![]() |
Mwinjilisti John Chinyuli, Mkurugenzi Mkuu wa Rudisha watu kwa YESU kampeni na mbeba maono ya Shindano la Mitihani ya Biblia Tanzania. |
Shalom mteule wa MUNGU popote uliko.
Awamu ya tano ya shindano la mitihani ya Biblia linafanyika Mwezi huu tarehe 17 Jijini mbeya katika ukumbi wa shule ya St Mary Kadege.
Je,Wewe ni Mkirsto harafu uko Jijini Mbeya au nje ya mbeya na utapenda kushiriki Shindano
hili zuri la mitihani ya Biblia mwaka huu?
Ni rahisi sana sana wasiliana na wahusika kwa namba zifuatazo ili wakuelekeze maana washinda watapata zawadi nzuri sana.
Namba za wahusika ni 0767 592989 au 0712 592989.
Au wasiliana nao kwa Email hii
mashindanoyamtihaniwabibliatz@gmail.com
mashindanoyamtihaniwabibli
Zawadi ya Mshindi wa kwanza ni Laptop Mpya kabisa yenye warrant ya mwaka mmoja, Nafasi ya Kushinda zawadi hii nono ni ya kwako safari hii na na Mshindi wa pili atapata Smart Phone Mpya ya kisasa. Mshindi wa tatu atapata Fedha Taslimu Tsh. 70,000/= na jambo la kukumbuka ni kwamba washindi 30 wa mwanzo kila mmoja atapata Zawadi.
Wahi sasa maana hujachelewa.
Vituo vya Usajiri,kama unataka kushiriki Shindano fika ujisajili kabla ya tar 10/12/2016
-Ofisi za Soma Biblia Mkoa wa Mbeya - Kabwe Stand
-Radio Baraka - Kadege
- Radio Ushindi - Isyesye
-Dukani kwa Kalinga - Mbalizi
-Umoja wa Kujisomea Biblia(UKB) Dukani kwa Mwakisembeja -Mwanjelwa(karibu na stand ya Tukuyu ya Zamani)
-Iyunga Moravian
-Ofisi za Soma Biblia Mkoa wa Mbeya - Kabwe Stand
-Radio Baraka - Kadege
- Radio Ushindi - Isyesye
-Dukani kwa Kalinga - Mbalizi
-Umoja wa Kujisomea Biblia(UKB) Dukani kwa Mwakisembeja -Mwanjelwa(karibu na stand ya Tukuyu ya Zamani)
-Iyunga Moravian
Unaweza pia kujisajili kwa Mpesa au Tigo pesa kwa namba hizi 0767 592989 au 0712 592989.
Ni kwa sababu Biblia ni Neno la MUNGU lenye ushindi na uzima ndani yake.
Kwa mshiriki kupitia kusoma Biblia na kufanya mitihani hakika utakuwa umeongeza kiwango chako cha uelewa wa Neno la MUNGU na kwa njia hiyo utakuwa umekuwa kiroho na kuwekwa huru maana kazi za Neno la MUNGU ni;
1. Kukupa uhakika wa mpango wa MUNGU juu ya maisha yako.
2. Kukuweka huru.
3. Kukufanya ujitambue na utambue kwamba unatakiwa ufanyeje ili umpendeze MUNGU.
4. Neno la MUNGU ni taa ya kukumlikia ili utembee nuruni mwa YESU KRISTO.
5. Neno ni silaha kuu ya kukufanya umshinde shetani.
6. Neno la MUNGU ni pumzi ya MUNGU yenye uhai na uzima.
7. Kukuongezea Imani yako.
Maandiko yanasema juu ya wanaosoma Neno la MUNGU na kulishika na kulitii;
Yohana 8: 31-32 ''Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi MKIKAA KATIKA NENO LANGU, mmekuwa WANAFUNZI WANGU KWELI KWELI;
tena MTAIFAHAMU KWELI, nayo hiyo kweli ITAWAWEKA HURU.''
Neno la MUNGU hupa Nguvu za kuomba.
~Ikumbukwe kwamba neno ni mbegu, maombi ni kama maji. Mbegu pasipo maji kamwe haikui,bali hufa pia maombi pasipo neno la MUNGU hayana muelekeo mzuri. Neno la MUNGU litakuongoza katika maombi yako ya kwamba nini cha kuomba na nini si cha kuomba kwa wakati. Tazama maisha ya akina Danieli,Hanania,Mishaeli na Azaria,wakaomba ,maana walikuwa na maarifa ( Danieli 2:17-19)
Neno la MUNGU ni la muhimu sana ndio maana tunakukaribisha kwenye mtihani wa Biblia ili uongeze maarifa ya MUNGU kupitia kulisoma neno la kulifanyia mitihani na kushinda.
Ubarikiwe.
Comments