KANISA HALISI LAZIMA LIWE ROHO MTAKATIFU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kibiblia hiki ni kipindi cha ROHO MTAKATIFU.
Ukiona kanisa halimhitaji ROHO MTAKATIFU hakika kanisa hilo linapishana na mpango wa MUNGU wa wakati huu.
Kanisa la leo la kweli linaongozwa na ROHO MTAKATIFU.
Ukiona kanisa halimhitaji ROHO MTAKATIFU ni kwa sababu kanisa hilo halitaki mpango wa MUNGU wa wakati huu.

BWANA YESU wakati anamtambulisha ROHO MTAKATIFU kwa kanisa lake alisema kwamba ROHO MTAKATIFU atakaa na sisi milele.
Yohana 14:15-17 ''Mkinipenda, mtazishika amri zangu.Nami nitamwomba BABA , naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.''

Kumbe ROHO MTAKATIFU hakuja katika kanisa la MUNGU kwa muda tu bali atakaa kwa watu wa MUNGU milele.

Kumbe kama yuko Mtume basi Mtume sahihi lazima awe na ROHO MTAKATIFU.
Kama yuko nabii basi Nabii sahihi sahihi lazima awe na ROHO MTAKATIFU.
Kama yuko Mchungaji au Askofu basi Mchungaji au Askofu sahihi lazima awe na ROHO MTAKATIFU.
Kama yuko Mwinjilisti basi Mwinjilisti sahihi lazima awe na ROHO MTAKATIFU.
Kama yuko Mwalimu wa Neno la MUNGU basi Mwalimu sahihi lazima awe na ROHO MTAKATIFU.

Watumishi hawa hawatakiwi tu kuishia kuwa na ROHO MTAKATIFU bali wanatakiwa katika kila jambo la kihuduma waongozwe na ROHO MTAKATIFU.
Anayetoa hizo huduma 5 kwa Kanisa la KRISTO ni ROHO MTAKATIFU, hivyo huwezi kuwa na moja ya huduma hiyo ndani yako harafu humtaki ROHO MTAKATIFU.
Unakuta Mchungaji anafundisha waumini wake kwamba ROHO MTAKATIFU sio muhimu. Mimi mchungaji huyo anayemkataa ROHO MTAKATIFU naona atakuwa anasumbuliwa na roho chafu za ukoo au hayo ni matokeo ya kujiita na sio kuitwa na MUNGU.`
Yeyote aliyeitwa na MUNGU anatakiwa awe chini ya ROHO wa MUNGU.
Waefeso 4:11-12 ''Naye(ROHO MTAKATIFU) alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe; ''
Ndugu yangu uliyeokoka nakuomba sana Kaa Na ROHO MTAKATIFU Siku Zote Za Maisha Yako Maana Yeye Ana Kazi Kubwa Kwako. Thamani Ya Kuokolewa Kwako Na BWANA YESU Anaijua ROHO MTAKATIFU Hivyo Usimwache Hata Siku Moja.
Ulimwengu haumtambui ROHO MTAKATIFU lakini sisi kanisa tunamtambua.
Ukiona kanisa halimtambui ROHO MTAKATIFU basi kanisa hilo liko kundi moja na ulimwengu maana ulimwengu ndio haumtambui ROHO MTAKATIFU.

Yohana 14:17 ''ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.''


Nampenda ROHO MTAKATIFU Maana Yeye Hutufundisha, Hutukumbusha Na Hutujulisha.

Tulikuwa na chapa za shetani kwa miaka mingi sana lakini siku tulipookoka Damu ya YESU KRISTO ilifuta chapa zote za shetani na sasa tukapigwa chapa ya MUNGU iitwao ''watakatifu kwa BWANA''
Na tena tukawekewa muhuri wa ROHO MTAKATIFU kuonyesha kwamba sisi ni wa MUNGU aliye hai. Hivyo ROHO MTAKATIFU ni Muhimu sana kwa wateule wote.

Muhuri wa ROHO MTAKATIFU kwa mwamini ni kibali kikuu sana cha kiMUNGU.

Waefeso 1:13 ''Nanyi pia katika huyo(YESU) mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na ROHO yule wa ahadi aliye Mtakatifu.''


Kama Kuna Mtumishi Anatumia Pepo La Utambuzi Wewe Omba Roho Ya Utambuzi Ili Umjue Na Kumuonya. Pepo La Utambuzi Ni Maroho Ya Kuzimu Yanayotumiwa Na Waganga Wa Kienyeji Au Na Mawakala Wengine Wa Shetani Ili Kuwadanganya Na Kuwalaghai Watu Wa MUNGU. Mganga Anapopandisha Mashetani Ndio Wakati Wa Pepo La Utambuzi Kusema Vitu Kumhusu Mteja, Vitu Hivyo Wakati Mwingine Vinakuwa Ni Vya Kweli. Hata Kwenye Baadhi Ya Makanisa Kuna Watumishi Mawakala Wa Shetani Ambao Wana Mapepo Ya Utambuzi Kiasi Kwamba Anaweza Kusema Yote Kuhusu Wewe Tena Yote Ya Kweli Lakini Mtumishi Huyo Ni Mjumbe Wa Shetani. Ndugu, Ni Muhimu Sana Kumuomba ROHO MTAKATIFU Akupe Kutambua Mapepo Ya Utambuzi. Muombe MUNGU Akupe Roho Ya Utambuzi Ili Umwaibishe Shetani Anayepanga Kujiinua Katika Kanisa. Ukishamtambua Mfuate Na Mwambie Aache Ushetani Wake. Arejee Kwa BWANA YESU Kwenye Usahihi Wote.
Lakini kanisa bila ROHO MTAKATIFU ni kama kuwa gizani tu maana kanisa hilo halitaweza kujua vitu vya shetani vinavyoweza kujipenyeza  katika kanisa.

 Kanisa La KRISTO Litajengwa Na Watu Wenye Moyo Haijalishi Watu Hao Wenye Moyo Ni 2, 3 Au 100. Wenye Moyo Ndio Watalijenga Kanisa La MUNGU Haijalishi Wako Wangapi ila tu wawe na ROHO MTAKATIFU ndani yao.

Tukikaa ndani ya MUNGU na MUNGU akakaa ndani yetu hapo ndipo uhusiano wetu na MUNGU muumba wetu utakuwa sahihi. Mara nyingi MUNGU hukaa ndani yetu lakini dhambi ya mwanadamu inaweza ikafuta mpango wa MUNGU wa kukaa ndani yetu.
MUNGU hukaa ndani yetu kwa njia ya ROHO MTAKATIFU hivyo mwanadamu au kanisa wakimkataa ROHO MTAKATIFU maana yake wanamkataa MUNGU.

1 Yohana 3:24 '' Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo ROHO aliyetupa. ''

YESU KRISTO Ni Mshindi, Alishinda Zamani, Anatushindia Sasa Sana Na Atatushindia Milele.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments