NAMSHUKURU JEHOVAH MUNGU WANGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe.
Namshukuru MUNGU wangu amenilinda.
Zaburi 121:5 '' BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.''

 
Namshukuru MUNGU wangu amenipa uzima .
Namshukuru MUNGU wangu amenipa faida na ushindi.
Isaya 48:17 ''Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, MUNGU wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.''


Namshukuru MUNGU wangu maana nimemtegemea siku zote za maisha yangu hata uzima wa milele.
Namshukuru MUNGU wangu maana watakatifu tangu zamani walimtumaini yeye akawaokoa na sasa wako uzimani.
Zaburi 22:4 '' Baba zetu walikutumaini Wewe(JEHOVAH), Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike.''


Namshukuru MUNGU wangu maana amenitetea katika maisha yangu.
Namshukuru MUNGU wangu aweangamiza watesi wangu.
Zaburi 60:12 '' Kwa msaada wa MUNGU tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.''.


Namshukuru MUNGU wangu Amewalinda ndugu zangu na marafiki zangu.
Namshukuru MUNGU wangu Amenipa uzima wa milele katika KRISTO YESU Mwana wa pendo lake.
Yohana 3:17-18 '' Maana MUNGU hakumtuma Mwana(YESU) ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''


Namshukuru MUNGU wangu ameharibu mipango ya adui zangu wote.
Namshukuru MUNGU wangu amewaangamiza maadui zangu wote wa sirini.
Namshukuru MUNGU wangu amefuta maagano yote ya mapepo.
Namshukuru MUNGU wangu ameihukumu mizimu na uganga wote ulikaa kwa ajili ya afya yangu.
Namshukuru MUNGU wangu amenishindia katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili pia.
Namshukuru MUNGU wangu aweteketeza vikao vya uchawi vilivyokaa kunijadili.
Isaya 54:15 '' Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako. ''


Namshukuru MUNGU wangu maana hajasinzia anilindae.
Namshukuru MUNGU wangu ametuma malaika wake waanye kituo kwangu.
Zaburi 34:7-8 ''Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa. Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. ''


Namshukuru MUNGU wangu amefuta alama zote za kipepo.
Namshukuru MUNGU wangu amefinyanga upya roho yangu kwa kuondoa moyo wa jiwe na kunipa moyo wa nyama.
Ezekieli 36:26-27 ''Nami(MUNGU) nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. ''


Namshukuru MUNGU wangu amenipa ROHO wake akae ndani yangu.
Namshukuru MUNGU wangu amekuja na uzima wangu.
Namshukuru MUNGU wangu amenipa Damu ya YESU ili kila kazi ya shetani ianguke na kuteketea.
Namshukuru MUNGU wangu Maana ni muumba mbingu na dunia.
Mwanzo 1:1 ''Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi.''


Namshukuru MUNGU wangu Ni MUNGU pekee wala hakuna MUNGU mwingine bali nje na yeye kuna miungu tu.
Namshukuru MUNGU wangu maana ni MUNGU wa karibu sana na maisha yangu na roho yangu ili anifikishe uzimani sala.
Yeremia 23:23 '' Mimi ni MUNGU aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.''


Namshukuru MUNGU wangu ameleta injili ya uponyaji kwangu.
Namshukuru MUNGU wangu amelituma Neno lake ili niniponye.
amenifuta machozi.
Zaburi 107:20-21 '' Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.''


Namshukuru MUNGU wangu amegeuza aibu iliyopangwa na watu wabaya na sasa amenipa kicheko.
Namshukuru MUNGU wangu amewapiga wachawi na uchawi wao.
Namshukuru MUNGU wangu amewatowesha waganga na uganga wao.
Namshukuru MUNGU wangu amewamaliza washirikina na ushirikina wao.
Namshukuru MUNGU wangu maana namtumikia.
Namshukuru MUNGU wangu amewaua majini na kazi zao.
Namshukuru MUNGU wangu kila mipango ya giza juu ya maisha yangu imefutwa na sasa ni huru katika mkombozi wangu YESU KRISTO Mwana wa MUNGU aliye hai.
Isaya 54:17 '' Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.''


Namshukuru MUNGU wangu ameijulisha dunia yote kwamba kwake kuna uzima.
Namshukuru MUNGU wangu maana kupitia YESU KRISTO Namshukuru MUNGU wangu ameniandika jina langu katika kitabu cha uzima.
Namshukuru MUNGU wangu maana amenifunuliwa mambo nisikuwa nayajua mwanzo.
Namshukuru MUNGU wangu amenipa kushinda na zaidi ya kushinda.
Warumi 8:37-39 ''Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU BWANA wetu.''


Namshukuru MUNGU wangu ameniandalia pahali mbinguni kwenye uzima a milele.
Yohana 14:1-3 ''Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi(YESU). Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.''


Namshukuru MUNGU wangu amefuta ukungu wote wa kipepo ulioelekezwa katika maisha yangu.
Namshukuru MUNGU wangu ameniondolea kila roho za uharibifu zilizotumwa katika maisha yangu.
Namshukuru MUNGU wangu amekuwa MUNGU wangu na mshindi wangu wa daimaTena ndiye MUNGU wangu Milele.
Zaburi 83:18 ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''

 
Dunia nzima leo jueni ya kwamba MUNGU wa kweli ni mmoja tu naye ni JEHOVAH MUNGU aliye hai.
JEHOVAH yu juu ya yote na juu ya vyote.
Ndugu uliyesoma ujumbe huu ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments