SOMO LA UFAHAMU KWA VIJANA



Na Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira


img1Haleluya Vijana, hususani wasichana, ule wakati wa kulialia MUNGU nipe mume umeisha, unaacha kufanya mambo ya msingi kwa ajili ya ustawi wako. 


Ni vizuri ujiulize upo tayari kuchukua majukumu? Mungu akikujalia leo mtoto una uwezo gani kumhudumia? upo tayari kutawaliwa?, wasichana wengi pengine kwa sababu ya elimu waliyopata hawataki kutawaliwa na wanaume. Kama Neno linavyosema Mwanzo 3:16 “Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”.


img1Kuna harakati mbalimbali duniani leo hii ambazo zinaelekeza kukiuka kile Mungu amesema, hasa katika USAWA, Mungu akiona nafsini mwako hutaki kutawaliwa hakupi mume kwa sababu hustaili.

Siku ulipo kuwa na rafiki wa kiume (boyfriend) mbingu ilihesabu huyo ni mume wako, kwa hiyo utakuta mtu ana rafiki wa kiume na anamuomba Mungu ampe mume, haiwezekani. Ukiokoka hakuna boyfriend wala girlfriend, achana naye baki na Yesu yeye akiona upo naye atakupa mume wa kufanana na wewe.




 Wewe binti tumia muda mwingi kujishughlisha, usiolewe ili katunzwe, au kwa sababu kwenu wamekuchoka, bali olewa ili kukamilisha ratiba za Mungu. Jishughlishe ili upate kipato na akiba Mungu aone hata akikupa Mume huendi kuwa mzigo/msalaba bali unakuwa baraka.

Sio vibaya kumuomba Mungu akupe mume ila ni vema ukajua kuolewa ni majukumu, ni kutawaliwa na ukubaliane na hilo, vinginevyo haitajulikana nani ni kichwa ndani ya nyumba. 




Tabia njema huvuta tabia njema, rekebisha tabia yako ili Mungu akupe wa kufanana nawe.

Ni maombi yangu MUNGU akupe mume wa kufanana naye wewe unayetarajia, na ukawe msaada na zawadi kwake. Katika mwaka huu wa mng’ao, Nuru yake ikakuangazie, KWA JINA LA YESU POKEA
Naamini kuna kitu umejifunza kwa somo hili fupi. PIA SIKILIZA SOMO HILI HAPA CHINI.




Comments