KUNA VITA ILI USHINDE KUNAHITAJIKA MAWE YA MUNGU YASHUKE KUWAANGAMIZA ADUI ZAKO NDIPO UTASHINDA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya ushindi.

Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Najua kwenye ndoto au kwenye maono umewahi kuona nyoka, paka au mnyama yeyote ambaye ni ashirio kwamba kuna maadui katika ulimwengu wa roho wanapanga vita juu yako au wanapigana kabisa na wewe.
Naomba leo upate ufahamu kwamba ukiona adui kwenye ulimwengu wa roho anakukimbia usifurahi na kudhani vita imeisha bali jua tu kwamba vita ya kiroho hiyo bado ipo.
Ili vita hiyo iishe wakati mwingine kunahitajika mawe ya MUNGU kuwaangamiza adui zako ndipo utashinda.

Ukiota unamfukuza nyoka haina maana vita dhidi ya kile anachokiwakilisha huyo nyoka kwamba vita hiyo imeisha.
Nyoka anaweza kuwakilisha majini, uchawi, mizimu, uganga, shetani au roho ya uongo. Hivyo ukiona nyoka kwenye ndoto hujamuua maana yake vita bado ipo na usifurahi bali ongeza maombi.
Kuna watu hupigana na adui yule yule kila siku, akija adui yule anapigwa kwa maombi lakini huyo adui akikimbia atarudi tena ndio maana vita yao haijafika mwisho bali kila siku unamfukuza tu adui ambaye huenda na kurudi.
Ndugu unahitaji mawe ya MUNGU ndipo vita yako ikome.

Hebu tuone Neno hili ambalo nimekuandalia.
Fungua nami Yoshua Sura ya kumi ili tujifunze pamoja.
Unaweza ukasoma kwa Biblia yako kuanzia mstari wa kwanza hadi mstari wa kumi na moja ila mimi nakuletea baadhi ya Mistari.

Yoshua 10:3-5,10-11 ''Basi kwa hiyo Adoni-sedeki, mfalme wa Yerusalemu, akatuma ujumbe kwa Hohamu, mfalme wa Hebroni, na kwa Piramu, mfalme wa Yarmuthi, na kwa Yafia, mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri, mfalme wa Egloni, akiwaambia, Haya, kweeni mje kwangu, mnisaidie, tuupige Gibeoni; kwa sababu umefanya mapatano ya amani pamoja na Yoshua na wana wa Israeli. Ndipo hao wafalme watano wa Waamori, mfalme wa Yerusalemu, na mfalme wa Hebroni na mfalme wa Yarmuthi na mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Egloni, wakakutana pamoja, kisha wakakwea, wao na jeshi zao zote, na kupanga marago yao kinyume cha Gibeoni, na kuupiga vita...... BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hata kufikilia Azeka, tena hata kufikilia Makeda. Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia MAWE MAKUBWA KUTOKA MBINGUNI juu yao hata kufikilia Azeka, nao WAKAFA; hao WALIOKUFA kwa KUUAWA na hayo MAWE YA BARAFU walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga ''

Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Kati maandiko hayo hapo juu tunaona Safari ya waisraeli wakitoka Misri kwenda Kaanani. Safari ya waisraeli kutoka Misri kwenda Kaanani inafananishwa na safari yetu wateule wa MUNGU Kutoka Duniani kwenda uzima wa milele.
Waisareli baada ya kupiga Yeriko na Mji mdogo korofi sana uitwao Ai hatimaye walifika Mji mkubwa sana wa Gibeoni. Mfalme wa Gibeoni alijua kabisa kwamba waisraeli hawashindwagi katika vita hivyo akamua kupatana nao na kuwapa nchi yake wakae. Katika Mji wa mbli kidogo na Gibeoni kuna Mji wa Yerusalemu ambao kwa wakati ule ilikuwa ni nchi na mfalme wake aliitwa Adon zedeki.
Mfalme huyo akamua kuwashirikisha wafamle 4 suala lake la kuwapiga vita waisraeli.
Wafalme wanne hao wakaungana na mfalme wa Yerusalemu na kutimiza idadi ya mataifa matano ambayo yalikuwa yanajiandaa kwenda kuwapiga Israeli.
Isareli nao wakapanga vita maana walijua MUNGU atawashindia tu.
Katika vita ile wale wanajeshi kutoka mataifa matano wakapigwa na Wanajeshi kutoka Israeli.
Walichoamua maadui wale wengi sana ni kukimbia mbele ya Isareli.
Kukimbia kwao hakukumaanisha kwamba vita na Isareli imesha bali walitaka kujipanga upya.
MUNGU kwa kujua kwamba alitaka Israeli ashinde na vita ile imalizike aliamua kutuma mawe kutoka mbinguni na mawe yale yaliwaangamiza maadui wote isipokuwa wafalme wale watano ambao walikuwa wamejificha katika pango lakini na wao baadae walikamatwa na kuchinjwa.
Waisraeli walikuwa na uwezo wa kushangilia baada ya kuona maadui zao wamekimbia lakini MUNGU alijua vita haijaisha ndio maana akamua kuwaua maadui za Israeli kwa mawe ndipo Israeli wakashinda.

Mwanzo mimi Peter Mabula sikuujua ujumbe huu na maana yake lakini ROHO wa MUNGU akanifundisha kwamba Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.

Zaburi 20:1-2 ''BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la MUNGU wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. ''

Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.

Kuna sababu nyingi za adui yako kukukimbia katika ulimwengu wa roho.
Adui anaweza kukukimbia na ukamuona akikimbia kwa sababu tu anataka kukuhadaa udhani kwamba vita imeisha.
Adui kwenye ulimwengu wa roho anaweza akarudi nyuma kwa sababu tu anataka umfuate na katika eneo ambalo ni baya kwako atakushambulia na kukushinda.
Anadui anaweza kukukimbia kwa lengo la kwenda kukusanya wenzake ili arudi maana atakuwa ameijua nguvu yako ya rohoni na ukubwa wake.
Adui anaweza akakukimbia ili uache maombi ukijua kwamba vita imeisha kumbe ndio kwanza vita bado ni mbichi sana.
Ndugu yangu sio kila adui anayekukukimba katika ulimwengu wa roho kwamba anakuogopa au umemshinda ila usipoangalia atarudi na kukushinda.
Ndiposa katika vita kama hiyo kunahitajika mawe ya MUNGU ili kuwaangamiza maadui zako na hapo ndipo na vita itakuwa imeisha.
Kuna watu hupambana na magonjwa kila baada ya muda, wakiomba kwa jina la YESU magonjwa yale yanapona lakini baada ya miezi kadhaa magonjwa yale yanarudi tena.
Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Kuna watu roho za madeni zinawafuatilia.
Kuna watu mikosi imekuwa sehemu ya maisha yao, huomba inaondoka lakini baada ya muda mikosi ile inarudi tena.
Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Nasema tena
Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Kuna watu mikosi huwa wakiomba inaondoka lakini baada ya muda inarudi tena.
Kuna watu balaa huwa zinaondoka kwa muda tu baada ya maombi lakini miezi kadhaa baadae balaa zinarudi.
Kuna watu migogoro kwenye ndoa huwa inaondoka kwa muda tu baada ya kuombewa lakini baada ya muda migogoro hiyo inarudi.
Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.

Zaburi 121:2 ''Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. ''

Ndugu yangu, kama kuna maadui wameshindikana kukuachia licha ya kuomba sana sasa yanahitajika mawe ya MUNGU ili kuwangamiza na vita yako hiyo itakuwa imeisha.
Mawe ya MUNGU yana macho ndio maana katika Yoshua 10:11 tunaona Biblia ikisema kwamba wanajeshi wa adui waliokufa kwa kuangukiwa na mawe walikuwa ni wengi kuliko waliouawa na majeshi ya Israeli.
Leo ita mawe ya MUNGU juu ya maadui zako wa sirini ambao huwafahamu ila wanakutesa sana.
Leo ita mawe ya MUNGU ili yawaponde maadui zako wanaokufuatalia kila siku wakijigeuza kuwa nzi au mbu.
Kuna vita ili ushinde kunahitajika mawe ya MUNGU yashuke kuwaangamiza maadui zako ndipo utashinda.
Je kuna jambo gani ambalo vita yake kwako huwa haikomi?
Leo Mwite BWANA YESU kupitia maombi yako na mawe ya MUNGU ukiyaita yatashuka na kuwaangamiza maadui zako na utashinda.

Naweza nikasema Mengi sana ila naamini kwa sehemu umenielewa na utahusika na hitaji lako ambalo unaona adui hawezi kuondoka lakini mawe ya MUNGU yatamwangamiza na vita yako itaisha na utaanza kushangilia na kufurahi mbele za BWANA YESU. Muhimu tu kwako ni utakatifu na kumwabudu MUNGU BABA katika Roho na kweli.
Kama wewe ni mtu wa michanganyo acha kuanzia leo.
Kama wewe ni mtu wa dhambi acha kuanzia leo.
Kama hujaokoka hakikisha unampokea BWANA YESU kwanza ndipo uombe maombi ya kuwatupia mawe maadui zako katika ulimwengu wa roho.
Waisraeli walikuwa na uwezo wa kushangilia baada ya kuona maadui zao wamekimbia lakini MUNGU alijua vita haijaisha ndio maana akamua kuwaua maadui za Israeli kwa mawe ndipo Israeli wakashinda.

Kwa muombaji ambaye hajazoea kuomba maombi ya vita anaweza akaomba kupitia maombi haya chini kisha akaendele na kuliendea hitaji lake mwenyewe ambao linahitaji mawe ya MUNGU ndipo hao maadui waangamie na yeye ashinde na vita iishe, lakini kwa muombaji mzoefu unaweza kuomba mwenyewe kuliendea hitaji lako ambalo unahitaji mawe ya MUNGU yashuke ili kuwaua maadui zako waliong'ang'ania.

MAOMBI YA KUITA MAWE YA MUNGU ILI YAWAANGAMIZE MAADUI ZAKO ILI USHINDE VITA.

BABA katika jina la YESU KRISTO aliye hai ninakuja mbele zako mfalme wa mbinguni nikiomba neema na rehema zako BWANA.
Nimesoma neno lako na linaonyesha wewe MUNGU ulishusha mawe ili kuimaliza vita iliyokuwa inawakabili wateule wako.
BWANA kumekuwa na maadui ving'ang'anizi katika maisha yangu ambao huenda na kurudi lakini kwa ufunuo huu MUNGU wangu naomba mawe yako yashuke na kuwaagamiza maadui hawa ili vita iishe na mimi niwe huru.
Natamani nianze kuombea mambo mengine na sio jambo moja tu ambalo adui amekuwa anakuja nampiga na anakimbia lakini baadae anarudi, ili asirudi adui huyo nimetambua BWANA kwamba yanahitajika mawe yako na yatamwangamiza na mimi nitakuwa huru sasa.
Katika jina la YESU KRISTO ninashusha mawe ya MUNGU ili kuwaangamiza maadui zangu wote wa sirini. walijificha nisiwaone na wamenitesa kwa muda mrefu lakini leo kwa jina la YESU KRISTO mawe yanashuka kutoka mbinguni na kuwaangamiza.
Ewe ugonjwa unayepona na kurudi leo nakuua kwa mawe ya MUNGU katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ewe jini la mgogoro katika uchumba wangu/Ndoa yangu sasa kwa jina la YESU KRISTO nakuponda kwa mawe ya MUNGU ambaye hakuna adui anayeweza kuyakwepa.
Ewe unayeniroga ufahamu wangu ili nisifaulu na wewe unayeiroga biashara yangu leo kwa jina la YESU KRISTO nawaponda kwa mawe ya MUNGU ambayo hakuna adui anayeweza kuyakwepa.
Enyi maadui zangu wote kuangamia kwenu ni leo kwa jina la YESU KRISTO.
MUNGU BABA na awaangamize kwa mawe kutoka mbinguni kwa jina la YESU KRISTO.
Kila adui na kokote aliko aliyezoea kunionea, leo kwa jina la YESU KRISTO nakuponda kwa mawe ya MUNGU ambaye hakuna adui anayeweza kuyakwepa.
Kila mkuu wa giza na giza lake, kila mshirikina na ushirikina wake na kila mchawi na uchawi wake na kila mganga na uganga wake nawaponda kwa mawe ya MUNGU kwa jina la YESU KRISTO.
Kama vile MUNGU BABA alivyowaangamiza adui za Waisraeli kwa mawe kutoka mbinguni ndipo leo, tena sasa, maadui zangu wote katika ulimwengu wa roho wanaangamia kwa mawe ya MUNGU kutoka mbinguni, Kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Asante MUNGU BABA kwa kunipa ushindi mkuu leo.
Maadui waliozoea kunionea leo wameangamizwa na mawe ya MUNGU kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Asante YAHWEH MUNGU wangu maana umetenda kwa utukufu wako.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi mkuu.
Amena Amen.


Asante kama unanielewa na kuomba ndugu yangu, ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments