JEHOVAH NI MUNGU MWENYE NGUVU ZOTE, MKIMBILIE UKAE SALAMA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Katika Mkesha Wa Kuukaribisha Mwaka 2014 Yaani Siku Ya Mwisho Ya Mwaka 2013 BWANA Alisema Nami Kwamba "NIMEKUFUNGULIA MLANGO AMBAO HAKUNA AWEZAYE KUUFUNGA-Ufunuo 3:8".
Mlango Wa Utumishi, Mlango Wa Mafanikio Na Mlango Wa Ushindi. Nimemuona BWANA YESU Katika Utukufu Wake. Nitamtukuza Yeye Siku Zote Ambazo Atanipa Kuishi. Hakika Nitamtukuza Milele.
Mwishoni mwa mwaka 2014 nilipewa ujumbe wa kufundisha kwa mwaka unaofuata yaani 2015, nilipewa ujumbe wa Mathayo 3:2  inayosema
 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
 Hata kama ningefundisha somo gani lakini jambo kubwa zaidi lilikuwa kuwaambia watu watubu maana ufalme wa MUNGU umekaribia.

Mwishoni mwa mwaka 2015 kipaombele changu cha kufundisha 2016 kilikuwa ni Matendo 3:19  inayosema ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''

Namshukuru ROHO wa MUNGU  maana mwishoni mwa mwaka jana yaani 2016 alinipa Yeremia 10:6  inayosema '' Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza.''

Huo ndio ujumbe wangu kipaombele wa kufundisha mwaka 2017.
Ni nyongeza njema nimepewa yaani nitafundisha kwa vipaombele vyote tangu 2013 hadi cha wakati kwa pamoja nitavifundisha.
 
Huu ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda maana hakuna hata  mmoja aliye kama JEHOVAH MUNGU wetu, yeye ni mkuu na katika yeye kuna uweza mkuu sana.
MUNGU wetu ni JEHOVAH maana yake ni MUNGU mwenye KUOKOA.
Kwanini ukimtegemea JEHOVAH katika KRISTO utashinda?
Ni kwa sababu  ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote-Zaburi 83:18''
MUNGU wetu yu juu ya wote na juu ya vyote.
Anaweza yote na anawapenda wateule wake katika KRISTO.
Huu ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU kwa utakatifu na maombi.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kumkataa shetani na mambo yake yote.
Ni mwaka ambao ukiutumia vizuri kwa YESU hakika utakutana na baraka kuu za MUNGU.
Kwanini MUNGU akubariki mwaka huu?
Ni '' kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37''
 
MUNGU wetu anaweza yote.
Umewategemea sana waganga wala hukufanikiwa, ndugu okoka sasa ana anza kumtegemea MUNGU Muumbaji wako.
Umeitegemea sana kazi yako lakini sasa mtegemee MUNGU na hakika utashinda.
Mtegemee MUNGU kwa maombi huku ukiishi maisha matakatifu safi sana ya wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.
Je kuna jambo lako lolote la kumshinda MUNGU?
Yeye MUNGU wetu anasema  ''Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?-Yeremia 32:27 ''

Hakika hakuna la kumshindaMUNGU wetu.
Ndani ya MUNGU wetu kuna Mwokozi wetu wa kipekee sana, Ni  YESU KRISTO Mwana wa MUNGU aliye hai.
Ni Mwokozi anayeweza yote pia.
Anaponya magonjwa yote hata kama yameshindikanaje.
Biblia inathibitisha kwamba anaponya magonjwa yote na sio baadhi ya magonjwa tu.
Mathayo 9:35 ''Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na NA KUPONYA MAGONJWA YOTE  na udhaifu wa kila aina.''

 Nampenda huyu Mwokozi anayeponya magonjwa yote.
Ndugu ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda. 
Nakuambia hivi, ukimtegemea MUNGU mwaka huu kwa maombi na imani thabiti huku ukiishi maisha matakatifu katika Bwana YESU hakika utashinda na zaidi ya kushinda.

MUNGU wetu anatupenda sana na ndio maana akaamua kutuletea Wokovu.
Ameandaa Wokovu kwa mwanadamu atakayependa kuokolewa.
Yohana 3:16-18 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''

MUNGU wetu ameandaa wokovu na wokovu huo ulio wa thamani sana uko pekee katika KRISTO YESU.
Wokovu ni kazi ya MUNGU pale msalabani ili kutuokoa.
Wokovu ni mpango wa MUNGU kumtafuta mwanadamu na kumuokoa kwa ajili ya uzima wa milele.
Maisha ya wokovu ni maisha ya ushindi dhidi ya dhambi.
Ni muhimu sana kila mwanadamu kuingia katika wokovu wa MUNGU ulio pekee katika KRISTO.
Ni muhimu kila mtu kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.
Ndugu yangu mwaka huu ni mwaka ulipewa na MUNGU ili uishi kwa kumtii MUNGU na Neno lake.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
MUNGU wetu anaweza kukushindia lolote lile linalokukabili kama tu ukimtegemea yeye kwa maombi ya imani na utakatifu. 
Yeye mwenyewe MUNGU anasema ''Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.-Isaya 43:19''

Hilo ni neno la kiunabii likiwa na maana kwamba MUNGU anaweza kukushindia katika lolote 
Kwa nini usimpende MUNGU wako aliyekuumba?
Kuna sababu nyingi sana za kumtegemea MUNGU na kumwabudu yeye peke yake.
Kwanza MUNGU ameumba mbingu na dunia 
Mwanzo 1:1 ''Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.''
Ukijua tu kwamba ni JEHOVAH ndiye aliumba mbingu na dunia na vyote vilivyomo basi hakika hiyo tu moja ni sababu ya kumtukuza na kumwabudu siku zote na kumtii maana hakuna muumbaji mwingine ila yeye.
Kama wapo wanaojiita waumbaji basi ni majoka tu ya kuzimu hayo yakihadaa wanadamu ili yawaingize jehanamu.
MUNGU wa kweli ni mmoja tu na ndiye MUNGU wa Biblia aliyejifunua katika utendaji kazi wa sehemu tatu yaani uumbaji, ukombozi na  utakatifu.
 
Ndugu yangu usiache kumtegemea MUNGU kwa maombi maana atakushindia
 Yeye MUNGU anasema ''Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.-Yeremia 33:6''

Ukiwa kwake huyu MUNGU wa uzima hakika umeshinda,
Yeye anasema Mwokozi anasema  '' Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. -Mathayo 11:28''

Wakuabudiwa ni yeye na huabudiwa katika roho na kweli
Yohana 4:24 '' MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.''

Na kwa msaada wake mwaka huu unaweza ukatenda makuu
Zaburi 60:12 '' Kwa msaada wa MUNGU tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.''

Kama umeokoka hakika uko upande sahihi hivyo songa mbele na Wokovu wa KRISTO.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU kwa maombi ya imani na utakatifu na hakika ushindi ni lazima.
 
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments