JE WEWE NI MTAUWA?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tunaangalia jinsi ya kuwa mtauwa.
Je wewe ni Mtauwa?
Utauwa maana yake ni ucha MUNGU.
Mtauwa maana yake ni mtu anayemcha MUNGU kwa moyo wote na kwa dhati.
Kuna maandiko 17 yanayolitaja Neno ''Utauwa'' katika Biblia ya kiswahili na kuna Maandiko 23 yanayolitaja Neno ''Mtauwa'' katika Biblia ya Kiswahili.
Kwa sababu utauwa maana yake ni ucha MUNGU basi  maana nyingine ya utauwa tunaweza kusema ni utakatifu.
Utauwa huanzaje katika maisha ya mwanadamu?
Biblia inajibu ikisema;
'' Na bila shaka siri ya UTAUWA ni kuu. MUNGU alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.- 1 Timotheo 3:16'' 

Je wewe ni Mtauwa?
 Siri ya utauwa ni kuu maana utauwa huanzia katika kumjua YESU KRISTO ambaye ndiye mwokozi kisha unachukua hatua ya kumpokea kama Mwokozi wako.
Ukimpokea YESU kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu katika yeye, wewe hapo unakuwa mtauwa.
Kumbuka kuokoka ndio mwanzo wa kumwabudu MUNGU katika Roho na kweli.
Hakuna Mtauwa nje na Wokovu wa YESU KRISTO.
MUNGU hawezi kuwaacha watauwa wake bali amewaandalia uzima wa milele, Lakini wanaokataa kuishi maisha ya utauwa katika KRISTO YESU wataangamia.

Zaburi 37:28 '' Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.''

Je wewe ni Mtauwa?
 Sio kila mtu ni mtauwa lakini inawezekana kuwa mtauwa kwa kuamua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha mataktifu ambayo kwa jina jingine Biblia inayaita maisha ya utauwa.

Je wewe ni Mtauwa?
 MUNGU anawapenda watauwa wake ndio maana huwaokoa na kila hila za shetani.

2 Petro 2:9 '' basi, BWANA ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;''

Je wewe ni Mtauwa?
= Maisha ya utauwa ni maisha ya kuanza na YESU na kumaliza na YESU.
Wakolosai 2:6 ''Basi kama mlivyompokea KRISTO YESU, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;'' 

Je wewe ni Mtauwa?
= Maisha ya utauwa ni maisha ya kuishi kwa ROHO MTAKATIFU na kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
Wgalatia 5:25 ''Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.''

Je wewe ni Mtauwa?
= Maisha ya utauwa ni matakatifu na yanaendelea kuwa matakatifu daima.
1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''

Je wewe ni Mtauwa?
 Kama umempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako basi yakupasa sana kuishi maisha ya utauwa katika yeye.
Maisha ya utauwa ni maisha ya ucha MUNGU.
Maisha ya utauwa ni maisha matakatifu.

Je wewe ni Mtauwa?
 Kila mteule wa KRISTO inampasa sana kuishi maisha ya utauwa.
Watauwa sio wazinzi wala waongo.
Watauwa sio wasaliti wa ndoa zao wala sio wanywa pombe.

Je wewe ni Mtauwa?
Inakupasa sana ndugu uishi maisha ya utauwa  katika KRISTO.
Watauwa sio wavaa nusu uchi wala sio wasengenyaji.
Watauwa hutoa fungu la kumi na sadaka.

 Je wewe ni Mtauwa?
Inakupasa sana ndugu uishi maisha ya utauwa katika KRISTO.
Watauwa sio watoa mimba na tena sio wazinzi wala waasherati.
Watauwa sio wezi wala sio walipiza visasi.

 Je wewe ni Mtauwa?
Watauwa husamehe na wala sio wenye viburi kwa MUNGU.
Inakupasa sana ndugu yangu uishi maisha ya utauwa katika YESU KRISTO Mfalme wa uzima wa milele.

 Je wewe ni Mtauwa?
Ndugu yangu nakuomba jizoeze kuishi maisha ya utauwa.
Utauwa ndio utakatifu wenyewe, ishi maisha mataktifu katika KRISTO YESU Mfalme wa uzima wa milele.

1 Timotheo 4:8-9 ''Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye. Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;'

Kanisa la MUNGU linapaswa kuishi maisha ya utauwa.
Watumishi wa KRISTO YESU  wote kokote waliko wanatakiwa kuishi maisha ya utauwa.
Wazee wa kanisa na mashemasi na viongozi wengine wote kanisani wanatakiwa sana kuishi maisha ya utauwa.
 Wanakwaya na waimbaji wote wa nyimbo za injili wanatakiwa kuishi maisha ya utauwa.

Zaburi 30:4 '' Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.''

Je wewe ni Mtauwa?
 BWANA YESU alifanya kazi kubwa sana pale msalabani, aliutoa uhai wake ili atuokoe mimi na wewe.
Baada ya BWANA YESU kutuokoa yamebaki mambo mawili  tu kwangu na kwako ndugu, yaani kuishi maisha ya utauwa katika yeye pamoja na kumtumikia yeye.
 
Zaburi 31:23-24 '' Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele. Iweni hodari, mpige moyo konde, Ninyi nyote mnaomngoja BWANA.''
 

 Utauwa hutunzwa  hivyo ndugu yangu utunze utauwa wako katika YESU KRISTO.
Ulipompokea YESU uliongozwa sala ya toba. Sala hiyo ya toba ni maungamo yanayokupatanisha wewe na MUNGU Muumbaji wako. Baada ya sala hiyo kinachokupasa wewe ni kuishi maisha ya utauwa katika YESU KRISTO.
Maisha ya utauwa ni maisha matakatifu.
Kumbuka vya dunia vyote vitapita lakini mtauwa wa BWANA YESU ataenda uzima wa milele.
Ndugu tazamia uzima wa milele kwa kuamua kuishi maisha matakatifu ambayo ni maisha ya utauwa katika YESU KRISTO.

2 Petro 1:3-11 ''Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na UTAUWA, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu UTAUWA, na katika UTAUWA wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu YESU KRISTO. Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu YESU KRISTO.''

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments