. ''
Anayechukua mke wa mtu au mume wa mtu ni kama mtu anayezima moto mkubwa unaowaka kifuani pake. Ukweli ni kwamba moto huyo lazima tu uunguze nguo zake, hayo ndio madhara ya dhambi hiyo.Kuungua nguo kunaweza kuwa ni kupigwa, au kuuawa au kuwekea kilema.
Kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu ni kukanyaga moto mwingi ambao kwa vyovyote lazima tu ukuunguze.
Tamaa mbaya siku zote huzaa dhambi.
Mithali 6:12-15 '' Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake. Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi. Basi msiba utampata kwa ghafula; Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona. ''
Kutamani mke wa mtu au mume wa mtu ni dhambi.
Kumtamani mke wa mtu kunaweza kukuletea madhara makubwa.
Kuna watu wamewahi kufukuzwa kazi nzuri za kuajiriwa, kwa sababu tu ta kutamani wake wa zatu au waume za watu.
Kumtamani mke wa mtu au mume wa mtu kunaweza kukuletea madhara makubwa kimwili na kiroho pia.
Kumtamani mke wa mtu au mume wa mtu kunaweza kukuletea hasara kubwa sana kiroho na kimwili.
Waefeso 5:3 ''Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; ''
Asante kama unanielewa ndugu yangu.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
Comments