Kusudi la Mungu katika kizazi chako

Na Askofu Dk Josephat Gwajima.

“Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.” Matendo ya Mitume 13:36
Kila mtu anakusudi la Mungu kwenye kizazi chake. Daudi alikuwa anakusudi la Mungu kwenye wakati wake alipomaliza kulitumikia alilala. Kila mtu aliye hai anakusudi la kuishi, awe budha, awe imamu, awe mchungaji au mtu yeyote analokusudi la Mungu katika kizazi chake.
Leo tunasafiri dunia nzima kwa muda mfupi sababu kuna watu walikua wanakusudi lao kuwezesha jambo hilo hapa duniani wakalitumikia na walipomaliza wakafa. Mtu hawezi kufa mpaka ile sababu ya yeye kuwa duniani inapotimia.
Wachawi, wafuga majini, wadaluashi, washirikina, wasoma nyota na wengineo wao kazi yao ni kupindisha kusudi lako ili usilitimize hapa duniani.
Leo duniani kuna watu bilioni saba na hao wote haijalishi kama kuna wabaya au wazuri lakini kila mtu analo kusudi lake lililomfanya aishi hapa duniani. Hata wale wabaya wanakusudi lao kwa siku ya ubaya. Hakuna mtu hata mmoja ambaye hana maana hapa duniani haijalishi umbile lake au rangi yake au namna yeyote ile anavyoonekana, kila mtu analokusudi hapa duniani.
Kuna wakati unaweza kujiona hauna maana sana kwasababu haujasoma, au unajiona hauna maana katika jamii, unatakiwa ufahamu hilo halizuii kusudi lako lisitimie.Mungu amempa kila binadamu uwezo wa kuanza kutimiza kusudi lake hapa duniani na kumaliza.
Wakristo wengi wanaelimu ndogo sana juu ya namna ya kuishi hapa duniani lakini wanaelimu nyingi sana juu ya mbinguni kule tutakako kwenda.
Bahati nzuri sisi tuliookolewa ni kondoo tusioliwa katikati ya mbwa mwitu. Hatukubali kuliwa na mbwa mwitu kwenye ndoa, kwenye biashara, kwenye kazi, kwenye elimu au sehemu yeyote ile kila mwanaume au mwanamke ambaye ni jeshi la Bwana.
Haijalishi wale wanaokuwinda ili wazuie lile jambo lililondani yako lisitimie. Hautakufa wala familia yako haita kufa, mpaka utimize kusudi la Mungu juu ya maisha yao litimie na kila atakaye fanya silaha juu yako haitafanikiwa kwa jina la Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai.
“Mungu afungue macho yako na akili yako na moyo waku uuone ulimwengu ujao ili wale waliopanga mabaya juu yako uwaone wakilia na wao waliofanya vita juu yako wabaki wakilia na kushangaa matendo ambayo Mungu amekutendea mbele yako kwa jina la Yesu.”
“Hakuna uganga juu ya Yakobo wala uchawi juu ya Israeli”
MAKUSUDI YA KUZIMU
Mtume Paulo alikuwa na kusudi lake la kuishi juu ya nchi.
“Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.” Matendo ya Mitume 9:15-16
Hakuna maisha ya kutengeneza mwenyewe, wanaokutengenezea maisha ambayo hujaitiwa wapigwe kwa jina la Yesu.
Wapo watu wanatoa kafara ili wawainamishe watu wasiongee jambo lolote wala kuuliza maswali wakiwa kazini au sehemu yeyote, kuna mtu anatoa kafara ya umasikini, kuna watu wametoa kafara ya utajiri ambao hauwezi kumsaidia mtu yeyote aliye ndugu yake, yake. Wapo waliotoa kafara ili wapate vitu au kuwazuia watu kwenye nyadhifa mbalimbali, wote hawa ni wapindisha makusudi ya watu ambao wanatakiwa kupigwa kwa jina la Yesu.
Mungu ametupa utajiri unaodumu ambao si ule unaopewa leo na kesho unayanganywa.
Nabii Eliya alipoibuka alikuwa hana muda wa kuhubiri Injili kwa watu kwasababu shauri lake yeye alikuwa anawashughulikia wachawi tu wanaokwenda kinyume na Mungu. Siku moja Eliya alisimamisha mvua kwa muda wa miaka mitatu na mbua haikunyesha mpaka alipoiruhusu yeye. Eliya alikuwa amesimama kwenye kusudi lake na kusimamisha mvua kwa muda wa miaka mitatu na nusu na halikuwa jambo gumu mbele yake kwasababu lilikwua ni kusudi lake.
Nasisi tunakusudi la kutokuwasamehe wachawi kwasababu ni kusudi letu kuwafyeka na kuwaangamiza kabisa. Wao wanakwamisha ndoa za watu, wanazuia biashara za watu wanaoharibu afya za watu kila siku sio watu wa kuwaacha na kuwasamehe dawa yao ni kuwaondoa juu ya nchi na kuwapiga kwa jina la Yesu.
Eliya alikuwa anakusudi la kufunga mvua na kuwazuia wachawi alitimiza kusudi lake na muda wake ukaisha ulikaisha akamfuata Yehu akamtia mafuta akawa Mfalme..
“Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.” 1 Wafalme 19:15-18
Yehu alipopakwa mafuta tu awe Mfalme wa Israeli aliwaalika waganga na wachawi na wasoma nyota Ikulu yake wakiwa wamevaa nguo zao rasmi sawasawa na kazi zao.
Yehu aliwaangamiza wachawi wote siku ile na Biblia inasema hivi ndivyo Yehu alivyoangamiza kizazi cha Baali na alipomaliza kuwaangamiza alimwendea mke wa Mfalme na kumwangamiza.
“Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana.Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.” 1 Samweli 28:5-14
Huyu mtu wa Mungu ameenda kwa mganga wa kienyeji kumpandisha mtu kutokea kuzimu. Sauli alienda kumpandisha Samweli kutojea kuzimu baada ya kuona Mungu amemwacha wala hamjibu tena na mara baada ya kumpandisha hakuwa na muda wa kumuuliza kama yeye ndiye Samweli wa kweli au siye.
Sauli alikuwa ameachwa na Mungu hivyo hakuweza kumwita Mungu tena ndiomaana akaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji. Cha ajabu yule samweli aliyepanda kwa Mganga akamwambia Sauli kama Bwana amekuacha kwanini kunifata mimi, pia mtu huyu aliyepanda kutokea kuzimu alikuwa anaongea mambo mabaya juu Sauli na kumhakikishai kesho yeye na wanawe watakuwa naye Kuzimu.
Tnaona Sauli alianguka kwasababu ya maneno ya Yule mchawi. Mapenzi ya kutokea kwa shetani yalikuwa kuangamiza familia yake na yote aliyoongea Yule mchawi yalitokea vilevile.
Yale mambo mabaya unayotamkiwa na wachawi usiyapuuzie maana yanaweza kukupata unatakiwa uyatengue kwa jina la Yesu.
Kama wachawi na waganga wanaweza kusema mapenzi ya kuzimu yakatokea, sisi pia tunaishi leo kwasababu ya makusudi ya Mungu juu yetu yatimie kwa jina la Yesu.
Sauli alipigwa mshale akafa, mwanaye alipigwa akafa kwasababu ya yale makusudi ya kutokea kuzimu.
“Mapenzi ya kuzimu juu ya familia yangu hayatatimia kwa jina la Yesu.”
Alijiona hawezi tena afadhali afe na akafa kama alivyowaza. Kulikuwa na uwezekano wa Sauli kutokufa lakini alikuwa hajui kwamba Bwana ni Mungu wa nafasi ya pili anaweza kumwokoa tena. Tatizo alilopata Sauli ni tatizo lililotokea kuzimu na akakubali kushindwa.
Kama jambo ambalo linawaangamiza wakristo wengi ni uoga.
“Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili.Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli.Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia.Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako.Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda.Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo;kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.” 1 Samweli 28:9-25”
Unaweza ukawa unaishi lakini kuna shauri la kuishi au kusudi la kuishi unalitimiza lilopangwa kutokea kuzimu, Sauli na watoto wake walikufa kwasababu ya shauri lililotokea kwa mchawi aliyepandisha roho kutokea kuzimu ambayo ilikuwa ikitoa mambo mabaya juu yake nayo yakatokea.
“Futa mashauri yote yaliyotamkwa juu yako na familia yako kwa jina la Yesu.”
“Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.” 2 Samweli 16:23
MSHAURI WA DAUDI
Daudi alikuwa anamshauri mmoja ambaye yeye alikuwa akikushauri ni sawa sawa umeshauriwa na Mungu. Utawala wote wa Daudi ulikuwa umeimarika kutokana na ushauri wa Ahithofeli ambaye alimsaliti. Daudi alikuwa anawasiwasi kwasababu Ahithofeli alikuwa amemsaliti na kwenda kutoa ushauri wa kumwangamiza kwa mwanaye.
Daudi alikuwa anajua shauri la Ahithofeli lilkikubalika amekwisha hivyo akamwita Hushai aende akalibatilishe shauri la ahithilfe. Absalom alipowaita washauri wote akawaambia “namchukia Baba yangu Daudi nataka nimwangamize niendelee kutawala, wakati ule Hushai alienda nay eye akijifanya kama amemsaliti Daudi.
“Kuna watu wanaweza kuingia kwenye maisha ya mtu ili wapindishe mashauri yake”
Ahithofeli alitoa wazo na hushai alikuwa naye alijua yupo pale kubadilisha shauri la Ahihofeli na akafanikiwa, Ahithofeli alipoona shauri lake halijatekelezwa akaenda kujinyonga sababu alijua Daudi atarudi ikulu. Kesho yake Absalom alienda kwa Daudi ili apigane naye na akapigwa akafa sababu shauri la mtu ambaye anasema kweli limepindishwa.
Kwenye maisha yako ya kila siku wapo wapindisha mashauri, wanaweza wakawa wapo kazini, wapo shuleni, wapo nyumbani na kila mahali wapo kwaajili ya kupindisha shauri lako ili usifike kule unapotakiwa kufika.
Kusudi la Kimungu limepindishwa na watu, adui anaweza kupanda mabaya ndani ya mtu.
Wanaopindisha mashauri yako, wanaona mbele yako kuna jambo kubwa unaloweza kulifanikisha ndio wanaokaa ndani yako. Mashetani wanaweza kukaa ndani ya mtu, unaweza ukawa unapatwa na magonjwa, una hasira, mvivu kumbe umewekewa mapepo ambayo yanapindisha shauri/kusudi la maisha yako lisiwe.
Ndoto ya mtu inaendana na maisha ya kila siku sawasawa na unavyoishi. Lakini wapo wapindisha mashauri wametumwa kupindisha mwonekano wako uwe wa tofauti, akili yako iwe ya tofauti, mawazo yako yawe tofauti na uanze kuwachukia wale wanaokusaidia na uanguke ufe.
Mpindisha mashauri anaweza akawa mtu anakushauri jambo ili akutenge a chanzo cha nguvu zako.
Siku zote kwenye maisha shetani atakutumia wabadilisha mashauri au tukio lolote kubadilisha shauri la maisha yako ili usifikie hatima yako.
Kuna sababu kwanini uko hai na haujafa, haijalishi hali ilivyo au watu wanasema nini au umefanya makosa mangapi ilimradi umerudi kwa Yesu. Yesu anakupokea saa ileile kama umekosea na umesema Bwana nimekosa naomba unisamehe, anakupokea kama hujafanya kosa lolote.
“Kwa jina la Yesu ninaamuru wapindisha mashauri waliokuja kwenye maisha yangu naamuru achia kwa damu ya Yesu, naamuru achia Elimu yangu kwa jina la Yesu, achia ndoa yangu kwa jina la Yesu, naamuru wapindisha kusudi langu kwa sababu ya dhambi naamuru achia maisha yangu kwa jina la Yesu. Omba kwa bidii amuru walikuja kwako kupindisha kusudi au shauli lako hapa duniani wahame kwa jina la Yesu. Amen

Comments