MLANGO WA KWENDA UZIMANI NI MWEMBAMBA SANA, UNATOSHA KUPITIA MTAKATIFU TU ALIYEOKOLEWA NA BWANA YESU.


Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Mathayo 7:13-14 ( Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. )


Mlango wa kwenda uzimani ni mwembamba na anayeweza kupita katika mlango huo ni mtakatifu tu aliyeokolewa na BWANA YESU.
Wenye dhambi hawataweza kupitia katika ule mlango wa uzima, Wazinzi na waasherati hawawezi kupita katika mlango wa uzima wa milele kwa sababu mlango huo ni mwembamba sana na anyeweza kupitia ni mteule wa KRISTO tu aliyesafishwa kwa damu ya YESU KRISTO.
Wachawi na waoga wa kumkiri YESU hawawezi kupita, Wanajimu na waabudu shetani hawawezi kupitia katika mlango huo maana mlango huo ni mwembamba sana na anayeweza kupiti ni mtu wa sifa moja tu yaani kuokolewa na BWANA YESU na kuishi maisha matakatifu ya wokovu katika KRISTO YESU.
Machangudoa na wezi hawatapita katika mlango huo maana mlango huo anayeweza kupita ni aliyesafishwa kwa damu ya YESU KRISTO tu.

Wasaliti wa ndoa zao hawataweza kupita katika mlango wa uzima.
Matapeli hawataweza kupitia katika mlango wa uzima.
Watoa rushwa na wapokea rushwa hawataweza kupitia katika mlango wa uzima.
Atakayeweza kupitia katika mlango wa uzima ni yule tu aliyeokoka na kuishi maisha matakatifu duniani.


Luka 13:24 ( Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. ).

Wengi watataka kupitia katika mlango huo lakini hawataweza.
Huwezi kupitia katika mlango wa uzima ukiwa na uasherati wako, tubu kwanza leo na anza kuishi maisha ya utakatifu katika wokovu wa BWANA YESU.
Huwezi kupita katika mlango wa uzima huku unaendeleza kutegemea waganga wa kienyeji, tubu kwanza na okoka kisha ishi maisha matakatifu ndipo utaweza kupitia katika mlango wa uzima wa milele.
Mlango wa uzimani ni mwembamba sana kwa watenda dhambi maana ukitaka kupitia katika mlango huo unatakiwa uache dhambi na umpokee BWANA YESU na kumtii yeye kupitia Neno lake.
Watenda dhambi watajaribu kupitia lakini hawataweza.

Wakati watakatifu walifurahi na BWANA milele, watenda dhambi waliogoma kumpokea YESU na kutubu wao watakuwa katika giza la nje wakilia na kusaga meno.

Ufunuo 22:14-20 ''Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. Mimi YESU nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi. Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana YESU.''


Ni muhimu sana kupitia katika mlango mwembamba ambao ni wa uzima wa milele na watakaoweza kupitia katika mlango huo ni waliokoka tu na kuishi maisha matakatifu katika Bwana YESU.
Wasengenyaji na mashoga hawataweza kupitia katika mlango wa uzima kama wasipotubia uovu wao na kuokoka.
Kumbuka kutubu ni leo na sio kesho.
Watenda dhambi wote hawataweza kupitia katika mlango wa uzima maana mlango huo ni mwembamba sana na anayeweza kupitia katika mlango huo ni mteule wa KRISTO tu aliyeokolewa na kuishi maisha matakatifu.
Waongo na wachawi hawataweza kupita katika mlango wa uzima wa milele.
Makahaba na walevi hawataweza kupita katika mlango wa uzima.
Wavuta sigara,bangi na madawa ya kulevya hawataweza kupitia katika mlango wa uzima wa milele labda watubu na kuokoka na kuanza kuishi maisha matakatifu. Kumbuka kuokoka ni leo na sio kesho.

Je unataka uzima wa milele?
Kama ni ndio kwanza ni lazima umjue anayeweza kukupa uzima huo wa milele maana ni mmoja tu yaani YESU KRISTO.
Yeye katika kukuhakikishia hiloa anasema;
'' Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.-Yohana 14:6''


Kwa sababu YESU ndio njia pekee ya uzima wa milele, MUNGU BABA anashuhudia kwako leo akisema;
''Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.-Mathayo 17:5''

 
ROHO MTAKATIFU katika Biblia ameendelea kusema na kusema na kusema kupitia aliowachagua.
Hapa anasema;
'' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.-Yohana 3:16-21''


Je matendo yako ni maovu na umeendelea kujificha wakati BWANA YESU anakuita leo utubu?
Je ukiendelea kujionyesha kwamba wewe ni mtakatifu mbele za wanadamu na huko MUNGU anakuona kabisa kwamba wewe sio mtakatifu, itakusaidia nini?
Si heri umpokee BWANA YESU na kutubu na kuacha dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu?
Ndugu, hii haina siri tena ila ukweli ni kwamba wenye dhambi hawataingia katika mlango wa uzima wa milele, lakini mwenye dhambi wa aina yeyote akiamua leo kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu hakika huyo uzima wa milele utamhusu kama asipoiacha njia ya uzima abayo ni YESU KRISTO.
Bado hujaelewa ndugu?
Biblia iko wazi sana kwako wewe unayedhani una MUNGU kumbe huna MUNGU maana MUNGU aliye hai hapatikane nje na YESU KRISTO.
Biblia inasema kwako leo kwamba
''Yeye amwaminiye Mwana wa MUNGU(YESU) anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini MUNGU amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao MUNGU amemshuhudia Mwanawe(YESU).Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana(YESU), anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU(YESU) hana huo uzima.Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa MUNGU.-1 Yohana 5:10-13 ''

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments