KWANINI BAADHI YA WALIOAMINI WATASHINDWA KUINGIA MBINGUNI?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kwanini watu wengi walioamini watashindwa kuingia mbinguni?
Ni kwa sababu baada ya kuokoka walikaa tu.

Yohana 15:2 "Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na BABA yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa."


MUNGU anapotuokoa anataka tudumu katika wokovu wake na anataka tufanye yale yampendezayo.
Kila Mkristo azae matunda mema.
Ndugu yangu zaa matunda kwa kumcha MUNGU.
Ndugu yangu zaa matunda kwa kuwa kielelezo cha matendo mema.
Ndugu yangu zaa matunda kwa kwa kumtumikia MUNGU.

Ndugu yangu zaa matunda kwa kuombea ndugu zako ili waokoke.
Ndugu yangu zaa matunda kwa kuwashuhudia wengine injili ya Wokovu wa YESU KRISTO.
Ndugu yangu zaa matunda kwa kuishi maisha ya haki matakatifu.
Injili ya Wokovu wa KRISTO inatakiwa iende mbele na anayeweza kuipeleka mbele ni wewe tu uliyeokoka.
Taji huja baada ya ushindi. Tutapewa taji ya uzima baada ya kushinda duniani.
Mtu asiposhinda duniani hawezi kupewa taji ya uzima wa milele. 

 Yakobo 1:12 ''Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, BWANA aliyowaahidia wampendao.''

Ndugu inakupasa sana kuishi maisha matakatifu ya Wokovu ndani ya KRISTO ili uipate taji ya uzima.
Kuishi maisha matakatifu huko ndiko kuzaa matunda kunakotakiwa.
Bila kuzishinda dhambi hakuna uzima wa milele.



1 Yohana 5:18-20 '' Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na MUNGU hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. Twajua ya kuwa sisi tu wa MUNGU; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. Nasi twajua kwamba Mwana wa MUNGU amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake YESU KRISTO. Huyu ndiye MUNGU wa kweli, na uzima wa milele.''
 
Ndugu tafuta kwanza ufalme wa MUNGU na haki yake. 

Hakikisha unamtumikia KRISTO.
Zaa matunda mema ya utakatifu kila siku.

Kataa kuitumia dhambi na jitenge na marafiki wanaowaza dhambi tu.

 Umeitwa na MUNGU ili uupate uzima wa milele hivyo juhudi yako ya kuishi maisha mema katika Bwana YESU itakuwa faida yako ya milele kama ukidumu siku zote.
 Kuna tofauti kati ya kuitwa Mkristo na kuwa na KRISTO ndani yako.
Ni Heri kuwa na KRISTO ndani yako na sio kuwa Mkristo tu kwa jina.

Warumi 8:1-2 ''Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika KRISTO YESU imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. ''

Zaa matunda mema mpendwa baada ya kumpokea YESU.
Ishi maisha matakatifu siku zote itakusaidia sana.
Litumikie kusudi la MUNGU la kuitwa kwako kwenye wokovu wake.
Suleimani alikuwa na mambo mawili moyoni mwake: Kujenga nyumba ya MUNGU na Kujenga nyumba yake.
Je , wewe unajenga nyumba yako na Kujenga kanisa la MUNGU?

Ndugu weka hazina kwa MUNGU itakusaidia baadae na hata uzimani itakusaidia.
Itafute haki ya MUNGU ya kukuita kwake kwenye ufalme wake.

Haki ya kupata kibali kwa MUNGU hupatikanaje?
Haki ya kupata kibali cha MUNGU hupatikana kwanza kwa utii wako kwa MUNGU.
MUNGU hawezi kumtumia mtu asiye na utii.
MUNGU hawezi kumtumia mtu asiye na unyenyekevu.
MUNGU kumtumia mwaminifu na mvumilivu.
MUNGU hataki walegevu katika kazi yake.


Yeremia 48:10A ''Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu;''

Ndani ya mtu mlegevu kuna uvivu na uzembe hivyo huyo hafai katika kumtumikia MUNGU hata akapata haki ya kibali cha MUNGU.

MUNGU hawezi kumtumia mtu mbinafsi. MUNGU hawezi kumtumia mtu asiyesamehe.


Wakolosai 3:12-17 '' Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa MUNGU, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama BWANA alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. Na amani ya KRISTO iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye.''

Unyenyekevu unahitajika sana kwa wanaotaka kibali cha MUNGU katika huduma zao.
Utii kwa MUNGU unahitajika sana kwa watu wanaotaka kumpendeza MUNGU na
kupata kibali chake.
Bwana YESU anawahitaji wanyenyekevu ili awape injili yake waipeleke kwa mataifa.

Baadhi ya walimwamini YESU watashindwa kuingia uzima wa milele kwa sababu walipompokea walishindwa kuzaa matunda mema.
Ndugu zaa matunda mema ya matendo na maisha yako yote.

Isaya 59:2-18 '' lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.  Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.  Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.  Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani. Kwa sababu hiyo hukumu ya haki i mbali nasi, wala haki haitufikilii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu. Twapapasa-papasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao waliowanda tumekuwa kama wafu. Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi. Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua; katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate MUNGU wetu, tukinena jeuri na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni. Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia. Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA  akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki. Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia. Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho. Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.'' 
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments