BWANA YESU NI HAKI YETU YA USHINDI NA UZIMA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Yeremia 23:5-6." Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu. "

BWANA YESU jina lake jingine anaitwa "MUNGU ni haki yetu"
Alipokuja kuungana na jamaa ya wanadamu alichagua kupitia kwenye ukoo Wa Daudi

BWANA YESU ni haki yetu.
✔Kwa sababu ana uzima Wa milele hakika uzima huo ni haki yetu. Tumpokee tu na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Warumi 5:8-11 ''Bali MUNGU aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa KRISTO alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na MUNGU kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika MUNGU kwa Bwana wetu YESU KRISTO, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.''
 
✔Kwa sababu BWANA YESU anaponya magonjwa, kuanzia Leo kupona magonjwa ni haki yako. Kimbilia tu maombezi hakika utapona.
 Mathayo 9:35 ''Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.''
 -Bwana YESU ni haki yetu ya kuponya ndio maana andiko hilo la Luka 9:35 linasema Kwamba Bwana YESU aliponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.

✔Kwa sababu BWANA YESU analinda hakika ni haki yako kuiita damu ya YESU ya uzima ikulinde.
BWANA YESU ni haki yetu.
Kupona ni haki yetu.
Kuwashinda wachawi ni haki yetu.
Kuondoka Kwa laana maishani mwetu ni haki yetu.
Kuwa na ndoa zenye furaha na Amani ni haki yetu maana ushindi wetu uko katika BWANA YESU aliye haki yetu.
Kupata mchumba ni haki yako.
Kufaulu masomo ni haki yako.

Yeye Bwana YESU anasema;
 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:13-14''
 
Kubarikiwa ni haki yako maana BWANA YESU ana kila ushindi na yeye BWANA YESU ni haki yetu.

Ndugu, mkimbilie BWANA YESU aliye haki yetu wanadamu ili akuokoe na kukuponya.

 Hayo magumu unayopitia unayajua wewe lakini MUNGU anajua atakutoa vipi katika hayo magumu kama tu ukiamua kumtegemea kwa maombi na utakatifu.
Amua kumtegemea MUNGU kupitia jina la YESU hakika utavuka salama na saa yako ya kushangilia itafika.

 Kumb 31:8 ''Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.''



 Kuna wakati wa adui kujipendekeza kwako. Akijipendekeza mruhusu ila usimpe siri zako.
Tii Neno la MUNGU maana hilo ndio pekee uzima wako.

Bwana YESU ni haki yetu na ushindi wetu na uzima wetu.


Jiwe walilolikataa waashi nimekuwa jiwe kuu la pembeni.
Waashi ni washika Dini huku wamemkataa YESU.
Waashi wamemkataa YESU ila wameshika Dini tu.
Waashi wamemkataa YESU japokuwa wanajua kabisa kwamba bila yeye YESU hakuna uzima wa milele.
Waliolikataa jiwe kuu la pembeni watajikwaa nalo yaani waliomkataa YESU na Wokovu wake watakwazwa hata na mahubiri ya Neno lake.

1 Petro 2:7-8 "Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa Waashi, Nimekuwa jiwe kuu la pembeni. Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo."

Bwana YESU ni haki yetu ya uzima wetu.
YESU alikuja kutuokoa mimi na wewe, ni jukumu letu tu kumtii na kumpokea kama Mwokozi wetu.
YESU ana upendo wa ajabu sana juu yako, ametuandalia makao mbinguni ili tukishinda ya dunia tukafurahi mbinguni kwa MUNGU milele, ni jukumu letu kushinda mambo ya dunia.
Inawezekama kabisa wakati mwingine unaishi na watu wasiomhitaji YESU lakini ndugu nakuomba hayo yasikurudishe nyuma bali songa mbele na wokovu wa MUNGU kwenye maisha yako.
Wokovu ni kazi ya MUNGU iliyofanyika pale Msalabani ili tu kukuokoa mimi na wewe.
Wokovu ni wa thamani sana na unatakiwa uwe vazi la maisha yetu yote.
YESU alinipenda mimi na wewe ndio maana akaja duniani ili kutuokoa.
Luka 19:10 '' Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.'

Hatutakiwi kuwa na muda wa kupoteza kwa ajili ya uovu tena, YESU ni ushindi wetu na tunakakiwa tu tulishike Neno lake na kulitii.
Biblia ndilo Neno la KRISTO ambalo tunatakiwa tulitii na kuliishi.
Biblia imeandikwa na ROHO wa MUNGU akiwatumia wanadamu waaminifu na kazi ya ROHO wa MUNGU ni kumshuhudia YESU KRISTO kwetu.
Yohana 15:26 '' Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa BABA, huyo ROHO wa kweli atokaye kwa BABA, yeye ATANISHUHUDIA.''

Hakika Bwana YESU ni haki yetu hivyo kila mwanadamu anatakiwa tu kumpokea na kumtii yeye na Neno lake.
 Ni muhimu sana kumpokea Bwana YESU maana nje na yeye hakuna uzima wa milele.
Yohana 14:6-7 ''YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.''

Hakika Bwana YESU ni haki yetu ya uzima hivyo tusonge mbele katika wokovu wake.
Ndugu hata kama watu wote watakutenga, kama ni kwa ajili ya kumpokea YESU wewe usijali bali songa mbele ya YESU KRISTO Mwamba wa uzima wako wa milele.
Dunia itapita na mambo yake yote yatapita lakini uzima wa milele ulio katika KRISTO YESU hautapita kamwe.
1 Yohana 2:12-17 ''Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua BABA. Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la MUNGU linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments