PICHA ZA MAZISHI YA MKE WA MWIMBAJI JACKSON BENTY YALIYOFANYIKA ARUSHA


Jackson Benty akiaga mwili wa marehemu mkewe, Winnie Benty.
Zifuatazo ni baadhi ya picha kati ya nyingi ambazo Gospel Kitaa imefanikiwa kukusanya ili wewe msomaji wetu ambaye hukupata nafasi ya kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Jackson Benty, marehemu Winnie Benty yaliyofanyika tarehe 12 Oktoba katika makaburi ya Njiro huko jijini Arusha. 

Awali kabla ya mazishi hayo mamia ya wakazi wa jijini Arusha na sehemu nyinginezo nchini wakiwemo waimbaji wa muziki wa injili walikusanyika nyumbani kwa mume wa marehemu ambako ibada ya mazishi iliongozwa na mchungaji Bryson wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kutoka Dar es Salaam, ambako Benty anaabudu (Ufufuo na Uzima Arusha), kisha kuwapatia watu nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho na kuelekea makaburini ambako waliupumzisha mwili wa marehemu.

Marehemu Winnie amezaliwa tarehe 7 Septemba 1985 na kufariki tarehe 8 Oktoba 2016, kutokana na ajali iliyohusisha pikipiki aliyokuwa amepanda, na basi la abiria mali ya kampuni ya Mtei Express maeneo ya Burka, Arusha. Marehemu ameacha mgane (Jackson Benty) na watoto wawili wa kiume.

Sehemu ya waombolezaji.


MC Joshua Makondeko

Maombi yakiongozwa na watumishi kutoka Kanisa la Ufufuo an Uzima Tanzania.


Mama wa marehemu.

Mwili ukiagwa

Umati ukitoa heshima zao za mwisho.

Baba akibembeleza mtoto wao wa pili.

Mchungaji Bryson kutoka Ufufuo na Uzima Dar es Salaam akiongoza maombi kwenye ibada ya mazishi

Upendo Mbila kutoka CHAMUITA Arusha akimfariji Jackson Benty


Msafara kuelekea makaburini ukaanza.


Waimbaji Matilda Jojo na Tuponile Komba

Waimbaji wanachama wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania - Arusha kwa umoja wakafika baada ya kutoka studio usiku wake walipokuwa wakirekodi wimbo kwa ajili ya marehemu.


Mavumbini tutarudi


Mume wa marehemu akiweka shada la maua.
Mchungaji Frank Andrew wa Ufufuo na Uzima Arusha akiweka shada la maua kwa marehemu amnbaye alikuwa mshirika wake.

Mtoto wa kwanza wa marehemu akiweka shada la maua.

Wazazi wa marehemu

Wana Ufufuo na Uzima

Kundi la waimbaji wenza.
Safari yetu huishia hapa.
Gospel Kitaa inawaombea wafiwa kwa Mungu wapate faraja ya pekee ipitayo zote. BWANA ametoa na BWANA ametwaa. Jina la BWANA lihimidiwe.

 Source:Gospel Kitaa

Comments