UNASUBIRI NINI KUOKOKA?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuokoka Maana Yake Ni Kusalimisha Maisha Yako Chini Ya Utawala Na Uongozi Wa YESU KRISTO.
Kuokoka Ni Jambo La Lazima Kwa Mtu Anayeutaka Uzima Wa Milele. 
Kuokoka Ndio Kuokolewa  na Mwokozi ni mmoja tu yaani MUNGU kupitia YESU KRISTO.
 '' Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna KRISTO, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna MUNGU duniani. Lakini sasa, katika KRISTO YESU, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake KRISTO. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.-
Waefeso 2:8-14 ''

Kuokoka Sio Kuhamia Dhehebu Fulani Lakini Kama Dhehebu Lako Mafundisho Yake Yanakataa Kuokoka Basi Dhehebu Hilo Ni La Kulikwepa Kama Ukoma, Ni Dhehebu La Kulikimbia Hakika. Tangu Zamani Walioutaka Uzima Wa Milele Waliokoka ndivyo Biblia inavyofundisha.

Matendo 16:30-32 ''kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?  Wakamwambia, Mwamini Bwana YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la BWANA, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.''

 Hivyo Kuokoka Ni Muhimu Sana. 
Kama Hujaokoka Nakuomba Uokoke Leo, Hiyo Ndio Injili Ambayo BWANA YESU Ameniambia Niihubiri Masikioni Mwa Kila Mtu.
Marko 16:15-16 ''Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.''

 Hata Kama Jina Lako Ni Zuri Na Watu Wanalisifia Sana Jina Hilo Lakini Kama Jina Hilo Halimo Katika Kitabu Cha Uzima Cha BWANA YESU Ni Hasara Kwako. 
Hata Kama Jina Lako Ni Maarufu Sana Mitaani Na Duniani Kwa Ujumla Lakini Kama Jina Hilo Halimo Katika Kitabu Cha Uzima Cha BWANA YESU Ni Hasara Kuu Kwako.
 Hata Hivyo Hujachelewa Sana Kuandikwa Jina Lako Katika Kitabu Cha Uzima Maana Ukimpokea YESU Leo Na Ukaanza Kuishi Maisha Matakatifu Utaandikwa Jina Lako Kwenye Kitabu Cha Uzima Na Utakuwa Umeokoka.
Bwana YESU mwenyewe anasema 
'' Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za BABA yangu, na mbele ya malaika zake..-Ufunuo 3:5''

  Ndugu zangu, Umaskini Ukiwa na KRISTO Ni Heri Kuliko Utajiri Ukiwa Na shetani. 
Form 4 Ukiwa Na Umeokoka Ni Heri Sana Kuliko PHD Ukiwa Na shetani. Utajiri Ni Mzuri Sana Ukiwa Umeokolewa Na BWANA YESU. 
Elimu Ni Ya Muhimu Sana Ila Uwe Umeokoka. Ingawa Maendeleo Ni Ya Muhimu Sana Lakini Ni Muhimu Pia Kujua Kwamba Maendeleo Bila Wokovu Wa KRISTO Ni Hasara.
  Ndugu zangu, hizi sio nyakati za kujifurahisha dhambini, ni nyakati za kutubu na kuokoka.
Dunia imeharibika na shetani amejichagulia kundi lake kubwa sana.
Wanadamu Wamejamiiana Na Wanyama. 
Wazinzi Wameendelea Kujamiiana. 
 Waasherati Wameendelea Kujamiiana. 
Wanaume Kwa Wanaume Wameendelea Kujamiiana. 
Wanawake Kwa Wanawake Wameendelea Kujamiiana. 
Ndugu Wa Damu Wameendelea Kujamiiana Na Mzazi Kwa Mtoto Nao Hujamiiana. 
Neno Moja Tu Muhimu Kulijua Kwa Sasa Ni Kwamba "HIZI NI SIKU ZA MWISHO". 
Ewe Mteule Wa MUNGU Shika Sana Taji Yako Ya Uzima Uliyoipata Kwa Wokovu Wa KRISTO Asije Mtu Akakunyang'ang'anya.
'' Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;-1 Petro 1:14-15 ''

Ni nyakati za kuishi maisha matakatifu.
Ni nyakati za kuishi maisha ya haki na kweli ya MUNGU daima.
Mtu Mkweli Hupanda Ukweli Na Mtu Muongo Hupanda Uongo. Ni Heri Muongo Akabadilika Leo Na Kuanza Kuwa Mkweli.
MUNGU ana kusudi jema na wewe ndugu, MUNGU anakutaka uokoke.
Usilikwepe kusudi la MUNGU la Wokovu maishani mwako.
MUNGU Akiwa Na Kusudi Na Wewe Huwezi Kukwepa, Hata Ukimbilie Wapi Huwezi Kubadilisha Kusudi La MUNGU. Anza Kumtii MUNGU Na Acha Kiburi Bali Anza Kumtumikia MUNGU.

  Jifunze Kumtii MUNGU na Neno lake.
Jifunze kuishi maisha matakatifu ili baadae uwasaidie na wengine ili waokoke.
Kubali maonyo ya MUNGU juu yako na tengeneza njia zako.
Wengine MUNGU anataka mtumike katika utumishi kwenye kanisa lake lakini dhambi zenu ndizo zimezuia. Ndugu kubali kukemewa na Neno la MUNGU leo na litii Neno hilo la MUNGU.
Kama Hujawahi Kukemewa Ni Ngumu Sana Na Wewe Kuja Kuwakemea Wengine Katika Utumishi Wako. 
Kama Mchungaji Ni Butu Ni Rahisi Sana Kuwafanya Butu Anaowaongoza. 
Kadri Utii Wako Kwa KRISTO Ulivyo Ndivyo Na Watu Watakavyokutii Wewe.
Kuhama dhehebu ni uamuzi wako lakini kuokoka ni jambo la lazima kama unauhitaji uzima wa milele.
Dhehebu halimpeleki mtu mbinguni lakini wakati mwingine mafundisho mabaya ya dhehebu la mtu yanaweza kumpeleka mtu jehanamu.
Ukienenda Kimwili Utakufa Kiroho.
  Barabara Ya Mbinguni Kwa MUNGU Imenyookaa Wala Haina Konakona, Inahitaji Tu KRISTO, Utakatifu Na ROHO MTAKATIFU Ndipo Utafika Kwa MUNGU.
 Kuna Tofauti Kati Ya "Kuokoka?" Na "Kuokoka." 
 Wenzako Leo Wanaokoka Wewe Unabaki Ukisema "Kuokoka?". Usipookoka Ndugu Unaweza Kujikuta Siku Ile Unasema "jehanamu?" Kipindi Ukielekea Huko Jehanamu Na Huku Wenzako Ambao Waliokoka Wako Uzima Wa Milele Kwa Sababu Hawakuacha Kuokoka Bali Waliokoka. 
Hata Leo BWANA YESU Anaokoa, Ukimpokea Leo Unaokoka, Ukiishi Maisha Matakatifu Katika Yeye Utaingia Uzima Wa Milele. Amua Vyema Na Utabarikiwa.
Yeye Bwana YESU anasema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.-Mthayo 11:28''

 Kama Mwalimu Wa Kufundisha Neno La MUNGU Ninajua Kabisa Kwamba Wanafunzi Wangu(japokuwa Sio Wote ni Wanafunzi) Wanahitaji Tu Niwafundishe Ufafanuzi Wa Ndoto Na Masomo Ya Baraka Za Duniani, Lakini Mwenye Neno Ambaye Ni ROHO MTAKATIFU Hunipa Zaidi Ujumbe Wa Kuwaonya Watu Na Kuwatahadhalisha.
Ndugu zangu ni saa ya kuokoka.
Ni saa ya kuacha dhambi zote kisha chukua hatua ya kumpokea Bwana YESU na anza kuishi maisha matakatifu katika yeye.
Ni saa ya kuachana na uzinzi na uchawi kisha mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Ni saa ya kuachana na uongo na wizi kisha mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Ni saa ya kuokolewa na Bwana YESU.
MUNGU Hajawahi Kubadilika. JEHOVAH Jana Alikuwa MUNGU, JEHOVAH Leo Ni MUNGU Na Kesho Yote MUNGU Atabaki Kuwa Ni MUNGU Tu.
 Nje Na JEHOVAH Hakuna Mungu Ila Kuna miungu Tu. 
Na katika JEHOVAH ndiko kumeandaliwa uzima wa milele kwa watii kupitia YESU KRISTO.
Wanadamu Au Mashetani Wanaojiita Mungu Ni Kwa Sababu Wanaiita Jehanamu, Maana MUNGU Halisi Ni Mmoja Tu Naye Ni JEHOVAH Aliyejifunua Kwetu Katika KRISTO YESUNa ROHO MTAKATIFU.
 Yeremia 10:6 ''Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.''
Ndugu chagua vyema leo kwa kumpokea Bwana YESU mwenye uzima wako wa milele.
Mimi niliyeokoka Biblia inasema kwamba mimi
   "...... Ni Hai, Wala Si Mimi Tena, Bali KRISTO Yu Hai Ndani Yangu-Wagalatia 2:20".
Hata wewe nfugu ukimpokea YESU KRISTO leo kama Mwokozi wako na unaanza kuisha maisha mataktifu katika yeye hakika yeye YESU atakuwa hai ndani yako na utakuwa mshindi na mbarikiwa daima.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana

Comments