HABARI NJEMA ZA KUFUNGA MWAKA 2016 NA KUUMILIKI MWAKA 2017.

Mwalimu Samwel Kibiriti

Bwana Yesu asifiwe rafiki yangu, napenda nikushirikishe habari hizi njema za Ufalme wa Mungu.
Kuna taarifa njema za masomo na vitabu naomba nikushirikishe.
Kile Kitabu cha KUUSAMBARATISHA UFALME WA WACHAWI ninakamilishwa kuandaliwa tatizo umeme ulisumbua ila baada ya muda mfupi nitawatangazieni ili mkipate. Ni katikati ya mwezi huu kitakamilika.
Lakini nimejaribu kuandaa maosomo mbalimbali na kuyaweka kwenye mfumo wa Pamphlet/pafekti kama ifuatavyo:
( i ) PAMPHLET/PAFEKTI LA KWANZA LA KITABU
Hiki kitabu cha pafekti kimebeba masomo yafuatayo
( 1 ) Je Maisha yako hayamo mikononi mwa Waovu?
( 2 ) Vita kati yetu na Wakuu wa Giza
( 3 ) Ardhi ya Eneo ulilopo ikiumwa ni nini Madhara yatakayotokea Eneo hilo?
( 4 ) Utajuaje kwamba Unamilikiwa na Madhabahu za miungu migeni?
Kuna ishara nimefundisha za kukutambulisha kwamba uko chini ya umiliki wa miungu migeni
( 5 ) Jinsi ya kumuombea Mgonjwa ambaye Shetani na wachawi wanataka kumuua kabla ya Wakati wake
Hapa nimeeleza kwa kina jinsi gani ya kumuombea mgonjwa wenu ili asife kabla ya wakati wake
( 6 ) Vita vya Kimazingira
Na kila somo limefundisha kwa kina na nimeweka muongozo wa Maombi yenye Nguvu za Roho Mtakatifu ambayo utayaomba ili uweze kuwa huru.
( ii ) PAMPHLET/PAFEKT LA PILI LA KITABU.
Hiki kitabu cha Pafekti kimebeba masomo yafuatayo:
( 1 ) Haki ambazo umezipoteza kupitia kutenda dhambi.
Unahitajika umuombe Mungu azirejeshe tena kwako.

( 2 ) Shetani akitaka kukutawala kwenye maisha yako na kutawala kila kitu chako anapitia kwenye maeneo yafuatayo rohoni
Watu wengi maisha yao yanatawaliwa na shetani pamoja na vitu vyao lakini hawajui shetani kapita wapi, somo hili linakjonyesha maeneo shetani anayopita ili kukutawala, na yako maombi ya nguvu ya kuuondoa utawala wa shetani kwako.
( 3 ) Siri iliyojificha kwenye pesa
Wengi pesa zimekuwa changamoto kwao kuzipata au kutokufanya mendeleo majibu ya kuijua fedha kiroho yamo humu.
( 4 ) Muongozo wa Maombi ya kujifungua kutoka chini ya minyororo ya roho za mizimu ya Ukoo wenu
Wengi wetu wameokoka kweli lakini roho za mizimu zinawatesa sana, maombi haya yatakufungua na kukuweka huru kabisa.
( 5 ) Siri iliyojificha katika Ndoto unazoota
Watu wengi sana huteseka kwenye ndoto pata uhuru kupitia somo hili na nimeweka muongozo wa maombi ya kuombea ndoto unazoota ili mbaya zisitimie kwako na Nzuri zitimie.
Naandaa Pamphlet/Pafekti la tatu ambalo litabeba Aina kama 40 za maombi mbalimbali yenye Mpenyo wa kiroho ambayo unatakiwa kuyaomba kila siku. Baada ya muda mfupi tu kitabu cha Pafekti hiki kitakuwa tayari.
UTARATIBU UKO HIVI:
Kama unahitaji nikutumie masomo hayo niliyoyaandaa yenye Maombi ya Nguvu za Roho Mtakatifu kwa njia ya Email popote ulipo duniani uniambie na kunitumia Email yako.
Na kama uko mikoani na Unahitaji kuyapata masomo na vitabu hivyo pia utaniambia Mkoa uliopo.
Ghalama ya kila kitabu cha Pamphlet/Pafekti la Masomo hayo mbalimbali niliyokueleza hapo juu ni Shilingi 5000 ( Elfu Tano )
Nimetoa kwa ghalama hiyo kama sadaka yangu kwa Mungu ili kukusaidia wewe na kila mmoja kuyapata maarifa haya ila huko mwakani nitakapoyaingiza kwenye mfumo lasmi wa vitabu ghalama yake itaongezeka kwa kila kitabu kukinunua na nitayatenga hayo masomo kwenye vitabu hayatakuwa kama hivyi kwamba kitabu kimoja kubeba masomo sita kwa pamoja hapana.
Usichelewe kujipatia Ofa hii ya kufunga mwaka na kuanza mwaka kwa Maarifa haya ya Neno la Mungu na maombi.
RATIBA YANGU YA HUDUMA
Nitakuwa na ratiba ya huduma baada ya muda mfupi ujao.
Kwahiyo kwa wale rafiki zangu walioko mikoa ya Dar na Arusha na Kilimanjaro na Tanga n.k nitapita huko sasa unaweza kuniambia ili nikipata mkoani kwako nikuletee Vitabu hivi vya Pafekti.
Kuhusu ghalama ya kukipata kitabu cha kuusambaratisha Ufalme wa Wachawi nitawaambieni kikishakuwa tayari
Kwa mawasiliano nami utanipata kwa namba hizi
Vodacom 0765 867574 ( WhatsApp )
Tigo 0673 784197
Airtel 0785 855785
Mimi ni rafiki yako Mwalimu Samwel Kibiriti
Mungu Baba akupatie wepesi katika kila eneo la maisha yako.

Comments