SHUHUDA MBILI KUTOKA KANISANI EFATHA.

Mtume na Nabii Josephat Mwingira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Efatha.
SHUHUDA:
Naitwa Melania Shao napenda Kumshukuru MUNGU kwa mambo makubwa aliyonitendea. Niliokoka mwaka 2010 lakini niliingia Efatha mwaka 2011 na mwaka 2012 nilipewa nafasi ya kuwa Kiongozi. Nikiwa mjamzito nilijifungua mwanangu akiwa mzima lakini baada ya miaka 3 alibadilika akawa anavimba hadi kushindwa kutembea akawa hakuwi, nikampeleka hospitali na baada ya kupimwa na wataalam wakagundua haumwi chochote. Siku moja nilimleta mtu Kanisani Kuombewa, Mchungaji Mdadila alipomaliza kumuombea huyo mtu akamuona mwanangu akiwa anacheza akaniuliza yule ni mtoto wa nani? nikamwambia ni wa kwangu akaniambia mbona simuoni mtoto? Nilikuwa napenda sana kumuweka urembo kichwani na kumsuka dreds Mchungaji akamnyoa nywele na kumuombea na mwanangu alipokea uponyaji na alianza kukua kama watoto wengine kwa sababu alipokuwa na miaka 5 alionekana kama mwenye miaka 3. Namshukuru sana MUNGU kwa kuweza KUMPONYA Mwanangu na sasa ana miaka 10 na Amerefuka.

Mwaka 2013 nilibeba mimba ya mwanangu wa pili na mimba ikawa ni ya miezi 12, nikaambiwa natakiwa nifanyiwe upasuaji kwa sababu ilikuwa kila nikipimwa inaonekana kuwa mtoto amesimama na alikuwa hageuki. Mimi nilikataa kwa kuwa Baba yetu Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira anatufundisha kuwa watoto wetu wasitokee dirishani bali pale alipoingilia ndipo atokee. Siku moja kukawa na Ibada ya SHUKRANI Kanisani na niliombewa niliporudi Nyumbani nikaenda hospitali kupima ikawa Mtoto wangu amegeuka na wiki iliyofuata nikajifungua salama.
Melania Shao
Baada ya hapo mwanangu tena akawa hakui na haongei, akawa mwembamba sana nikaambiwa nimpeleke India lakini nikawa nahudhuria kwenye maombi na sasa AMEPONA na alianza kuongea akiwa na miaka 3 na sasa ana miaka 5. Namshukuru sana MUNGU kwa aliyonitendea kwani kama siyo YEYE wanangu wote wangekuwa hawakui.
Mtu wa MUNGU usikate tamaa katika jambo unalopitia AMINI ipo siku yako kwa MUNGU, MUNGU Anaweza na ATAKUSHINDIA. Unachotakiwa ni wewe KUTII na KUFANYA kile Unachoelekezwa na Watumishi wa MUNGU Mfano:- KUWALETA Watu kwa YESU yamkini ndiyo ikawa SIKU yako ya wewe Kupokea UPONYAJI wako.


USHUHUDA!! USHUHUDA!
NAITWA THERESIA ATHANAS MOSHI
Natokea Kilimanjaro KDC, wiki iliyopita nilipigiwa simu na mwanangu anayeishi Dar kuwa amepitiliza siku zake za kujifungua na kwamba ameambiwa ajiandae kwa upasuaji (Operation) kwa ajili ya kujifungua maana mtoto alikuwa hajageuka.

Nikamwambia asiende kwanza hospitali anisubiri nakuja, nilipofika nikaja moja kwa moja Kanisani hapa Efatha Ministry Mwenge, Dar es Salaam, nikaonana na Mtumishi wa MUNGU Mchungaji Mwakisole, nikamweleza mwanangu ameambiwa atajifungua kwa upasuaji, Mchungaji AKAOMBA akasema atajifungua salama kwa njia ya kawaida, ila msimpeleke hospitali hadi uchungu utakapoanza.
Uchungu ulipoanza tukampeleka hospitali, manesi waligomba kwa nini tumemchelewesha, maana alitakiwa kuwahi kwa ajili ya upasuaji, mimi nikamwambia mwanangu hatajifungua kwa upasuaji. Wakasema haiwezekani maana mtoto hajageuka na mtoto akiwa katika hali hii huwa tunafanya operation ili kuokoa maisha ya mama na mtoto hivyo ni lazima apasuliwe.
THERESIA ATHANAS MOSHI
Nikampigia Mch. Mwakisole nikamweleza, akasema niweke simu kwenye tumbo aongee na mtoto, nikaweka akaomba. Baada ya hapo hali ya mwanangu ikawa mbaya akaanza kutapika hadi, kuishiwa nguvu. Akakimbizwa chumba cha upasuaji, mimi nikatoka nje nikimshukuru MUNGU.
Katika hali isiyo ya kawaida mtoto akaanza kutoka haraka kwa miguu akamalizia na kichwa, hadi manesi wakashangaa na wao walikiri kuwa ni MUNGU aliyefanya.
Wakaniambia usiache kumshukuru MUNGU kwa jambo hili.
Ndio maana nipo mahali hapa Kumshukuru MUNGU maana alisema kupitia Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kuwa sio sawa kujifungua kwa operation, bali mtoto anatakiwa kutoka kupitia njia ALIYOINGILIA. Namshukuru pia Mchungaji Mwakisole kwa kuwa pamoja nami, MUNGU ambariki sana. MUNGU HASHINDWI

Comments