MAOMBI YA KUFUTA MAAGANO YOTE YA KIPEPO YALIYOAMBATANISHWA NA JINA LAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya ushindi mkuu.
Leo tunafuta kila maagano ya kishetani yaliyoambatanishwa na majina yetu kisha tunafanya agano na damu ya YESU KRISTO.
Jina ni nini?
Jina ni alama ya kipekee uliyopewa wewe inayokutofautisha na wengine.
Jina lako linaweza likaambatana na laana au balaa mbalimbali.
Ndio maana Biblia inasema kwamba;
''Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.-Mithali 22:1''


Jina lako ni la muhimu sana.
Jina lako ndio wewe. Jina lako linaweza likabebeshwa uganga wa kienyeji tangu utotoni au tangu hujazaliwa kiasi kwamba unatamani kuwa mganga wa kienyeji. Ndugu mmoja aliniambia kwamba wazazi wake walipanga tangu zamani kabla hajazaliwa kwamba ataitwa jina alilonalo na atakuwa mrithi wa zana za uganga katika ukoo wao. Alipozaliwa alipewa jina lakini hakujua jina hilo limebeba nini. Kuna wakati kwenye maono alikuwa anaona nyoka akimulaumu na wakati mwingine nyoka huyo akimuelekeza kwamba aende porini akajimbe mtu fulani. Ndugu yule mwanza alikuwa anakataa lakini baadae alijishangaa anatamani kuwa mganga wa kienyeji. Katika kipindi ameamua kuwa mganga wa kienyeji ndicho kipindi alikutana na somo langu mtandaoni linalokataza kuwa mganga wa kienyeji. baada ya somo hilo ndipo aliponitafuta na kujijulisha. Nikamwambia kwamba nyoka aliyekuwa anamwelekeza ni mizimu ya ukoo ambayo inataka awe mganga kama walivyokubaliana wazazi wake na babu zake. Tuliomba kufunja mipango hiyo ya shetani na akawa huru. Jina lako linaweza kubebeshwa machukizo ndio maana usipokuwa na YESU unaweza ukajikuta unayaishi machukizo hayo.
MUNGU katika Bilia aliona jina Abramu halitimizi kusudi lake ndio maana Abramu akaitwa jina jipya na MUNGU kwamba awe Ibrahimu na simu Abramu. Sarai naye akaitwa Sara maana sarai ilikuwa haitimizi kusudi la MUNGU. Ibrahimu maana yake ni baba wa mataifa mengi na sara ni binti mfalme, lakini Abramu ina maana nyingine na Sarai ina maana nyingine ambazo hazikuwa zinatimiza kusudi la MUNGU.

Mwanzo 17:5, 15 '' wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. MUNGU akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.''

Jina lako linaweza likaambatanishwa na mikosi hivyo leo ita damu ya YESU KRISTO ili ifute maagano yote ya kishetani yaliyoambatanishwa na jina lako.
Kumbuka majina mengi chanzo chake ni maneno yaliyonenwa kuambatanishwa na jina hilo. Mnenaji wa neno hilo ndio anayejua kusudi la jina hilo ndio maana tunatakiwa sana tutakaswe kwa damu ya YESU ili kuondoa kila kazi ya shetani katika majina yetu. Tunatakiwa majina yetu yatakaswe kwa damu ya YESU KRISTO.
Sio lazima ubadili jina lako kama jina hilo halima maana mbaya lakini jina hilo hilo lenye maana nzuri inawezekana ulipewa na wazazi wako au ndugu zako likiambatanishwa na maneno ya kipepo waliyoyanena.
Mithali 18:21 ''Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.''


Kumbe mabaya au mazuri yako katika uwezo wa ulimi. Kama ulitamkiwa mabaya hakika unaweza kuyaishi mabaya hayo kama hutamwitaji BWANA YESU ili alitakase jina lako.
Unaweza kuwa mtu wa kuonewa tu kwa sababu jina lako limebebeshwa kuonewa.
Jina lako linaweza likaambatanishwa na majanga na ukaja kuwa mtu wa majanga tu.
1 Samweli 25:25 '' Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.''

Huyu mtu wazazi wake walimpa jina Nabali yaani mpumbavu na katika maisha yake alikuja kuuishi upumbavu maana jina lake lina maana ya upumbavu na limebeba upumbavu.
Unaweza kuwa mtu wa majanga tu kwa sababu jina lako limebebeshwa majanga.
Unashangaa kila mara ajali ni wewe tu.
Kila uharibifu na wewe unakuhusu.
Unakuta watu wote wanakuchukia wewe tu na haujui chanzo cha kuchukiwa huko.
Kumbuka jina lako ndio wewe mwenyewe, jina likibebeshwa mabaya hakika mabaya hayo umebebeshwa wewe na yatakupata wewe.
Unashangaa njaa ni kwako tu kila siku kwa sababu jina lako limebebeshwa umaskini.
Jina lako linaweza likaambatanishwa na roho ya kukataliwa.
Inawezekana kabisa mimba yako ilimhangaisha sana mama yako hadi akakuita shida au Tabu au Masikitiko akidhani kwamba atakuwa anakumbuka shinda zilizompata wakati wa Mimba kumbe amekubebeshwa wewe hiyo shida. Leo Mwite BWANA YESU ili alitakase jina lako na alitenge jina lako kutoka kila maagano ya kipepo yaliyoambatanishwa na jina lako.

Maagano ya shetani lazima yafutwe kwa damu ya YESU KRISTO kwako ndipo utakuwa huru na ndipo utashinda.
Hosea 10:4 ''Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.''

Sio lazima kujua wazazi wako au ndugu zako au walezi wako walikupa jina lako kwa sababu ya nini na walitamka nini, wewe futa maagano yote ya kishetani yaliyoambatanishwa na jina lako.
Kuna watu hata afanye mazuri kiasi gani bado ataonekana tu mbaya kwa sababu majina yao yameambatanishwa na roho ya kukataliwa.
Unakuta kila mchumba anakukataa.
Unakuta kila biashara inakukataa wewe tu.
Kila Fursa nzuri za uchumi haziji kwako tu.
Omba maombi ya kulitaka jina lako na kulitenga na kila maagano ya kishetani.
Jina lako linaweza likaambatanishwa na roho za magonjwa.
Kuna watu wanateswa na magonjwa kila siku. Kuna watu wanaumwa lakini vipimo hospitalini vinaonyesha ni wazima wakati wanauma tena wanaumwa sana.
Kuna maroho ya kishetani yanaweza yakaambatanishwa na jina lako ndio maana unamhitaji sana BWANA YESU ili upone.
Kwa sababu jina lako ndio wewe basi yaliyotamkiwa jina lako yanaweza yakakufuatilia.
Damu ya YESU KRISTO pekee ndio inaweza kuyafuta maagano yote ya kishetani yaliyoambatanishwa na jina lako.
Inawezekana jina lako ulipewa na bibi yako kwa lengo ambalo si wewe wala wazazi wako wanajua ila ni bibi mtoa jina tu ndio anajua.
Jina lako ni muhimu sana, likichafuliwa jina lako ni wewe umechafuliwa.
Jina lako lilibebeshwa matatizo ni wewe umebebeshwa matatizo hayo.
Leo futa maagano mabaya yote yaliyoambatanishwa na jina lako, futa kwa jina la YES KRISTO.

Maombi haya chini ni maombi ya mfano ya kumsaidia muombaji mchanga ili ajue kuomba na aombe akiliendea hitaji lake mwenyewe. Kwa yule ambaye ni muombaji mzoefu basi baada tu ya kulisoma somo lote na kulielewa basi utaomba vizuri bila kutumia maombi ya maelekezo hapa chini.
Jambo muhimu sana katika maombi yeyote ni utakatifu hivyo tubu uovu wako na usiufanye tena kisha omba maombi haya.



MAOMBI YA KUFUTA KILA MAAGANO YA KISHETANI YALIYOAMBATANISHWA NA JINA LAKO, KISHA FANYA AGANO NA DAMU YA YESU KRISTO.

BABA katika jina la YES KRISTO aliye hai. Ninakushukuru MUNGU wangu kwa uzima ulionipa na ninakushukuru sana kwa nafasi hii uliyonipa ili niombe mbele zako maombi ambayo utayajibu Mfalme wangu.
Nalitakasa jina langu kwa damu ya YESU KRISTO. Naomba BWANA YESU uliondoe jina langu katika kila agano baya ambalo walionipa jina ndio wanalijua.
Katika jina la YESU KRISTO ninafuta maagano yote ya kishetani yaliyoambatanishwa na jina langu, ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila maroho ya kishetani yaliyoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za magonjwa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za mauti zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kukataliwa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za uonevu zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kudharauliwa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kufeli zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za uongo zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za wizi zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kuibiwa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za dhambi zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za anasa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za uchafu zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za uzinzi na uasherati zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za hasira mbaya zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kuogopwa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kutengwa na ndugu zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
roho za kuonewa zilizoambatanishwa na jina langu ninafuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
kila roho ya shetani iliyoambatanishwa na jina langu naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Asante MUNGU BABA maana kupitia jina la YESU KRISTO nimeshinda.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kuamini hivyo nimepokea ushindi mkuu.
Amen Amen.


Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments