(Christmas) Kutoka chini na kuinuliwa juu

Na Askofu Dk Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

Dunia ina pande mbili upande wa usiku na upande wa mchana, kama Tanzania kukiwa na mchana marekani kule ni usiku, Watu wengi wanadhania Yesu alizalila tarehe ishirini na tano mwezi wa 12 jambo ambalo sio kweli.Tarehe 25 mwezi wa 12 karibu kila sehemu duniani huwa kuna nuru ndiomaana ikachaguliwa tarehe hii kama kumbukumbu ya nuru ya Yesu kuingia duniani, kwenye tarehe hii hata kama sehemu nyingine duniani kuna giza mbala mwezi huwa inawaka kwenye sehemu hizo.
Sukukuu ya Christmas sio muujiza wa kuzaliwa kwa Yesu kristo bali, Muujiza wa kuzaliwa kwa Yesu ni ule uwezekano wa kuzaliwa kutoka kwenye mavumbi na kuketishwa na wakuu. Dunia imejaa na mtazamo kwamba kwenye kabila hilo hawawezi kutoka Raisi wa nchi, au kwenye familia hii hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa akaenda nje ya nchi, au kwenye taifa hilo hakuna mtu ambaye anaweza msaada.
Sisi Christmas inatufundisha kwamba watu wanaweza kutoka kwenye mavumbi na kuinuliwa na kukaa na wakuu. Christmas sio kukutana pamoja na kula pilao na nyama na kwenda disko, bali kuzaliwa kwa kristo kwetu sisi ni matumani ya uhamisho, ni matumaini baada ya kufa kuna nchi inaitwa mbinguni ndipo makazi yetu ya asili yalipo.
Christmas kwetu inamaanisha aliyepuuzwa anaheshimiwa tena, aliyeitwa mwenye pepo baadaye anaitwa Mungu na mfalme wa yote, Christmass kwetu inamaanisha aliyedharaulliwa na kutukanwa anaitwa tajiri na mfalme.
"Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni." Luka2:1-6
Watu wengi wanadhania Yesu kristo alizaliwa maskini jambo ambalo si kweli, Siku zile kulikuwa na kauli ya amri kutoka kwa Kaisari kuwa watu wote waende kwenye miji yao wakahesabiwe katika sehemu walikozaliwa (ili unabii na andiko litimie, Yesu atazaliwa Bethlehemu).
Yohana 7:41 "Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?"
Yusufu na Mariamu walipoenda Bethlehemu ambako huko ndipo alipozaliwa. Yusufu alisafiri na Mariamu kilometa 111 kwenda kuhesabiwa Bethlehemu. Biblia inasema walipofika kule Bethlehem zile siku za kuhesabiwa zilitimia na kulikuwa na watu wengi wamerudi ili kuhesabiwa jambo ambalo lilisababisha wakakosa nafasi ya kulala, huku Mariam akipatwa na uchungu wa kujifungua.
Kila mahali kulikuwa kumejaa mpaka Yesu akaenda kuzaliwa kwenye zizi la ngombe, Sio kwamba Yesu alizaliwa kwenye umaskini hapana, Mungu aliruhusu mazingira ya umaskini yatokee ili kutufundisha kuwa unaweza ukaanzia kwenye hali ya chini na baadaye ukaja ukaketishwa juu, kwenye hali ya uchumi Yusufu alikuwa anauwezo sababu alikuwa anakazi ya ufundi.
Tumejazwa uweza kutoka kwa yeye aketiye juu na tutafika kule tuendako kwa msaada wake, kuzaliwa kwa Yesu kunatuonyesha kwamba japo kila mahali kumejaa na hakuna msaada, japo kazi zote zimeshikiliwa na watu, japo hakuna upenyo wa kupita kwenye biashara na doa, na elimu, kila mahali kumejaa, viwanja vimejaa, lakini Mungu amekuandalia mahali pa hali ya chini sana akusaidie uanzie pale ili baadaye uje usimamee uitwe mtu mkuu.
Mungu anaweza kukutoa mahali pale ulipo akakusimamisha na kukupa jina jipya, Mungu anayo njia kwenye maisha yako.
Yesu alizaliwa kwenye zizi la ng’ombe sio kwasababu alikuwa maskini bali Mungu aliruhusu matendo ya kimaskini yatokee ili tujifunze. Hata kama ungekuwa tajiri kiasi gani huwezi kufika mahali ukakuta hoteli imejaa ukataka atolewe mtu ili wewe ukae
“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.” Marko 6:3
Kwa wayahudi Yesu anaonekana mtoto haramu ndiomaana wanamwita mtoto wa Mariamu, Lengo la Christmas ni wale wasio na tumaini, walikosa thamani wapate tumaini jipya na kuinuka juu.
Mathayo 13:55-56 “Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?”
“Wengi wao wakasema, Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?” Yohana 10:20
Christmas ni kwaajili ya wale waliopuuzwa walioitwa wanamapepo, wamebadilisha dini, walioitwa wamepotea na kuchanganyikiwa na kudharauliwa.
“Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.” Mathayo 2:13
Kutoka Bethelemu kwenda Misri ni kilomita 690 na kipindi kile kulikuwa hakuna gari, wala guta ‘ Yesu alizaliwa kwenye maisha ya masumbufu na adui yake alikuwa mkubwa maana alikuwa ni mkuu wa nchi, Christmas ni kwaajili ya waliotishiwa kuuwawa wameandaliwa mahala pa kupumzika, usiogope kuna mahala umeandaliwa pa kupumzika mbali na watesaji, mbali na wasumbufu Mungu ni mwaminifu na anazo njia za kukuhifadhi utafanikiwa kwa jina la Yesu.
Unaona kilomita zile walizo safari kwa wakati ule na Biblia haijasema ni siku ngapi walitembea huku wakijificha Mfalme asiwakamate lakini walitembea umbali huo wakafika Misri na kujifichia huko.
Christmas kwetu sisi ni kumtoroka adui wako, magonjwa, laana, mikosi, umaskini, kuelekea 2017 uwatoroke adui zako kwa jina la Yesu.
Baa ya Mfalme kufa, Yusufu alitokewa na malaika tena akamwambia arudi Nazareth na sio Bethlehemu kwasababu aliyetaka kumuua Yesu ameshafariki. kutokea Misri kwenda Nzarareth ni kilometa zaidi ya 700, Christmas kwetu sisi maana yake ni kurudi kwenye asili yako. Kurudi kwenye asili yako kuna umbali mrefu lakini Mungu ndiye akufikishaye usikate tama simama songa mbele utafika kwa jina la Yesu.
Malaika alimpa Yusufu taarifa kwamba walioitafuta roho ya mtoto waiuwe wamekufa ndipo Yusufu aliporudi Nazareth. Mwaka 2017 walioitafuta roho yako wafe ili urudi kwenye asili yako kwa jina la Yesu Kristo.
“Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,” Mathayo 2:19
Hii ndiyo Christmass tunayoisheherekea ambayo Yesu alizaliwa kwa shida akakimbilia kwenye nchi ya ugenini baadaye akaja akapewa jina lipitalo majina yote.
Kuzaliwa kwa Yesu ni kutoka chini kwenye mavumbi kwenda juu, Mungu akuinue juu kw
a jina la Yesu

Comments