YESU KAMA ALFA NA OMEGA

Na Mtumishi Nickson Mabena

*Sehemu ya pili*
Nianze kwa Swali, Ulifanya homework iliyopita?.
Baada ya somo hili pia, kutakuwa na homework nyingine!.
Tuliangalia kwa kifupi, kuhusu nafasi alizonazo Yesu, ambazo anazitumia kutenda kazi!.
Nataka nikuonyeshe Nafasi hii, ya ALFA NA OMEGA anavyoweza kuitumia, kutenda kazi..
Alfa na Omega maana yake ni Mwanzo na Mwisho!.
Yesu akija, kama Alfa, maana yake anakuja na NGUVU YA KUANZISHA JAMBO, alafu atakujq kulikamilisha hilo jambo kwa sababu yeye ni OMEGA!.
Nimewahi kufundisha kwamba kuna upako wa ALFA NA OMEGA, Upako huu, unakuwezesha/unakusaidia, Kuanzisha Vitu na Kuvikamilisha (Bila Kuishia Njiani),
Si unajua kuna watu wanaanzisha vitu, alafu wanashindwa kuvimalizia?,
Mimi nilikuwa na huo ugonjwa, nasoma kitabu, alafu nashindwa kukimalizia!.
Tunatofautiana, Mwingine, Anaanza Uchumba, alafu haufiki mwisho, unavunjika katikati,
anaanza Shule, hamalizi, anaishia njiani,
Anaanza ujenzi, anakwama njiani..
Hii ya ujenzi, wakati mwingine inasababishwa na roho zinazotawala eneo,
Kuna roho, inaitwa SPIRIT OF INCOMPLITNES,
Ni roho inayoweza kutawala eneo, Watu wa Eneo husika, wakijenga nyumba, hawazikamilishi, bila sababu zinazoeleweka!.
Wewe uliyeokoka, kama upo kwenye eneo kama hilo, unaweza ukawasaidia, watu hao kwa kuzifukuza hizo roho!.
Nitumie mfano mmoja, wa Kwenye Biblia, Yesu alipokuwa na Wanafunzi wake!.
*"Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapende chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano"* MATHAYO 14:22
Inavyoonyesha wanafunzi wa Yesu, hawakuwa tayari kupanda chomboni, kwenda Ng'ambo!.
Ndio maana Yesu akatumia 'ukubwa' flani Kuwalazimisha hata Wakakubali Kwenda!.
Wakati natafakari, nikajifunza hata kwetu inaweza ikatokea,
Yesu anaweza 'akakulazimisha' kufanya jambo flani, au kuanzisha kitu flani,
Kwa sababu zako za Kibinadamu, Ukakataa kufanya!.

Ni Neema tu itokee, ukubali, kama walivyofanya wakina Petro!.
Uliambiwa ufanye nini, ukakataa?, hadi pale ulipolazimishwa ukakubali?,
Nyinyi mliajiriwa Serikalini, au Mnaosubiri Ajira, unaweza ukapelekwa eneo usilolitaka, kama ungepewa nafasi ya kuchagua kwa kweli ungekataa, lakini ndio UMELAZIMISHWA HIVYO😂😂.
Wanafunzi wa Yesu walikutana na misukosuko ya Kutosha, njiani, na walisahau kabisa, Kama SAFARI YAO ALIYEIANZISHA NI ALFA NA OMEGA!.
Yesu akatokezea, na kuwatia moyo ili wamtambue!.
*"Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope"* MATHAYO 14:27
Hilo neno, NI MIMI.. maana yake, Ndiye niyeanzisha safari yenu, MSIWE NA SHAKA, maana yake, Ndiye niliyefanya kwa Wengine, na kwenu nitafanya hivyo, MSIOGOPE..
Kwa hiyo, na wewe, kwenye jambo lolote, uliloanza na Yesu kama ALFA, alafu unaona misukosuko, ukimuita, atakuja kukutia moyo, na kukupa uhakika wa kufika mwisho salama, kwa sababu yeye ni OMEGA pia..
Nahisi hiyo sentensi, haijaeleweka vizuri, ni hivi, Yesu akianzisha jambo lolote, anajua kulitimiliza, kwa sababu yeye ni Alfa na Omega!.
Kwenye Imani hii tuliyonayo, Biblia inatufundisha vizuri sana,
*"tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu;* ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu" WAEBRANIA 2:2
Aliyeanzisha imani yetu, ataitimiza tu, Aliyeanisha safari ya Wokovu ndani yetu, atatufikisha tu Mbinguni,
Haijalishi magumu tuliyonayo, ni kwa kitambo tu, tutafika salama, tutafika salama hakika!.

Ninapokaribia kumalizia, nikupe shauri,
Jambo lolote, unalotaka kuanza, anza na Yesu!.
Ukianza na Yesu, Utafika salama safari yako!.
Utajijingea mazingira mazuri ya kuja kutetewa na Yesu, pale bahari inapochafuka!,
Ukiwa miongoni mwa watu Wanaishia njiani kila safari unayoianzisha, Ujue unamuhitaji Yesu kama ALAFA NA OMEGA,
Unayetaka kwenda Kuanzisha Huduma sehemu, nenda kaanze na Yesu huyu,
Kama upo katikati ya misukosuko, muite Yesu kama Alfa na Omega!.
Wakina Petro walivuka,
*"Na walipokwisha kuvuka*, walifika nchi ya Genesareti" MATHAYO 14:34..

Yesu ni Alfa na Omega, Hakika Utafika Mwisho, hakika Utavuka,
Litumie somo hili kwenye Maombi, Jifunze Kumuita Yesu kama Alfa na Omega, pale inapobidi!.
Nina imani kuna ulichojifunza kupitia ujumbe huu,
Uweke kwenye matendo, ili ukuletee matokeo mazuri!.

USISAHAU; IMANI BILA MATENDO IMEKUFA!.
Homework; Tafuta kwenye Biblia, Utendaji kazi wa Yesu katika nafasi mbalimbali, tulizoziona kwenye somo hili, na ulizoongezea kwenye homework iliyopita!.
-Mfano, Yesu alipofanya kama Mwalimu, au kama Mchungaji, n.k
Naitwa,
Mwl. Nick
0712265856
(WhatsApp)

Comments