SHUHUDA KUTOKA EFATHA MWENGE.




efatha shuhuda

Namshukuru MUNGU pikipiki iliyoibiwa imepatikana na mwanangu ameokoka


Naitwa Dorah Juliasi, namshukuru MUNGU kwa MATENDO yake ya AJABU, Mwanangu alinunua pikipiki, ilikuwa ni siku ya Jumatano na Alhamisi akamkabidhi ndugu yake (mdogo wake) aifanyie kazi (biashara) kwa ajili ya kuendesha bodaboda. Ilipofika siku ya Jumamosi ikaibiwa, mwanangu akanipigia simu akaniambia kuwa imeibiwa nikamwambia usijali mimi kesho (Jumapili) naenda Kanisani, akasema twende kwa mganga mimi nikamkatalia, nikamwambia Mimi nina Imani na MUNGU, Mimi nitamtazama MUNGU, ila yeye akaenda na akaambiwa apeleke jina la mtu anayemuhisi kuwa kachukua, akarudi nyumbani ili apange siku ya kupeleka hilo jina. Mume wa mwanangu aliyenunua hiyo pikipiki, naye akaenda kwa mganga akaambiwa apeleke hela nyingi tu na yeye akarudi nyumbani ili ajipange kupeleka hizo pesa. Mimi nilipofika Kanisani nikawashirikisha Viongozi wangu wa Eneo la Yerusalemu tukaomba, na ilipofika Jumatatu nikafunga huku namlilia MUNGU na siku ya Jumanne pikipiki IKAONEKANA. Huku kati ya mwanangu na mume wa mwanangu wakiwa Hawajafanikiwa kurudi kwa mganga, namshukuru MUNGU sana kwa mengi aliyonitendea, baada ya hayo huyu Mwanangu wa Kiume ambaye Pikipiki aliibiwa, akaniambia “Mama nataka kuja huko Kanisani EFATHA”, kweli Jumapili iliyopita alikuja Kanisani hapa na AKAOKOKA na leo nimekuja naye ili Tumshukuru MUNGU pamoja. Mganga wetu ni YESU KRISTO, Husipate tatizo ukakimbilia kwa mganga mwingine bali njoo kwa YESU maana YEYE ndiye Kila kitu Kwako na Kwake tunapata USHINDI.

shuhuda

Nimefaulu First class ya Chuo Kikuu


Naitwa Anthony John Bosko, namshukuru Mungu kwa mengi aliyonifanyia katika elimu yangu. Wakati ninaanza shule (yaani darasa la kwanza) kulikuwa na changamoto kwa maana kuanzia darasa la kwanza nilikuwa ninaandikiwa nimeshindwa katika mitihani yangu lakini ninamshukuru Mungu nikafaulu (second selection). Nilipofika kidato cha pili (form 2) nikaokoka (Efatha) na hali ya masomo yangu ikabadilika sana nikaanza kupata 80 hadi 100 wanafunzi wenzangu tuliokuwa nao toka shule ya msingi walidhani kuwa ninabahatisha ila kumbe ilikuwa ndio Mungu ameanza kunibadilisha.
Nikafanikiwa kuingia kidato cha tano na cha sita na baada ya hapo nikaingia chuo Kikuu cha Mzumbe, nilipoingia chuo nikamwambia Bwana Yesu nataka nitoke na first Class nikawa ninaandaa sadaka maalum kwa ajili ya mitihani yangu na kila mtihani niliokuwa nafanya nilikuwa napata A tu. Namshukuru Mungu nikaweza kutoka na kile nilichokuwa nakihitaji (first class), sio kwa nguvu wala uweza wangu bali ni kwa YEYE anayeweza yote MUNGU mwenye NGUVU. Wokovu unamaana sana na wokovu ni Kipawa cha kukufanya uende mahali pa UTUKUFU mimi nimeshuhudia.

shuhuda

Mwanangu amefunguliwa kutoka katika vifungo vya kichawi


Naitwa Mboni Mwaminifu namshukuru Mungu kwa Kumkomboa na Kumponya mwanangu kutoka katika nguvu za kichawi. Shetani alimtumia kuharibu vitu vingi na kufanya mambo mengi ya kipepo, tulihangaika makanisa mengi bila kupata msaada, lakini siku moja tukaamua kumleta hapa Efatha ambapo aliombewa na siku ya tarehe 14/8/2016 tulienda Precious Center Kibaha ambapo kulikuwa na Ibada, Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alitamka kuwa kila uchawi na ulozi mwisho leo, na tukashiriki meza ya Bwana baada ya Ibada ile alitapika sana na sasa amekuwa mzima kwa kuwa amefunguliwa kutoka katika nguvu hizo ambazo alipewa na Bibi yake. Hakika Mungu ni mkuu na anatenda mambo ya ajabu Sifa na Utukufu namrudishia yeye aliye mwenye uweza wote.



Comments