![]() |
Patience Ozokwori a.k.a Mama G kampa Kristo maisha yake |
![]() |
Majid akimuombea mtu ibadani hii sio maigizo ni kweli |
Mama G nyota wa Nigeria katika ugizaji ambaye asilimia 90 ya filamu
alizoigiza ni za ukatili kama mama mkwe au uchawi, aliamua kumpa Kristo
maisha yake mapema mwaka huu na kufanyika baraka kwa waigizaji wengine
akiwemo Majid Michael kutoka Ghana ambaye alihubiriwa na mama G nakuamua
kuokoka na sasa amebarikiwa na kuwa mchungaji rasmi. Licha ya mama G
lakini pia kuna orodha ya waigizaji wengine watano wa Nollywood ambao
kwasasa wameokoka na kuamua kujikita kwenye injili.
Aidha kwa upande wa mwanamama huyo yeye amesema licha ya kuokoka lakini
hajaachana na uigizaji kwakuwa Mungu hajamwambia aachane na suala hilo,
na kupinga taarifa za watu zilizosambazwa kwamba baada ya kuokoka hataki
tena kuitwa mama G, mwigizaji huyo amesema si kweli na kwamba mtu
yoyote akimwita kwajina hilo ataitika kama kawaida kwasababu amepewa na
mashabiki wake na haoni tatizo kulitumia. Taarifa zaidi za waigizaji
waliokoka akiwemo Majid Michael ambaye inadaiwa ana upako wa pekee toka
siku nyingi, na hivi sasa pia amejikita katika uinjilist.
Source:Gospel Kitaa
Comments