UNAONGOZWA NA NINI KATIKA KUPATA MCHUMBA?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la Uzima.
Je unaongozwa na nini kupata Mchumba?
=Kuna watu huongozwa na tamaa zao lakini tamaa za mwili zinaweza kuamua vibaya na ukajuta baadae.
1 Yohana 2:16-17 '' Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA(MUNGU), bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele.''

=Kuna watu huongozwa na misukumo ya kipepo ndio maana ni muhimu sana kuzichunguza kila roho kama zinatokana na MUNGU maana waongo ni wengi sana.
1 Yohana 4:1A '' Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU;''

=Kuna watu huongozwa na ROHO MTAKATIFU na hao hufanikiwa sana na kama wakidumu katika maongozo yake kuiona ndoa ni paradiso ndogo, ila ROHO MTAKATIFU yuko kwa waliookolewa tu na BWANA YESU.
Kuongozwa na ROHO MTAKATUFU ni kushinda hakika, Yeye anasema;
''Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.-Zaburi 32:8-9''
Je wewe unaongozwa na nini katika kumpata mchumba?
Kuna wengine kwa sababu hawajataka kumfuata BWANA YESU ili awaokoe ndio maana adui amewafunga kiasi kwamba wao kuoa au kuolewa ni tatizo kubwa bali wameishia tu kila mara kuota wanafanya mapenzi.
 Kuota Unafanya Mapenzi, Hilo Ni Jini Mahaba. Kama Umezoea Kuota Unafanya Mapenzi Angalia Vita Na Ugumu Utakaokupata Wakati Wa Harakati Za kupata mchumba au Kufunga Ndoa, Maana Kupitia Ndoto Ulikuwa Unamilikiwa Na Mwanaume Wa Kipepo Au Mwanamke Wa Kipepo Ambaye Hatakubali Kirahisi Uoe Au Uolewe Na Mwanadamu Mwenzako. Pambana Ndugu Ukimwangamiza shetani Huyo Kwa Jina La YESU KRISTO Mfalme Wa Uzima.

Ni kweli unataka mchumba lakini je kwa wakati huu MUNGU Akiangalia Dhamiri Yako Inawaza Nini Leo, Je Ataona ni Jambo Jema Unalowaza Leo?
Kuna wengine husema wanatafuta wachumba lakini ukweli ni kwamba wanatafuta wa kuzini nao, ni mbaya sana.
Ninachojua Ni Kwamba Binti Anayekubali Kuchezewa Na Anadumu Katika Unajisi Huo Hana Akili Hata Moja.
Kijana anayezini hana akili hata moja. Biblia inasema;
'' Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.-Mithali 6:32-33  ''

 Ukiwa Mwaminifu Kwa MUNGU Ni Lazima Tu Utapata Upendeleo Kwa MUNGU Na Kwa Wanadamu.
Ukiwa mwaminifu kwa MUNGU hakika utapata kitu chema, utapata mchumba sahihi na utapata wa kufanana na wewe rohoni.
Changamoto nyingi leo ni watu wa MUNGU kukubali kukaribisha shetani kwenye maeneo yao wakati wa uchumba.
 Uchumba Wa Chumbani Chumbani Sio Uchumba Bali Uchumba Sahihi Ni Ule Uchumba Unaotambulikana Kwa Kanisa Na Wazazi Huku Uchumba Huo Ukiambatana Na Utakatifu Mwanzo Hadi Mwisho. Uchumba Wa Chumbani Chumbani Sio Uchumba Bali Uhawara Tu.
1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ''

Uzuri Wa Mwanamke Sio Urembo Bali Ni Tabia, Tena Uzuri Wa Mwanamume Sio Pesa Bali Ni Utakatifu. Iweni Makini Ndugu Zangu. Ni Heri Ukampata Mchumba Wako Madhabahuni Na Sio Kumpata Kwenye Vilabu Vya Pombe.
Ijapokuwa Ni Rahisi Sana Kupata Mchumba Lakini Pia Naomba Ujue Pia Kwamba Ni Rahisi Tena Ni Rahisi Sana Kuachwa Na Mchumba Huyo Kama Atagundua Kwamba Wewe Una Tabia Mbaya, Na Kwa Tabia Hizo Mbaya Hauna Sifa Za Kuishi Na Yeye Katika Ndoa. Kuvunja Uchumba Sio Dhambi Ila Ndoa Haivunjwi Hadi Kifo Kinawetanginesha. Hivyo Wachumba Kuweni Makini Na Mcheni BWANA YESU Mtashinda.
 Je unaongozwa na nini kupata Mchumba?

Katika kupata mchumba sahihi ni muhimu kumtafuta kwanza huyo mchumba kupitia maombi na sio kupitia macho yako.
Maombi unayoomba leo yanaweza kuwa jambo la kumkumbusha MUNGU katika hitaji lako la kesho.
1 Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''
Ni muhimu sana kuwa muombaji na sio kutegemea tu kuombewa.
Marko 11:24 ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo
yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu''

Nakusihi ndugu kuhakikisha unakuwa mwana
maombi na husika na maombi kila siku, Ombea uchumba, ombea mchumba wako, ombea ndoa yako na ombea maisha yako.

Kutamani kuolewa au kuoa huku hata kuomba hujui ni hasara kwako 
 Je unaongozwa na nini kupata Mchumba?

Kuna Mabinti Leo Wanasema Wanataka Watoto Wakati Hata Kuolewa Bado. Ukiruhusu Mawazo Hayo Ndani Yako Binti/mwanamke Shetani Atakuletea Mtu Wa Kuzaa Naye Na Sio Kuolewa Naye, chunga  kinywa chako na Mche MUNGU.
Bidii Yako Kwa BWANA YESU Inaweza Kutengenza Mambo Matatu;
 =Itatengeneza Baraka Za Kiroho Na Kimwili.
=Itatengeneza Maendeleo Ya Kimwili Na Kiroho.
=Itatengeneza Kufanikiwa Rohoni Na Mwilini.

 Ibada sio kwenda tu kanisani bali ibada ni kutii kile BWANA YESU alisema.
Mathayo 7:9-11 ''Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?''

Inawezekana uchumba wenu umeanzia katika urafiki tu wa kawaida kisha mkawa wachumba na sasa mnataka kuoana, Kama ni mpango wa MUNGU na mnadumisha utakatifu endeleeni lakini kama ni urafiki uliotengenezwa na shetani basi uwe makini sana.
 Kuna Urafiki Ambao Una ROHO MTAKATIFU Ndani Yake Na Kuna Urafiki Ambao Hauna ROHO MTAKATIFU Ndani Yake. Ukiona Urafiki Hauna ROHO MTAKATIFU Ndani Yake Uvunje Maana Huo Ni Urafiki Utakaokuletea Madhara Makubwa Sana Hata Kama Kwa Sasa Wewe Kwa Macho Yako Unauona Kuwa Ni Urafiki Bora.
 Je unaongozwa na nini kupata Mchumba?

Mchumba wako kama atachukua nafasi ya KRISTO moyoni mwako hiyo ni makosa makubwa.
mke kama atachukua nafasi ya MUNGU ndani ya mume hiyo ni sanamu.
mume kama atachukua nafasi ya MUNGU ndani ya mke hiyo ni sanamu.
Ni muhimu sana kila mtu kumpa MUNGU nafasi ya kwanza.
Mathayo 5:14-16 '' Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze BABA yenu aliye mbinguni. ''
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments