JICHUNGUZE TABIA YAKO:

Na Mtume na Nabii Josephat Mwingira

Kila eneo katika Maisha ya Mwanadamu linahitaji aina Fulani ya TABIA na TARATIBU zinazowezesha kumpatia USHINDI. Tabia ni roho kamili inayoweza Kumsababishia Mtu KUFANIKIWA au KUSHINDWA katika Maisha ya KIROHO na ya KIMWILI. Ili ufanikiwe ni Muhimu kujenga TABIA SAHIHI na Kuzingatia TARATIBU Zinazotakiwa. Mfano kuna TABIA na UTARATIBU wa Kufanya:
- Biashara.
- Kufanya Kazi Ofisini.
- Kuishi katika Ndoa.
- Kutenda Kazi ya MUNGU.
- Kuwa Wacha – MUNGU.
- Na Kadhalika.

Ili mtu aweze kupata BARAKA alizokusudiwa na MUNGU inambidi kujenga TABIA NZURI kwa JUHUDI zote huku Akitenda Matendo yenye KUMPENDEZA MUNGU na Wanadamu.
Sasa anza KUJICHUNGUZA Wewe;
- TABIA zako na UTARATIBU wako kwenye Ndoa yako Ukoje? Unamfurahisha MUNGU? Unamfurahisha Mumeo au Mkeo?
- TABIA zako na UTARATIBU wako kwenye KUMCHA MUNGU Ukoje? Bado umeokoka lakini una Sengenya watu, Wewe ni Mtu wa Kulalamika tu, Wewe ni Mchoyo, Unasema Wenzio Vibaya, Unapenda Mabaya kwa Wenzio, Unasababisha Fujo na Chuki Kanisani, Zone na Eneo lako, Wewe ni Muongo, Wewe ni mzinzi na muasherati, Unatukana matusi, Wewe ni mnafiki, Wewe ni mchafu?
- TABIA zako na UTARATIBU wako kwenye Kutenda Kazi ya MUNGU Ikoje? Unajituma, Unabidii kwenye Kazi ya MUNGU, Unahudhuria Taratibu za Kukutana kama Mlivyoagizwa, Au wewe ndio chanzo cha Uharibifu kwenye Kazi ya MUNGU, Unasababisha Wenzako Wasitumike Ipasavyo, Unatii Viongozi wako, Unashirikiana na Wenzako vizuri, Unawajibu vema Wenzako, Una Kiburi na Kujiona na Kujiinua, Je una Tabia ya dharau?
- TABIA zako na UTARATIBU wako kwenye kufanya Kazi Ofisini Ukoje? Je unawahi Ofisini kwa Wakati, Unajituma Kazini au ndio ukifika Wewe ni Kusikiliza Muziki, kuangalia kutazama Video ofisini Siku nzima, Wewe ni Kusoma magazeti ya Umbeya, udaku na n.k. siku nzima badala ya kufanya Kazi uliyoajiriwa au uliyojiajiri, Wewe ni Mtu wa kuzungumza, kuongea tu mambo ambayo hayana maana kutwa nzima na Kazi wala hufanyi, Wewe ni mtu wa kuchat tu kutwa nzima na Kazi wala hufanyi ikupasavyo?

JICHUNGUZE TABIA YAKO, JICHUNGUZE TABIA ZAKO, Amua kuwa na TABIA NZURI huku Ukitenda Matendo yenye KUMPENDEZA MUNGU na Wanadamu.

Comments