WAISLAMU WAUWAWA KUTOKANA NA KUMTETEA MKRISTO NIGERIA

Nigeria

Katika hali ambayo inaashiria kukua kwa chuki kati ya jamii ya waislamu na wakristo nchini Nigeria, kundi la watu limewauwa waislamu wenzao kwa kudaiwa kutetea ugomvi uliohusisha vijana wa pande hizo mbili za dini Kaskazini mwa Nigeria Jumapili ya tarehe 21 Agosti 2016.
Tukio lenyewe lianelezwa kutokea wakati vijana wawili walikuwa wakibishana kuhusu dini zao, na kisha kutoka kwenye majibizano ya hadi kushambuliwa, ambapo chanzo kinaelezwa kuwa mtoto Mkristo anadaiwa kuikashifu dini ya Kiislamu.

Baada ya kushuhudia shambulizi hilo ambalo lilifanywa na kundi la vijana wa Kiislamu, msamaria mmoja Muislamu alijitokeza pamoja na Mkristo mwingine kumsaidia kijana Mkristo aliyekuwa anashambuliwa na vijana wa Kiislamu, ambapo waliwatawanywa na kusaidia kumpeleka kijana huyo hospitali, jambo ambalo lilizua hasira zaidi kwa waislamu wenzake, ambao waliamua kushambulia makazi ya mtu huyo na kisha kuichoma moto, na kupelekea watu nane waliokuwa ndani kufariki dunia. Anaeleza Askofu John Danbita wa Kanisa la Anglikan la Zafara.

Pamoja na kufanya mauaji hayo, kundi hilo lieliendelea zaidi na kushambulia makanisa matatu tofauti, wakiharibu madhabahu na vifaa vingine vya umeme. Makanisa hayo ni ECWA, Living Church na Kanisa la Anglican.

"Isingelikuwa kwa vikosi vya usalama kuingilia kati, basi madhara zaidi yangetokea", Askofu Danbita anaongeza.

Tukio hillo la mauaji na kushambulia makanisa, limetekelezwa siku moja baada ya kumjeruhi kijana wa Kikristo aliyedaiwa kumkashifu Mtume Muhammad, jambo lililochochea hasira kwa kundi la waislamu wanaotajwa kuwa wenye msimamo mkali.

Christian Post | Christian Headlines

Comments