CHAPA ZA KICHAWI

Na Mtume Peter Rashid Abubakar
2 Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.”
Shetani hawezi kuwaletea watu mabaya kabla hajawawekea alama ya ubaya huo, anao ufalme kwasababu yeye ni mafalme wa giza. Kila mtu unayemwona anaishi duniani mambo yanayompata ni sawasawa na chapa aliyo nayo.

“Lolote la kichawi ndilo hilohilo la kishetani” unaweza ukajiuliza kwanini nisiongee upako, karama au mafanikio. Biblia inasema Mungu ameshatupa vitu tayari, Mungu hana uponyaji wetu, Baraka zetu, furaha yetu tayari ameshatupa hata kabla hatujaumbwa lakini yupo azuiaye Baraka hizo ambaye ni shetani na wakala wake.Biblia inasema nitakurudishia afya yako maana yake Mungu alishakupa afya lakini iliibiwa, mahali pengine kwenye Biblia Mungu anasema nitakurudishia miaka yako iliyoliwa na nzige maana yake alishakupa miaka lakini nzige waliila. Wachaiwi, wasoma nyota, waganga wa kienyeji hao ndio wazuiao Baraka zetu na hao ndio tunaoshindana nao na kuwashinda kwa jina la Yesu.
Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.”
ALAMA HIYO NDIYO YA IBILISI.
Mhubiri 9:11 “Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.”

Hili neno bahati limetafasiriwa kama fursa na wakati huwapata wote, maana yake kuna wakati wa fursa kwa kila mtu. Mungu anasema wakati na fursa zinawapata wote. Maisha yametawaliwa na fursa, Mungu akitaka kumbariki mtu hadondoshi Bilioni moja na kama unategemea kuokota umeshakuwa maskini tayari.
Shetani pale mtu anakuwa na wakati wake wa fursa lakini hajui kama wakati wake wa fursa ndio huu, mfano unaweza kuona watu wanasema mweshimiwa fulani angefanya mambo haya au mtu fulani angefanya hivi na hivi baadaye angekuwa mbali sana lakini mweshimiwa huyu au mtu huyu anayezungumziwa hajui na haioni fursa hiyo. Unaweza kumwona mtu fursa anayo au yuko karibu na mtu fulani lakini hajui kama mtu yule ni fursa kwake na ni wakati wake wa kubarikiwa kwasababu amepigwa chapa ya kichawi asione wala asifahamu wakati wake wa kubarikiwa.
Wagalatia 4:4-5 “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.”
Mungu analeta fursa tunaona maisha yanawakati na fursa. Maana yake Mungu huruhusu mambo ya aina fulani yatokee kwa wakati fulani tu. Mfano Musa alizaliwa ili kusudi lake awavushe wana wa Israeli wafike mto Yordan. Kila mtu unayefahamiana naye Mungu ameruhusu ufahamiane naye, uishi naye ili baadaye kuna jambo utafanikiwa kupitia mtu huyo, kabla hujapiga magoti kuomba ishi na watu vizuri kwanza.
“Kabla hujawakimbiza watu angalia wanaweza wakawa ndio“ kunguru wa Eliya aliyekuletea mkate” akili kubwa kuliko zote ni kuijua fursa iliyoletwa na Mungu mbele yako bila kumwangalia mtu”
Mithali 18:16 “Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu.”
Kabla hujakutana na mtu tanguliza zawadi kwanza hata kama umeshaomba. Huu sio wakati wa kumwambia Mungu nipe Mume/mke Mungu ameshakupa tayari huu sio wakati wa kumwambia Mungu akupe mtaji, Mungu ameshakupa vyote ila yupo anayezuia, Kumbuka imeandikwa atakuja mpinga kristo atawawekea watu alama/Chapa ambayo hawataweza kununua wala kuuza.
Ukiri:
“Katika jina la Yesu nafuta chapa zote za kichawi zilizo juu yangu na familia yangu kwa damu ya mwana kondoo”

Shetani anajua wakati na majira, anajua majira ya Baraka za watu na inapofika wakati ule hutuma vuzuizi na balaa ili kuzuia Baraka zisiwafikie watu hao. Kila mtu anawakati wake wa kubarikiwa
Wagalatia 6:17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.”

SHERIA YA UFALME NA MAKOSA
Ufalme wa Mungu tunaouishi unayo damu ya mwanakondoo, Maandiko Matatifu yanasema nawaandikia ninyi watoto msitende dhambi lakini mkitenda dhambi mnaye msaidizi anyewaombea, tena Biblia inasema hata kama dhambi zenu zikiwa nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama sufu, tena imeandikwa zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote” , Zaburi 107:20 “Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”

Kama umepigwa ukaanguka chini,usilale palepale chini ukasema umepigwa hivyo huwezi kuamka tena, simama uanze upya tena, Mungu ni Mungu wa nafasi ya pili usijilaumu hata kama umekosea tena na tena usijilaumu simama uanze kupigana utashinda na kumiliki Baraka zako kwa jina la Yesu.
Kuna wakati unajiskia kwamba huu ni wakati wako wa kubarikiwa lakini unajiona umekosea sana hivyo hustahili, hapana shetani akiona unajiskia hivyo anafurahi sana na kukuzidishia vita, unatakiwa ufahamu hekima ya masumwi kama umepigwa ukaanguka chini usibakie palepale chini maana utahesabiwa kama bado uko palepale chini utashindwa hivyo simama usonge mbele Yesu ameshakusamehe tayari. Haimaanishi utende dhambi tena baada ya kutubu hapana lakini unayonafasi ya kusimama tena na Mungu atakungarisha kama dhahabu utangaa tena na kumiliki miaka yako iliyoliwa na nzige. Simama upigane vita urudishe vyote vilivyozuiliwa na chapa za kichawi kwa jina la Yesu. Amen

Comments