MAUTI ILIYOTENGENEZWA

Na Mchungaji John Kilima, Ufufuo na uzima Tanga.

UTANGULIZI: Mauti siyo tukio Mauti ni roho ambayo inaweza kuvaa umbo la kitu chochote,
Mtu anaweza akawa anaishi lakini,ipo mauti ndani yake ambayo inawekwa na wachawi,na waganga wa kienyeji ikiwa inasubiri kutimiza kusudi lao
•ufunuo 6:8 Nikaona na tazama farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyempanda jina lake ni mauti,na kuzimu akafuatana nae,nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi wauwe kwa upanga,na kwa njaa,na kwa tauni,na kwa hayawani wa nchi•
-Mauti ilikua imepanda farasi na kuzimu pia ilikua imepanda farasi, Wakapewa mamlaka ya kuua,
•Kazi ya mauti ni kuua
•na kazi ya kuzimu ni kuhifadhi ndo maana mauti anatangulia na kuzimu anamfuata nyuma.
•Yeremia 9:20-21 Lakini lisikieni Neno la Bwana,enyi wanawake na masikio yenu yapokee Neno la kinywa chake,mkawafundishe binti zenu kuomboleza,na kila mmoja na jirani yake kulia kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu ipate kuwakatalia mbali watoto walio nje na vijana katika njia kuu•
-hapa tunaona mauti inapandia madirishani, tukio haliwezi kupanda dirishani lakini mauti ina roho kamili yenye akili inayoweza kutumwa kwako ikatafuta sehemu mojawapo katika mwili wako ikatulia kusubiri muda iliyoelekezwa kufanya kazi
-unaweza ukawa huumwi na sehemu yoyote katika mwili wako na bado mauti ikawa ipo ndani yako,ndio maana kunaweza kutokea ajali kukawa na majerui wengi lakini akafa mtu ambaye hata hajachubuka kwa sababu mauti ilikua inamtafuta yeye.
•2wafalme4:40 Basi wakawapakulia hao watu ili wale ikawa walipokuwa katika kula chakula wakapiga kelele wakasema,mauti imo sufuriani ee mtu wa Mungu wala hawakuweza kula•
-unaona hapa mauti ikaonekana ndani ya sufuria
•2Samwel 22:6 kamba za kuzimu zilinizunguka mitego ya mauti ikanikabili•
-Kuzimu ni roho, ambayo kama roho zingine,inaweza ikavaa umbo au kujigeuza na kuwa kitu chochote ndio maana hapa imejigeuza ikawa kamba,
Kamba za kuzimu zikikuzunguka mauti inapata uraisi zaidi kukukabili au kukushambulia moja kwa moja kupitia mitego kama magonjwa,ajali,kifo, n.k

INFORMATION MINISTRY
UFUFUO NA UZIMA TANGA:

Comments