Na counselor Nicholaus Simon. |
MADHABAHU ni mahali rasmi ambapo watu au mtu hutumia kufanya ibada kwa Mungu au mungu ambaye ndiye mwabudiwa. Kuna utofauti kati ya mungu wa herufi ndongo na Mungu huyu wa herufi kubwa ya mwanzo , huyu ni mungu wa dunia hii ambaye hakuumba mbingu na nchi ,ila Mungu wa herufi kubwa ya mwanzo huyu ndiye Mungu muumbaji.
Kutoka 20:2-3 ‘‘Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miung mingine ila mimi. ”
MUHIMU: usitumie herufi ndogo mwanzoni unapo andika kumwakilisha Mungu wa muumbaji, ni kosa kubwa sana.
IBADA HUJUMUISHA YAFUATAYO; Kuadhimisha, kutoa sifa , kutoa sadaka ,kuomba na kumtumikia Mungu au mungu.
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani , na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israel, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyo andikwa katika toati ya Musa , mtu wa Mungu. Ezra 3:2
AINA ZA MADHABA
(i) Madhabahu ya Mungu wa mbinguni.
Je Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu.Yakobo 2:21.
Hii ni madhabahu ya kweli ambayo ndiyo iliyo sahii kwa mtu aliye mwamini Yesu kuijua kwa undani zaidi.
(ii) Madhabahu za kishetani. Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene , katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari mambo ya dini. Kwasababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya Ibada yenu, naliona madhabahu iliyo andikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYE JULIKANA. Basi mimi nawahubiri habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Matendo 17:22-23.
Ni dhahiri kwamba mtume paul aliyo iyona ni madhabahu ya kishetani ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu wa Kweli. Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.1korintho10:14-22. Ibada ya sanamu ni ipi? ni ibada inayo fanywa kwa mungu wa dunia hii, ambaye ni shetani.
HIZI NI BAADHI YA MADHABAHU ZA KISHETANI.
(a) Madhabahu za maji. Unaweza kuwa shahidi katika jambo hili yapo baadhi ya makabila ndani ya Nchi hii ya Tanzania na nchi nyingi duniani. Ambao hufanyia baadhi ya Ibada kwenye mito, baharini, maziwa na mabwawa katika maeneo haya watu huenda kutoa sadaka, au huita kutambika. Tambua maji yanasikia kwahiyo upo uhusiano mkubwa katika ulimwengu wa roho kati ya maneno yanayo tamkwa kipindi cha kutoa sadaka. Tusome 2wafalme 2:19-22 Watu wa mji wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama Bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akaseme,Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
(b) Misitu na miti mikubwa. hii pia hutumika kama maeneo ya kufanyia Ibada za kishetani ambazo huusisha utoaji wa sadaka.
(c) Njia panda. Hili si geni kwa watu wengi katika miji na vijiji pia limekuwa likifanywa , kwa kutumia njia panda kama sehemu ya kutoa sadaka mbalimbali mfano; Nazi kuvunjwa, vibuyu kuvunjwa.
(d) Nguzo maalumu na minara. Haya yote yamekuwa maeneo ya kutolea sadaka katika miji mikubwa ambayo hasa vizazi na vizazi hulithi utamaduni huu.
(e) Milima. hasa milima mirefu hutumika kama maeneo muhimu katika Ibada za kishetani, na tambua kwamba tunapo ongelea ibada, Hakuna ibada pasipo kutoa sadaka. Swali ni kwamba sadaka hiyo inatolewa kwa nani ?
(f) Madhabahu za mateso.
Hizi humilikiwa na watu mfano, Wachawi, Waganga, Wanajimu na makuhani wa sanamu, hawa wote wanakuwa na kibali cha kipepo katika kuendesha ibada hizo ila kwa lengo la kutesa maisha ya watu tu.
Kazi yao ni kutengeneza Madhabahu hizo kwa ajili ya kupeleka Nguo, Majina, Picha,Vitu ,Fedha na visanamu vya watu wanaotaka wawatese. sababu hii hupelekea watumishi wa Mungu kuwafundisha sana, wakristo kuwa makini katika maisha yako ya kila siku ,una kula nini? Una vaa nini? Una ongea nini? yote haya katika ulimwengu wa roho yana umuhimu na yanaweza kumuonganisha mkristo hata yeye pasipo kujua.
Pamoja na kuangalia mfumo wa madhabahu za kishetani iko nguvu zaidi kwa madhabahu ya Mungu wa mbinguni. Mfano Elia na manabii. 1Wafalme 18:30-35, Jitahidi sana kuisoma habari hii yote na utaona jinsi ambavyo madhabahu ya ki-Mungu ilivyo na nguvu , ambazo ziliweza kumdhihirisha kuwa yeye ni Mungu mkuu.
MUHIMU: pasipo madhabahu hakuna msingi imara wa kiroho.
FAHAMU HATUA ZA KUJENGA MADHABAHU.
Jambo la kwanza fahamu ,Madhabahu zote za ki-Mungu lazima ziungamanishwe na kanisa lililopo hapa duniani.
Madhabahu yaweza kuwa ya mtu mmoja au kikundi cha watu wengi.
Mfano, Agano la kale Ezra 3:5 walitumia hasa kuchinja wanyama , ila kwa Agano jipya utaratibu hasa sa ni sadaka pasipo damu ya wanyama. Ila unaweza toa ; Pesa ,mnyama au kitu chochote
FAIDA YA MADHABAHU YA KI- MUNGU
(i) Huweka upatanisho (msingi)
Madhabahu ya ki-Mungu pale mwamini anapotoa sadaka, jambo la kwanza ni “UPATANISHO”
Mwanzo 18:6-10 ili Upatanisho uwe dhahiri ni endapo tu kutoa kutakuwa kwa moyo wa kupenda. Mfano unapo soma maandiko hayo yanaonyesha Baba wa Imani akifanya kwa kupenda na si kulazimiswa na watu, Ibrahimu alijua siri.
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia , Ee Ibrahimu, Naye akasema , Mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye , Isaka , ukaende zako mpaka nchi ya moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu yam mlima mmojawapo nitakaokuambia. Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa. Mwanzo 22:1-3.
Kiukweli si kwamba Ibrahimu jambo hili katika hali ya kibinadamu lilikuwa lahisi kwake, ila mtumishi wa MUNGU huyu alijua maana ya madhabahu, Madhabahu unapo jenga huanzia rohoni kwanza kwahiyo pale alipo kubali kumtoa Isaka Kuwa sadaka ya kuteketezwa tayari alikuwa amejenga.
MUHIMU: Kwa kila jimbo, ulifanyalo kuwa makini katika kujenga Madhabahu.
(ii) Hufungulia Baraka.
Kupitia Madhabahu ya Mungu wa Israel, inaleta baraka za haki isivyo kawaida.
Ukisoma, Mwanzo 22:15-18 ''Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni. akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.''
Katika maisha yako ya kawaida jitahidi kabla ya kuomba Baraka, fanya kitu kwanza mbele za Mungu.
Soma maneno haya pia utaona jinsi Mungu anavyo toa maagizo kwa balaamu kuwa akanene na Baraki.Hesabu 23:16-20
Jitahidi upitie vifungu hivi pia vitakavyo kujenga sana juu ya baraka za KiMungu.
''na Baraka hizi zote zitakujulia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani'' Kumb 28; 2, 8.
''Atawabarikia wamchao BWANA, Wadogo kwa wa kubwa.'' zaburi 115:13
Atukuzwe Mungu , Baba wa Bwana wetu Yesu kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni , katika ulimwengu wa roho, ndani yake kristo. Efe 1:3
MUHIMU: tambua mambo ya rohoni huzaa na baadaye huja ya kimwili. Galatia 3:9 Unapofanya jambo hili Imani huitajika sana.
Tulio mwamini Yesu, wote tumebarikiwa ili kuzifanya Baraka ziwe dhahiri maishani mwako LAZIMA UFANYE KITU. Matendo ya mitume 3:25-26. ''Ninyi mmekuwa watoto wa Manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na Baba zenu, akimwambia Ibrahimu, katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.''
(iii) Ulinzi wa Ki-Mungu.
Tambua Mungu wetu ni Mungu wa Maagano huachilia ulinzi katika maisha ya mtu kwasababu pale anapo mtazama mtu huyo huona “AGANO”. Mfano, ukisoma mandiko haya yote yanazidi kuonyesha faida ya maagano. Nuhu, Mwanzo 6:18, 9:11. ''Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe na wanao, na mkeo na wake za wanao, pamoja nawe. na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika , baada ya hayo, kuiharibu nchi.''
Maandiko yote haya yanaonyesha kuwa kupitia sadaka huweka agano ambalo Mungu huliangalia hilo kwa kipindi kirefu sana.
Ibrahimu, Mwanzo 17:4 ''mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.'' Mungu wetu ni Mungu wa Maagano yeye huweka na hilo agano hudumu kwa kipindi kirefu sana, unapo toa sadaka inakuwa agano mbele za Mungu ambalo hudumu kwa kipindi kirefu sana.
Kumb 29:25 ‘‘Ndipo watakaposema watu, ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri’’.
(iv) Humkumbusha Mungu. Jambo hili ni siri kubwa sana, Madhabahu huongea yaani Inasema mbele za Mungu. Zaburi 106:45 ''Akawakumbukia agano lake ; Akawahurumia kwa wingi wa fadhiri zake.''
Ufunuo 16:7a.''Nikasikia hiyo madhabah ikisema'' Kwahiyo katika maisha ukiwa kama mwamini unapo kuwa na tabia ya kujenga madhabahu kwa mambo uyafanyayo ,kwasababu kutokana na shughuri mbalimbali za kimaisha upo wakati utasahau wewe binafsi kama ulifanya kitu mbele za Mungu, ila Hiyo Madhabahu “ITASEMA MBELE ZA MUNGU KWAAJILI YAKO”
(V) Humdhiirisha Mungu au humfunua. 1wafalme 18:22, 32-38 ukisoma vizuri na kwa umakini utagundua kuwa ugomvi au ubishani uliokuwepo kati ya nabii Eliya na Manabii wa Baali ulikuwa nani Mungu wa kweli kati ya Mungu wa Eliya na wao Baali, ubishano wao ulikuwa mkubwa sana ambao usingwezwa kuisha kwa uhalaka kwasababu IMANI ni kitu cha thamani kwa mtu aliye nacho ,pale anapo amini juu ya jambo fulani si kwa ulahisi unaweza mwambia usiamini, ni mpaka pale UDHIHIRISHO unapo tokea. Kwahiyo Nabii Eliya akawaambia ‘‘kwa hiyo na watutolee ng’ombe wawili; wao na wajichagulie ng’ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza ng’ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni,wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu”.
Kiukweli katika maneno hayo, kinacho tamkwa ni kwamba LEO NA TUONE NANI ALIYE WA KWELI KATI YA mungu au MUNGU.
KITU CHA KUFANYA
Kama hukuwahi kujenga madhabahu jitahidi kujitoa kwanza kwa kujengea vitu vyako vyote ukianzia ,watoto wako, ndugu kiujumla. elimu ,biashara ili uviungamanishe na Mungu, pia baada ya kuyajua yote haya ,JITAHIDI UYAFANYIE KAZI NA MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI.
Ni mimi ndugu yako; counselor Nicholaus Simon.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
0766-635382/0654-623492
nicholaussimon3@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.
Comments