SIYO YOTE NI MAKANISA,MENGINE NI MAKABURI

Na Mtumishi Generali Geoffrey Mwanza
Ni ujumbe kwa njia ya shairi lililotungwa na Mtumishi Geofrey Mwanza Kutoka Mombasa Kenya.
Karibu kujifunza.

Wakati umewadia; nikupe tena wosia;
Ni lini utasikia;nikishakwambia;
Maonyo umesikia;na bado wanililia;
Siyo yote ni Makanisa;mengine ni makaburi.



Dhambi yashabikiwa;na bado Bwana asifiwe,
Ni wapi karuhusiwa;dhambi ishabikiwe,
Miujiza mwauziwa;haja yenu mbarikiwe,
Siyo yote ni Makanisa;mengine ni makaburi.



Usipoiacha dhambi;jehanamu yakungojea,
Sio moto wa tambi;siku zinasongea,
Usiifiche dhambi; maana inaongea,
Siyo yote ni Makanisa;mengine ni makaburi.



Nilichokutabiri; sasa kinatendeka,
Ili upate kukiri;na kweli utaanguka,
Rudia MUNGU si siri;na utakubalika,
Siyo yote ni Makanisa; mengine ni makaburi.



Achana navyo vitisho; kitambo nilikuonya,
Shetani anao mwisho;na sasa mekutawanya,
Itakuwa thibitisho; tena hamna mwanya,
Siyo yote ni Makanisa;mengine ni makaburi.



Generali nimemaliza; mie mwana wa Mwanza,
Yesu anakuwaza;moyo wako aupate kwanza,
Safari imeanza;tafuta ufalme kwanza,
Siyo yote ni Makanisa; mengine ni makaburi.



Imetungwa nami Generali Geoffrey Mwanza nikila lunch mahali tu nikahisi ujumbe umenijia (13:37pm)
Ubarikiwe sana ndugu mpendwa na kama hujaokoka; okoka sasa hivi.

Comments