MAMLAKA ZA KIROHO NA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO

Na Mchungaji Adriano Makazi, Ufufuo na uzima
Luka 22:53-54 “Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali.Bwana Yesu ametuoyesha kuna mamlaka za giza ambazo zinaweza kumshikilia mtu, lakini ni vizuri kujua kuna roho zilizo kifungoni.”
1 Petro 3:18-19 “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri”

Kati ya mateso ambayo Yesu alipitia moja wapo ya kusudi lilikuwa ni kutuleta kwa Mungu. Watu wengi maisha yao hawafanikiwi kwasababu wamewekwa vifungoni ambapo hawawezi kutoka ndani yake, mtu anaweza kuonekana ana migogoro na matatizo na mambo yake haiendi vizuri kumbe kuna tatizo laki fungo cha rohoni.
Luka 3:16-17 “Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Marko 5:25-29‘Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.”

Huyu mama alikuwa kifungoni, ametokwa na damu na kuzunguka sehemu mbalimbali kutafuta msaada ikashindikana mpaka alipokutana na Yesu. Kuna watu wanaumwa moyo, wanaumwa mgongo, wanaumwa magonjwa ya kila aina lakini kumbe wamefungwa.
Matatizo yote hutatuliwa kwa namna ya kiroho yakatatuka kabisa lakini ukiyatatua kwa namna ya kibinadamu yanakuwa hayaondoki kabisa bali hujirudia tena na tena. Tumeona huyo mama alikuwa amezunguka kila sehemu ili aponyoke kifungoni alikuwa ana pepo wa udhaifu.
Biblia inasema mwanamke huyu alikuwa kwenye hali hiyo miaka kumi na miwili na alienda kila mahali akashindwa kupata ufumbuzi. Bila shaka alienda kwa wganga wa kienyeji lakini ikashindikana akachoka kuzunguka kila mahala akasikia habari za Yesu na ndipo alipamua kwenda nyumbani kwa Bwana na kuamua kulishika vazi la Yesu na mara akapona saa ileile.
Yesu anazo nguvu ambazo hatujazigusa bado, kuna nguvu zipo ndani ya Yesu hata leo ili aweze kuponya, huyu mama aliondoka akiwa mwenye kwa imani akalishika vazi la Yesu akapona kabisa.
Kama shetani anaweza kumfunga mtu basi anaweza kufunga hata biashara ya mtu, anaweza kufunga hata elimu ya mtu ionekane ni bure, kuna wajanja wa dunia hii wanaweza kukuzuia usifankiwe kwenye ulimwengu wa roho, unatakiwa ufahamu maarifa ya kuwapiga wampaka wakuachie kwa jina la Yesu.
Marko 11:1-4 “Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.Wakaenda zao, wakamwona mwana-punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua.”
Yesu anawatuma wanafunzi wake akawaambia nendeni kwenye kijiji kile kinachowakabili mtamkuta mwanapunda amefungwa mfungueni mumlete nina haja naye. Wale ambao Yesu anataka awatumie kwa kazi yake huwa anawafungua kutoka vifungoni na kuwatumia.
Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.
Luka 8:2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
Mariamu alikuwa kwenye kifungo, Yesu alimfata akamfungua na mapepo saba ambayo yalitolewa ndani yake akaanza kumtumikia Mungu. Hata leo hii inawezekana kuna watu wapo tayari kukusaidia lakini hawawezi kwasababu wamefungwa wasikuvushe hapo ulipo.
Kuna watu wengi leo hii wamefungwa wameshindwa kuyafanya yale ambayo wamekusudiwa. Watu wengi huomba Mungu awasaidie lakini hawajui kuwa Mungu hawezi kuja yeye kama yeye kwasababu ni Roho, Mungu huwasadia watu kupitia watu.

Kikwazo kimoja wapo ambacho kinawazuia watu wasimtumikie Bwana ni kifungo, hauwezi kumtumikia Bwana ukapata Baraka kama upo kwenye vifungo, Mungu huwafungua watu kutoka kwenye vifungo ili waipeleke injili. Injili inapelekwa na watu, sio wote wanaweza kuipeleka injili bali wengine wanaweza wakafanya kazi na biashara ili washiriki kuipeleka injili mbele kwa mali zao.
Mungu alimwambia Ibrahimu wakati alipokuwa bado hajapata mtoto kuwa atamfanya taifa kubwa, inamaana Mungu anaweza kuongea na mtu kwa habari ya mambo yajayo.
Mwanzo 15:12-15 “Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.”
Maana ya kuwatumikia watu wengine nikwamba unaweza ukawa umeajiriwa unafanya kazi kwa bidii lakini haufaidiki na kitu chochote kutoka kwao, inamaana miaka yako yote unawafanyia wao kazi kubwa lakini yale unayoyapata ni madogo hayalingani na kiwango cha akili ulichotoa, hayalingani na nguvu ulizotoa. “Kila jambo ambalo halijaanza na Mungu limeanza kwa uchawi,ushetani.”
Yoeli 2:25 “Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.”
Mungu anasema atakurudishia miaka yako uliyoibiwa na hao watu. Mungu anasema unaweza ukawa unatumikishwa lakini baadaye utatoka mahali hapo na mali nyingi.
Yusufu alikuwa ana nyota ukimweka mahala mali yako inaongezeka, Yusufu alipitia kwenye shida nyingi mpaka akaishia gerezani akawa anatafasiri ndoto inatokea. Siku moja Farao akaota ndoto akakosa mtu wa kuifasiri hivyo Yusufu peke yake ndiye aliyeweza, Yusufu aliitafasiri ndoto ya Farao akafanywa kuwa waziri mkuu juu ya nchi ya Misri akakusanya vyakula na haikutokea njaa kwenye nchi ya Misri wakati huo, inamaana kama kuna sehemu akiwapo mtu wa Mungu basi hapo hapatakuwa na njaa.
Biblia inasema ndugu zake Yusufu walikosa chakula lakini walikuwa wanahela wakaamua kwenda Misri ili wapate chakula.
“Mwota ndoto hafi mpaka ndoto yako itimie”, kila magumu unayoyapitia fahamu sio kwa bahati mbaya bali ni njia inayokupeleka kwenye ndoto yako. Njia za Mungu hazichunguziki usikate tama maana Mungu ndiye amebeba njia yako anataka akupeleke mahala alipokuandalia.
Ukoo unaweza kukutenga lakini usikate tama maana, Mungu anaweza kumtumia adui yako ili akupeleke mahala alipokuandalia, Sio kwa maombi yako ndipo ufike pale ulipoandaliwa na Bwana bali Mungu anajua mahali uendapo yeye pekee.
Mfano mwingine kwenye Biblia, Sauli alipoteza Punda wa Baba yake, Baba yake akaamuru aondoke nyumbani mpaka punda apatikane, (Zamani Punda alitumika kama usafiri, ingekuwa leo hii ni kama gari). Ayubu alipoondoka alifika yeye na msaidizi wake wakamtafuta nabii mwonaji kwanza ili awajuze mahali punda alipo.
Mungu alisababisha tukio Sauli atoke kule aliko ili akutane na Samweli, (Lakini Samweli naye alikuwa hakai mahali hapo walipokutania). Sauli alipofika kwa Samweli, aliambiwa Bwana ameshampa habari zake lakini si za Punda bali za kuwa mfalme wa Israeli, mara moja alimiminiwa mafuta akafanywa kuwa Mfalme wa taifa la Israel. (Sauli aliondoka nyumbani kwao akiwa amefukuzwa akarudi akiwa Mfalme wan chi.)

Kuna wakati mwingine matatizo uliyonayo sio kwa bahati mbaya bali Mungu alikuwa anamtafuta ili ampeleke mahali anapostahili. Hata wewe hapo ulipo usikate tama sababu Mungu anakutafuta uwe kama alivyo kusudia uwe. Hata leo Mungu anakutafuta simama utafika kwa jina la Yesu. Wachawi na washirikina yale mambo wanayokufanyia wanakupeleka kwenye hatima yako, usimtendee mtu mabaya sababu hujui baadaye utakutana naye sehemu gani, hata kama upo mahali unafanya jambo kwaajili ya watu usiwafanyie kwa ujanja ujanja maana hujui jambo litakalokupata baadaye ukakutana nao mahali wakakusaidia.
Yusufu alipokuwa waziri mkuu wa Israeli, aliwapokea ndugu zake bila kinyongo akawaombea hifadhi kwa Mfalme, eneo lililoitwa Gosheni, baadaye mfalme huyo akafariki akaja akainuka Mfalme ambaye hamjui Yusufu akaanza kuwatesa wana wa Israeli mpaka miaka 400 ya utumwani ikapita ndipo wakamlilia Mungu akawasikia akamtuma Musa kama mkombozi wao. Taifa liliondolewa mikononi mwa farao kwa kutumia mtu mmoja, inamaana Mungu huwasadia watu kupitia watu, mara nyingi wale watu waliotumwa kwaajili ya majukumu ama ya kitaifa, ama ya kifamilia, ama ya Injili huwa wanamatatizo mengi yanawaandama. Wengine wametolewa ndani ya miili yao wamewekwa kifungoni.
Tumeona kumbe mtu anaweza kufungwa kwasababu ya kusudi ambalo liko ndani yake, shetani hana shida na watu bali anashida na kile kilicho ndani yao, unaweza kujiuliza mbona fulani yuko vizuri japo ni mlevi, mzinzi, mkatili n.k kumbe hana kitu ndani yake lakini wewe unakitu kwaajili ya kuwasaidia watu wengine hivyo ndiomaana unapatwa na shida na changamoto nyingi kwenye maisha yako.
Matendo ya Mitume 5:12-18 “Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;hata ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao.Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza”

Biblia inasema Kuhani mkuu na masadukayo watu wa dini, wakawakamata na kuwatia gerezani, inamaana kuna watu leo hii wamefanikiwa kidogo wakakamatwa na kuwekwa gerezani,
wamekuona unaanza kustawi wakasema haiwezekani tumkomeshe ikatokea wakatoa karafa unaanza kushuka na wale mpaka watu ambao ulikuwa unawasaidia hauwaoni tena, hata wale waliokuwa wanakusalimia huwaoni tena wamebaki wanasema hiyo ni nguvu ya soda tu kumbe ndio hao waliokufunga kwa waganga.
Biblia inasema walipowekwa gerezani, Malika wa Bwana akawafungulia akasema enendeni mkaifanye kazi yenu tena, enendeni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu:- kuna watu waaina mbili wapo wanaokusukuma ili uharibikiwe na wengine wapo wanaokusaidia, imeandikwa yeye aangukaye mara moja atainuka tena.

“Biblia inasema hakuna jambo gumu lisilomshinda Bwana, yote yanawezenaka kwake yeye aaminiye, nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”
Nguvu unaipata unapoanza kulisoma neno la Mungu. Ukilijaza neno la Mungu kwenye nafsi yako utaishinda kwa jina la Yesu. Leo hii yapo magereza ya kiroho unamwona mtu anatembea lakini yupo gerezani, mtu aliye gerezani maisha yake huwa magumu sana sababu kuna watu wenye wivu wamemweka gerezani kwasababu ya wivu. Wapo wanaokupangia mipango ya kukaa gerezani lakini hutakufa bali utaishi uyasimulie matendo makuu ya Bwana.
Matendo ya Mitume 16:24-28 “Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.”
KULINDWA KIFUNGONI
Wakina Paulo walikuwa wanalindwa na kufungwa kwa mikatale ili wasitoroke, ina maana kuna watu leo hii wamewekwa kwenye vifungo na kuwekewa ulinzi wa kutokuamini injili ya Mungu ili waendelee kubaki ndani ya kifungo hicho bila kutoka. Kuna watu wamefungwa kwa mashetani ya kulinda ili kwamba abaki kwenye kifungo. Silaha nyingine ya kulindwa ubaki ndani ya tatizo ni kujifanya mjuaji kwenye kila jambo. Watu wengi huwa wanakwenda kwa utaratibu wao wenyewe kwasababu ya kukosa uvumilivu na kuwa na tabia ya ujuaji.
Petro alikua anajua taratibu za kuvua samaki ni usiku lakini Yesu alipomwambia tupa nyavu, hakubisha wala kusita bali alisema kwa neno lako nashusha nyavu na walipata samaki wengi kuliko kawaida, inamaana kwa Yesu ni lazima ufate neno lake kama asemavyo kwa imani na utafanikiwa sababu unakuwa umetii na kuvunja mapenzi yako binafsi.

Kifungo cha utii kinaweza kukukosesha mambo mengi, kwenye mambo ya Mungu ili mtu abarikiwe ni lazima atii na aanzie chini ili Mungu amtengeneze kwaajili ya Baadaye na kumweka juu. Amen

Comments