WEWE NI NANI KULINGANA NA NENO LA MUNGU?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la Uzima.
Wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Ni Vizuri Kujitambua Kwamba Wewe Ni Nani Kulingana Na Neno la MUNGU, Sio Kulingana Na Familia Yenu Au Ukoo Wenu, Sio kulingana na jamii yako au taifa lako Bali ni muhimu kujua kwamba wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU.
Kama umeokoka wewe ni Mtoto wa MUNGU.
Neno La MUNGU Linasema Kuwa Wewe Ni Mtoto Wa MUNGU;
Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''

Maana Yake Umezaliwa Kiroho Na MUNGU Kupitia Kumpokea Kwako YESU KRISTO.
Mtoto Ana Heshima Yake, Mtoto Ana Haki Zake.
Ukijitambua Kwamba Wewe Ni Mtoto Wa MUNGU Mwenye Haki Zote, Basi Hakika Haki Zako Utazidai Kwa Maombi Na Kupokea. Mtoto Wa MUNGU Ana Sifa Nyingi Lakini Kuu Kuliko Zote Ni Kuushinda Ulimwengu, Biblia Inasema;
"Kila Kitu Kilichozaliwa Na MUNGU Huushinda Ulimwengu; Na Huku Ndiko Kushinda Kuushindako Ulimwengu, Hiyo Imani Yetu-1 Yohana 5:4".

Ndugu Mteule Mwenzangu Wa BWANA YESU. Sifa Ya Watoto Wa MUNGU Ni Kuushinda Ulimwengu Na Mambo Yake Yote. Kama Wewe Ni Mteule Na Bado Dunia Inakushinda Jiangalie Sana, Haiwezekana Uzinzi Na Anasa Za Dunia Vikushinde, Haiwezekani Uongo Na Wizi Vikushinde, Haiwezekani Dhambi Ikushinde. Watoto Wa MUNGU Huushinda Ulimwengu. Kushinda Sio Ombi Ila Ni Lazima kwa wewe mtoto wa MUNGU.
Neno limesema hapo juu kwamba waliombokea BWANA YESU ni watoto wa MUNGU, Je ambao hawajaokoka na haishi maisha matakatifu ni watoto wa nani?
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Biblia inataja wazinzi na wachawi kwamba hawataurithi ufalme wa MUNGU.
Ufunuo 21:8 '' Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.'' 

Je wewe ni mwabudu sanamu, Neno la MUNGU linasema waabudu sanamu sehemu yao ni katika ziwa la moto.
Kama jina lako ni mwabudu sanamu basi badilika leo.
Je wewe ni mzinzi au mchawi kulingana na Neno la MUNGU, Je umeitambua sasa hasara ya kuwa mzinzi?
Biblia inasema kwama waongo na walevi hawataingia uzima wa milele.
Je wewe ni mlevi au muongo kulingana na Neno la MUNGU?
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.'' 

Je Neno la MUNGU linakutambua wewe kama mwasherati, mfiraji au mlawiti?
Je wewe ni Mlevi au mtukanaji?
Sehemu ya watu wa namna hiyo ni katika ziwa la moto.
Kuokoka leo ndio kubadilishiwa jina na kuishi maisha matatifu ndio kuwa mtakatifu kabisa jina lako.
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Huo ni mfano tu wa dhambi chache ambazo ziko katika wanadamu na kwa sababu wanazitenda dhambi hizo, Neno la MUNGU linawaita kwa jina la dhambi hizo.
Unaweza ukajiita kwamba wewe ni mtoto wa MUNGU lakini kama wewe ni mwizi basi hakika wewe sio mtoto wa MUNGU bali kulingana na Neno la MUNGU wewe ni mwizi na wezi wote hawatauridhi uzima wa milele.
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?

Kufanya Kitu Huku Unaelewa Unachokifanya Ni Vyema Sana Kama Kitu Hicho Ni Chema Mbele Za MUNGU. Tunahubiri Injili Ya Wokovu Wa KRISTO Kwa Sababu Tunajua Kwamba Watu Tunaowahubiria Kama Wakimpokea YESU Na Wakaanza Kuishi Maisha Matakatifu Hakika Wataingia Katika Uzima Wa Milele.
Tutaitwa wahubiri wa injili kama ni kweli tunahubiri injili ya KRISTO ya kweli.
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?

Katika Familia, Mzaliwa Wa Kwanza Akipoteza System Ni Rahisi Zaidi Na Watoto Wengine Wa Familia Hiyo Wakapoteza System.
Katika kanisa mchungaji akipoteza systemni rahisi sana kanisa lote kuposteza system.
Je wewe ni mpoteza system au ni nani?
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kama ni mchungaji lakini pia wewe ni mzinzi basi jina lako wewe kulingana na Neno la MUNGU ni mzinzi na wazinzi wote hawana sehemu katika uzima wa milele.
Ndio maana Biblia iko wazi sana ikisema sio wote wamwitao YESU kwamba Bwana Bwana watakaoingia Paradiso.
Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Mathato 7:21-23 ''21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.''

Ndugu, Je Uko Muda Huu Mahali Ambapo MUNGU Anataka Uwe Muda Huu?
Je unayoyafanya muda huu yanampa MUNGU utukufu?
Kama ni mambo mabaya Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kuwa MTEULE sio kazi ndogo, ni kumkataa shetani na watoto wake wote na kukimbilia kwa YESU KRISTO kisha ukajazwa nguvu za ROHO MTAKATIFU na baada ya hapo unamtii
ROHO MTAKATIFU milele.

Kama humtaki YESU Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kama hulitaki Neno la MUNGU Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kama humtaki ROHO MTAKATIFU Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kama hutaki kuishi maisha mataktifu Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
MUNGU BABA tusaidie mimi na huyu anayesoma ujumbe huu ili tuwe WATEULE wa BWANA YESU milele.

Isaya 13:9 ''Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.''

Karama Za MUNGU Hatupewi Kwa Manufaa Yetu Binafsi Bali Kwa Manufaa Ya Kulijenga Kanisa La KRISTO. Kama Unageuza Karama Za MUNGU Ulizopewa Kuwa Mtaji Unakosea Sana.
Wewe uliyegeuza karama kama mtaji Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Kama karama yako unaitumia kuibia watu Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Sisi Wateule Ndio Tunaomtafuta MUNGU Na Sio MUNGU Kututafuta Sisi, MUNGU Alitutafuta Sisi Tulipokuwa Tungali Dhambini, Ili Tuje Kwenye Wokovu Wake, Lakini Wakati Huu Tukiwa Ndani Ya Wokovu Ndio Wakati Wa Kumtafuta MUNGU Na Sio MUNGU Kututafuta Sisi. Tumtafute MUNGU Kwa Maombi, Matoleo Na Utakatifu. Zingatia Hilo Wewe Uliyeokoka Na Utabarikiwa.
Kama humtafuti MUNGU Je wewe ni nani kulingana na Neno la MUNGU?
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments