VIKWAZO USIKUBALI VIKAKUONDOLEA UTAKATIFU WAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze.
Je, Unajua Kwamba Kuna Watu wabaya Wanatafuta Faida Kwako? 
Watu Hao Wanaitumia Faida Hiyo Kukusema Vibaya. 
Wanatafuta faida kwako na wakiipata faida hiyo wanaitumia kukufukuzisha kazi.
Wanatafuta faida kwako ili wakiipata faida hiyo waitumie kukuvunjia uchumba wako au ndoa.
Wanatafuta faida kwako na wakiipata faida hiyo wanaitumia kukumaliza kiuchumi. 

Tito 1:10 '' Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ''
 
Jihadhari Na Watu Wabaya Unaowapa Siri Zako Ili Waje Wazitumie Siri Hizo Kukusema Vibaya Baadae au kukuangamiza au kukuharibia baraka yako. Uwe Makini Maana Sio Lazima Kila Mtu Umweleze Siri Zako.
Jambo hilo ni moja tu ya vikwazo katika vikwazo vingi ambavyo unapaswa kuvishinda.
Siri zako unazowaambia baadhi ya watu zinaweza kuja kuwa vyanzo vya vikwazo katika sehemu fulani ya maisha yako.
Sio kwamba usiwaambie watu siri zako lakini usiwaambie wati wote siri zako. Hakikisha unamweza mtu siri yako kwa faida na sio hasara. Mweleze mchungaji siri yako ili akuombee, Mweleze baba yako au mama yako ili akusaidie kiushauri. Waeleze watu uliowathibitisha kwamba ni wema ili wakusaidie. Kuna mambo ukiendelea kuyaficha hutafanikiwa wala hutavuka kutoka hapo ulipo lakini angalia sana watu wa kuwaeleza siri zako maana wengine wanaweza kuchukua hizo siri zako kuwa faida kwao kwa ajili ya kukumaliza.
Inawezekana kabisa sasa unasumbuliwa na vikwazo ambavyo ulivisababisha wewe mwenyewe kwa kuwaambia siri zako watu wasio sahihi, Leo shinda vikwazo hivyo kwa jina la YESU KRISTO.
Kama unaficha jambo ambalo ni la dhambi hakika huko ni kujiangamiza maana hutafanikiwa, ila kama ni jambo lako jema unaweza ukawaficha baadhi ya watu ili usiwape faida ya kukuharibia.

 ''Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. -Mithali 28:13''
 
Kuna vikwazo vingi ambavyo unatakiwa uvishinde.
Vikwazo utavishinda kwa maombi pamoja na kubadilika mfumo wako wa maisha. Usikubali kuwapa faida watu wabaya ili faida hiyo waitumie kukuangamiza.
Kuna wengine vikwazo vyao ni kushindwa kumngoa BWANA.
Unakuta binti baada ya kukaa muda mrefu bila kuolewa anaamua kufumba macho ili yeyote atakayemjia atamkubali na kuolewa naye, hicho kinaweza kuwa kikwazo kibaya baadae.
Kuna ambao kwa kwenda kichwakichwa walijikuta wameolewa na wachawi au majambani na kuingia katika matatizo makubwa zaidi.
kama MKRISTO uliyeokoka unatakiwa umngoje BWANA kwa maombi na utakatifu na utumishi maana baraka yako ipo tu na itakuja siku moja..
Kiwango Cha Juu Sana Cha UchaMUNGU Wa Mtu Ni Kumngoja BWANA Hata Katika Magumu, Kumwamini MUNGU Hata Unapojaribiwa Au Unapopitia Magumu. 
Je Kwa Sasa Una MchaMUNGU Kwa Kiwango Hicho?
Ndugu shinda vikwazo vyote huku ukimcha MUNGU.
Ayubu 5:19-22 ''Yeye(MUNGU) atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa. Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga. Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja. Wewe utayacheka maangamizo na njaa; Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.''

Ni muhimu pia ukawa mwaminifu kwa MUNGU wakati wote.
Ukiwa Mwaminifu Kwa MUNGU Ni Lazima Tu
Utapata Upendeleo Kwa MUNGU Na Kwa Wanadamu.
Ndugu shinda vikwazo vyote huku ukiwa mwaminifu kwa MUNGU.

Mithali 28:20 ''Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.''

Wakati wa magumu pia ni muhimu sana kukumbuka kwamba Ni Lazima uwe Na Ushirika Na Huyu YESU Aliyekuokoa. 
2 Kor 13:14 '' Neema ya Bwana YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ukae nanyi nyote.''
Kuwa Na Ushirika Na KRISTO Ni Kudumu Katika Fundisho Lake Na Kulitii. Ushirika Wetu Na MUNGU Ni Wa Muhimu Sana Ili Tupate Nguvu Za Kusonga Mbele Katika Maisha Ya Wokovu. Ukiona Mtu Anayumbayumba Katika Kuhudhuria Ibada Au Katika Kiroho Chake Ni Kwa Sababu Hana Neno Ndani Yake Na Hiyo Kupelekea Ushirika Wake Na KRISTO Uyumbe.
Ndugu shinda vikwazo vyote huku ukiishi maisha matakatifu.

Warumi 8:35-39 ''Ni nani atakayetutenga na upendo wa KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU Bwana wetu. ''

Kuna Vitu Vinaweza Kuja Kwako Ili Tu Kubadili Ratiba Yako Ya Ibada, Lakini Mteule Halisi Wa KRISTO Huwa Habadilishwi Na Chochote Katika Kumcha BWANA, Hata Katika Magumu Bado Humtii BWANA Na Kumngoja BWANA.
Ndugu shinda vikwazo vyote huku ukimcha BWANA.

 Kuna Vitu Vinaweza Kuja Wakati Fulani Maishani Mwako Ili Tu Kubadili Ratiba Yako Ya Kumpenda BWANA, Lakini Wateule Halisi Wa KRISTO Humngoja BWANA Hata Katika Magumu.
Ndugu shinda vikwazo vyote huku ukiongeza utakatifu.


 Utakatifu Ndio Msingi Wa Wokovu Wa Mteule Wa KRISTO. Kama Mkristo Akiacha Kuishi Maisha Matakatifu Maana Yake Ameubomoa Msingi Wa Nyumba Yake(uzima Wa Milele) Kiasi Kwamba Asipotengeneza Tena Huo Msingi(utakatifu) Basi Nyumba(uzima Wa Milele) Nayo Haitakuwepo.
Ndugu shinda vikwazo vyako vyote huku ukiendelea na wokovu wa KRISTO.
Wakolosai 2:6-10 ''Basi kama mlivyompokea KRISTO YESU, BWANA, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya KRISTO. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. ''
 
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments