NDOA ZA KICHAWI

Na ASKOFU MKUU Dr JOSEPHAT GWAJIMA


Maana halisi ya ndoa kwenye Biblia.
Ndoa ndio mahala pekee duniani ukijumlisha moja na moja unapata jibu n moja,kwa maana hiyo kama mwanandoa mmoja ni mbovu na mwingine ni mzuri wakiwa kwa pamoja wote wataharibika vilevile kama moja akiwa mzuri na mwingine mzuri wote wataongezeka kuwa wazuri.
Kwenye maisha ukimwona mtu ni mgonjwa ana matatizo lazima kuna chanzo cha tatizo lake, na ukiamua kushughulikia tatizo hilo bila kushughulika na chanzo chake, lazima tatizo litakirudi zaidi lilivyokuwa mwanzo.
Mwanzo 10:8-9 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.”
Ndoa ya kichawi ni kitendo cha mwanadamu na mchawi au jinni/pepo kuwa kitu kimoja kwenye ulimwengu waroho lakini, unaweza ukawa unahangaika sana na jambo fulani kwenye ndoa na usielewe tatizo ni nini kumbe hapo ndipo chanzo cha mikosi, balaa, magonjwa, umaskini vinatokea.
Waefeso 5:31 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”
Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Waefeso 6:16-18 “zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
Kila mtu ananyota yake na unaweza ukawa na nyota nzuri na kibali mbele za watu lakini ukajikuta umeungamanishwa na mtu ambaye anaroho ya kichawi nadani yake kwenye uhusiano na baraka zako, nyota zako vikatoka kwako vikaenda kwake kwasababu mmekuwa kitu kimoja.
Unaweza kumwona mtu anaonekana mzuri kumbe amekuja kwako kujichanganya na wewe ili akuletee kitu kingine ambacho ni kichafu kikuingie bila wewe kujua.
Ezra 9:1-3 “Na mambo hayo yalipokwisha kutendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, wamefanya sawasawa na machukizo yao, yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori.Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili.Nami niliposikia hayo, nikararua nguo yangu na joho yangu, nikang'oa nywele za kichwa changu, na ndevu zangu, nikaketi kwa mshangao.”
Mtu mmoja anapozaa mtoto na mtu mwingine mtoto huyo atakapozaliwa kama baba au mama alikuwa vizuri rohoni anamsikiliza Mungu na kumpenda, mtoto anaweza akarithi kutoka kwa mzazi mmoja wapo na akaendelea vizuri.
Ezra 9:12 “Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele.”
Nehemia aliwakuta watu wa Mungu ambao wameoa/olewa na watu ambao hawakuwa kitu kimoja na wao rohoni kwa maana hii tunajifunza alikuwa anamaanisha ndoa sio kitu cha kuchezea. Ukitaka kuolewa au kuoa lazima umpate anayefanana na wewe kiroho.
Nehemia 13:25 “Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.”
Maana nyingine ya ndoa za kichawi ni pale mwanamke au mwanaume mchawi ambaye anangangana awe na mahusihano na wewe akijua moja jumlisha na moja ni moja lengo lake akitaka vile vitu vyako vitoke kwako viende kwake na vile vyakwake vije kwako na hapo ndipo magonjwa, kufa kabla ya wakati, balaa, nuksi, ulemavu, upofu vinakupata. mnanapokuwa na mahusihano maana yake mnakuwa si wawili tena bali mmoja hivyo mnapeana kama ni mikosi, nuksi zinahama kwa mmoja zinaenda kwa mwingine na nyota nzuri inahama kwa mmoja inakwenda kwa mwingine. Hapo unashangaa baada ya miezi miwili kama upo kwenye ndoa talaka inaanza kukujia, magonjwa yanaanza, kukataliwa kunaanza, kupata na kupoteza kunaanza kukupata.
Kwenye maisha tunayoishi wachawi ni wengi kuliko wasio wachawi, maana yake kila unayemwona ambaye hakusanyi pamoja na sisi basi huyo ni mchawi kabisa.
Kuna aina za wachawi.
Kuna wachawi ambao wanajua amezaliwa kutokea kwenye familia ya kichawi, kuna wengine wa kununua, mfano mtu anataka watu watetemeke wanapomsikia na kumwona hivyo anaamua kuwa mchawi, kuna wachawi wa kutokujua ambao wapo wengi sana, hawa ni wale wanaokaa kwenye familia na wanakuwa kwenye familia zao wamechanjwa chale za kichawi tangu wakiwa wadogo ili kuandaliwa kuwa wachawi baadaye bila wao kujua. Hawa ni wale wanaokuwa na kujikuta wakipenda mambo ya kichawi na kishirikina wao wenyewe.
Unaweza ukawa unaishi na mtu kwenye uhusihano ambaye ni mchawi na yeye ndiye aliyekufanya upatwe na mabaya hayo. Maana yake tangu umekutana naye mambo yako yamerudi nyuma huku ukijiuliza kwanini kumbe ni yeye amekuletea na kusababisha hayo kwa kujua au kutokujua.
Maandiko yanasema waziwazi kuna uwezekano kwamba mtu mmoja kwenye ndoa anaamini tayari huku mwingine haamini lakini kama yupo unayeamini anaweza akasimama akawasha moto mpaka yule mtu asiyeamini akaondoka na balaa zake, na mikosi yake, na laana zake zote bila kugombana huku afya yake na uhai na nyota yake huyu anayeamini iliyokuwa inanyonywa ikarudi na kuwa kama zamani.
Kutoka 22:18 "Usimwache mwanamke mchawi kuishi."
Unaweza ukawa tangu umeanza maombi mahusihano yako yameanza kuyumba, umeanza kuona watu wako wa karibu wanakutenga fahamu si maombi yaliyowakutenga nao bali umeharibu zile kazi zao na kung’oa nguvu zao zilizowafanya wajiunge na wewe ili wakuharibu na kutumia nyota yako na vipawa vyako. Aliyeumbwa na Kristo ni roho moja naye na aliyeumbwa na mchawi ni mwili mmoja naye.
kuna watu wanavutiwa kukaa na watu waliokaa vibaya wasiokuwa na maana kwasababu wametekwa na kuibiwa. Duniani imezoeleka mtu akikaa karibu na mtu wa Mungu anajiskia vibaya lakiini akiambiwa anapendwa na mtu wa duniani ambaye hana roho ya Mungu ndani yake,kuna watu wakiambiwa na mtu wa Mungu wanapendwa hawajisikii kama wanapendwa hawaelewi wala haoni uzito wake lakini anajiskia vizuri lakini akiambiwa anapendwa na mtu wa kidunia wanajiskia vizuri sana mpaka inashangaza, maana yake wametekwa na kuibiwa nafsi zao zinafanya yale mapenzi ya ufalme uliowateka na kuwaweka kifungoni.
Shetani aliyevaa mwili.
Kuna malaika wa aina mbili, malaika watakatifu na malaika wachafu, Malaika watakatifu ni watakatifu na malaika wachafu ni wachafu kabisa.
Mwanzo 19:5 “Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.”
Hapa tunajifunza tena Mungu alitaka tujifunze kwamba malaika wanaweza kujigeuza wakavaa miili wakawa kama watu na watu wakavutiwa nao wakawa na mahusihano nao, malaika wachafu ambao ni mapepo na majini wanaweza wakavaa maumbo akaja kwako kama kijana mzuri anataka kukuoa au kuolewa na wewe na kama wewe hujui lolote kuhusu ulimwengu wa rohoni unajikuta unaingia kwenye mahusihano naye na maisha yako yanaanza kuharibika sababu Yule hakukupenda bali alikuja kuchukua ulivyo navyo mbavyo ni nyota, kibali, upendeleo uliopewa tokea mbinguni, huku ukibakiwa na magonjwa, taabu, mikosi nay eye akiujenga ufalme wa giza kutumia nyota na vipawa vyako.
Ufalme wa shetani umejengwa kwa kutumia vitu vya watu na shetani sio muumbaji na hatakaa kuja kuwa muumbaji. Unaweza ukawa unamwona Kaka, dada, mama au baba unakuta anauhusihano na mambo ya kichawi lakini mchana ni daktari, au mwanasheria anavaa suti vizuri kabisa huwezi kumdhania ni mwanga hata kidogo kumbe ni mrukaji anaharibu maisha ya wenzake na hataki kuacha, hawa ndio wa kuwashughulikia mpaka waishe kwa jina la Yesu krito.

Unatakiwa ujue kuangalia watu kwa makini sana kabla hujaanza mahusiano nao, hasa ukikutana na mtu mwenye Mungu fahamu kuwa anavyo vyote hata kama anaonekana amepinda kidogo ni kwa muda huu tub ado ni yai muda wake ukifika hutaamini kama ndiye yeye aliyekuwa amepinda na kuchoka.
Kama mtu hana Mungu hata kama yupo vizuri ana mali nyingi huyo hafai maana baada ya muda lazima ataanguka. Usitafute vile ambavyo vimetafutwa ukasema mkale pamoja maana kila aliyesimama yupo aliyemsimamisha akafika akasimama, usifanye mchezo kuanza mahusihano na mtu asiye wa Mungu utaumia na kuhangaika bali mtafute mtu muanze pamoja mkiwa na Mungu mwende pamoja lazima mtafika pamoja. Hata kama mtu hajui kufunga tai lakini ana Mungu ndani yake huyo anafaa utamfundisha mbele ya safari cha muhimu awe na Mungu basi maana ukiwa na Mungu unavyo vyote.
Kila mtu aliyepanda juu kuna waliompandisha akafika pale, hakuna kuinuka bila kuwa na muinuaji, ndiomaana Yesu alisema “nitakapoinuliwa nitawavuta na wengine twende juu” kila alichokipanda mtu atavuna hichohicho.
Mtu anaweza akawa ananyota ya uso na wachawi wanapomwona wanaangalia anapenda nini ili wamfuate wachukue uso wake. Kuna watu wameolewa rohoni na majini mahaba na mwilini pia wanaishi na watu wasio watu na hao ndio wanaoleta balaa na mikosi kwake.
Kuna watu wana nyota ya mdomo kila wakiongea wanapata uraisi, kuna watu nyota yao iko mdomoni ukimsikiliza lazima utamkubali kwasababu ya nyota ya mdomoni. ‘Usidharau mtu wa Mungu’.
Magonjwa yanaweza yakawa yanakupata ukaugua kwasababu ya kuwa na ndoa ya kichawi. Kuna mambo ambayo fedha haiwezi kuyaondoa, wala raisi, wala serikali haiwezi kuyaondoa lakini mtu wa Mungu ndiye anayeweza kuyaondoa pekee. Kuna mtu ananyota ya miguu akifuatilia jambo lazima alipate, kuna mwingine ananyota ya macho akiangalia lazima mtu ampishe, kuna mwingine ananyota ya mikono akifanya jambo linafanikiwa, kuna mtu tumbo lake limebarikiwa akizaa basi atazaliwa mchungaji, Raisi, Jaji mkuu, Waziri lakini watu wenye nyota ya tumbo kuolewa kwao huwa ni vigumu na kama wameolewa basi kuzaa huwa ni vigumu na kama akizaa atazaa kwa taabu sana sababu kuna waliofunga naye ndoya ya kimwili au kiroho wanazuia nyota yake ili waichukue waitumie kwenye ufalme wa giza.

Watu wenye ndoa za kichawi ni wale waliokutana na mtu ambaye wakampokea kama mpenzi au rafiki na walipoachana naye wakaanza kupatwa na mabaya na taabu kumbe yeye ndiye aliyeondoka na nyota zao.
Hutakaa umwone Mungu kwenye maisha yako lakini Mungu ameweka maneno ndani ya vinywa vya watu wake kwaajili yako, ukiyasikia ukayatendea kazi lazima utafanikiwa.
UKIRI. “Leo ninarudisha asili yangu kwa jina la Yesu, nyota ya kuongea, nyota ya mikono, nyota ya miguu, nyota ya tumbo nairudisha leo kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu kila mtu niliyekutana naye kimahusihano akaniachia mabaya, balaa na mikosi namrudishai yeye kwa jina la Yesu, Kwa jina la Yesu ninaamuru moto wa Mungu upenye ndani yangu kwa jina la Yesu.”
Sio darasa linaloamua uwe nani ni nyota inayoamua uwe nani maana sio wale wanaokuambia utakua nani ndipo utafanikiwa bali ukirudisha nyota yako utakuwa vile unavyotakiwaa uwe kama ulivyotoka mbinguni.

Matendo ya Mitume 16:16-18 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.”
Pia ndoa ya kichawi ya rohoni ambayo hii hutokea pale mtu anapoota anafanya mapenzi ndotoni, hiyo ni namna nyingine ambayo unakuta mtu ameolewa rohoni usiku aliyemuoa anamfuata na kufanya mapenzi naye ndotoni na huyo ndiye anayekuja kumwekea magonjwa, balaa, kukataliwa ndiye anayekuja kuchukua nyota na vipawa vyake huko akimwachia magonjwa na vifungo. Mahusihano hayo ya usiku huishia kuleta kuharibia biashara, au ndoa, au kazi au familia na magonjwa na vifungo huanza kumfuata mtu huyo.
Namna nyingine ya ndoa za kichawi ni jini au joka anakuja kujiungamanisha na wewe na huyo anavaa mwili anakuja kama mtu, kumbuka shetani akija anakuja ili aibe, aharibu na kuchinja. Akija kwako anakuwa ametumwa au anajua wewe unayo nyota anayoihitaji na ndiyo anayokuja kuichukua kwa kujiungamanisha na wewe ili kutimiza sheria ya kuwa kitu kimoja na baada ya kufanikiwa basi anachukua vyote na kukuacha mtupu.
Waefeso 5:23 “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.”

Kama umeolewa na jini basi lile jini ndilo linalokuamulia kila kitu,ndiomaana akitaka ulale unalala, akitaka uharibikiwe unaharibikiwa, akisema ufilisike unafilisika. Hii inamaana kama una ndoa ya kichawi kwamaana kwamba umeolewa au huwa unaota ndoto za kuingiliwa utakuwa na mambo yatakayokupata kama matano. 1. Kama unabiashara itafilisika, 2.Ni ngumu sana kuolewa/kuoa kwasababu utakuwa kuwachukia wanaume/wanawake sababu ya wivu wa aliyejiungamanisha na wewe kichawi, 3. Ikitokea umeoa/olewa na mtu kupata mtoto ni kazi sana kwasababu ya Yule mke/mume wa rohoni anazuia usipate mtoto, 4. Kukataliwa iwe kazini au kwenye jamii ya watu. 5. Magonjwa, haya yanasababisha mwili wako unashindwa kuwa imara unakuwa kila wakati mgonjwa mara uso unacheza wenyewe, mpaka kwenye ndoa inashindikana kutimiza baadhi ya majukumu. Yote haya na mengine chanzo chake ndoa ya kichawi.
Kuna watu wengine wameunganishwa na ndoa za kichawi kwa pete walizozivaa, kwa zawadi walizopokea bila kuzitakasa kwa damu ya Yesu, kuna wale ambao wanamaagano ya kichawi kwenye ukoo au familia hivyo wamejiungamanisha wakawa na uhusihano na mizimu na majini ya koo.
1 Samweli 30:8 “Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.”
UKIRI- “ kwa jina la Yesu ninavunja maagano ya kichawi, mikufu ya kichawi, nguo za kichawi, zawadi za kichawi ambazo nimepewa na mtu naziharibu kwa jina la Yesu, kama kuna nguo au chochote kile nilichopewa kama zawadi na mchawi ninakiharibu kwa jina la Yesu. Kwa jina la Yesu jini au pepo au mchawi niliyefunga naye ndoa ninamteketeza kwa jina la Yesu.”
Ninaamuru nyota ya akili, nyota ya uso, nyota ya miguu, nyota ya kusafiri, nyota ya miguu iliyoibiwa naifuata nakuirudisha kwa jina la Yesu, kwa damu ya Yesu kuanzia sasa ninatamka mahala popote palipo na nyota yangu ya biashara, nyota ya kazi, nyota ya kinywa, nyota ya uso naamuru njoo kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa mtu yeyote aliyenifanya niingie kwenye ndoa ya kichawi namponda namwangamiza kwa jina la Yesu, naamuru nyota yangu irudi kwa jina la Yesu kristo (Simamia kwenye tatizo ulilo nalo kama unaona umeibiwa nyota yako irudishe kwa jina la Yesu, [Mungu anatenda sawasawa na unavyoamini na kusema kwa jina la Yesu] Amen.)

Comments