KUBARIKIWA ILI KUWABARIKI WENGINE

Na Mchungaji na Mwalimu Menirald Anthony Mtitu

Katika Mpango wa Mungu hakuna chochote katika Asili kinacho ishi kwaajili yake tu.Mfano mito hainywi maji yake yenyewe,bali yananywewa na viumbe vingine.Miti haili matunda yake yenyewe inayozalishwa ,yanaliwa na ndege na wanyama wengine ambao hata hawakuhusika nayo.Liangalie jua, halitengenezi na halitoi joto kwaajili yake lenyewe,hivyo hivyo kwa Mwezi wengine wanafurahia mbalamwezi yake.
Kuishi kwaajili yaw engine ni sheria ya asili.Ishi kwaajili ya wengine,fanyika Baraka kwa wengine na Mungu atakubariki kwa wingi.Sheria nne za Baraka .
MWANZO 12 :1-2

BWANA akawa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. “Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka. Nitawabariki wale wanaokubariki, yeyote akulaaniye nitamlaani na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.”

  1. Baraka zetu lazima zitiririke kwa Wengine:

Biblia inatufundisha kwamba tumebarikiwa  sio ili tu tujisikie vizuri  tu ,sio tu ili tujisike furaha na raha,lakini ili kwamba tuwabariki wengine. Mungu alimwambia Abramu  katika Mwanzo 12:2  “Nitakubariki… Nawe utakuwa baraka”. Hii ni sheria ya kwanza ya Baraka:Lazima itiririke kwenda nje.
Swali ni kwa namna gani unaweza kubariki wengine? Jibu rahisi ni kwa kuwahudumia mahitaji yao yawe ya kimwili au msaada wa kihisia,Masada wa kifedha,hata ushauri wa kivitendo na zaidi sana msaada wa kiroho. Tunaweza kufanya hivyo  kwa kuwapa wengine rehema .kuwaonyesha upendo,kuwajali kuwathamini.
Wafilipi 2:4
 “Kila mmoja wenu asiangalie mambo yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.”
Kumbuka Mungu anabariki watu ili wawe Baraka kwa wengine.Tuna fanyika Baraka na kuwabariki wengine kwa kuwaonyesha na kuwasaida kumtafuta na kumjua Mungu.Kila Aliye mwamini wa Kristo anapawa kuwa aweze sio tu kuwaleta watu wengine kanisa.lakini pia aweze kuwaeleza kwa uwazi habari njema za Injili wale ambao bado hawamjua Mungu ili waweze kumjua Yeye kupitia Yesu Kristo.
I PETRO 3:15
bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Sikuzote mwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima.”
Kuna methali ya Kiafrika  inayosema
“ Kuna kosa moja tu kubwa zaidi ya muuaji wa jangwani, na hilo ni kujua wapi maji yapo na kutokusema”
Mungu ametuongoza kwa Kristo,maji yaliyo hai,ametubariki na wokovu wake na ameahidi kutubariki  sisi kwa wingi huko mbeleni.Hivyo tunawajibu wa kuwafikia wengi kwa Baraka  hii ya kiroho.
  1. Tunapo wabariki wengine,Mungu anajali mahitaji yetu.
Mungu ameahidi kwamba kama tutakaza katika kuwabariki wengine,Yeye atajali na kuhusika na mahitaji yetu. Hakuna ambacho Mungu hawezi kufanya kwa mtu  ambaye kwa kumaanisha amejitoa kuwasaidia wengine.
LUKA 18.28-30
Ndipo Petro akasema, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” Yesu akajibu, “Amin nawaambia, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.’’
Tunapo jali kuhusu kuwasaidia watu wengine,Mungu anachukua jukumu la kuwajibika na matatizo yako.Na hiyo ni Baraka halisi,kwani Yeye anaweza zaidi kushughulikia matatizo yako kuliko wewe.
  1. Baraka zetu kwa wengine zitaturudi tena sisi.
Kadiri unavyo wabariki watu wengine na unavyo wasaidia wengine zaidi,ndivyo Mungu naye anavyo kubariki maisha yako zaidi. Hii ni sheria ya tatu ya Baraka
LUKA 6:38
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
Huwezi kumshinda na kumpita Mungu,kadiri unavyo jaribu na kujitajihidi kuwabariki watu wengine wanakuzunguka kwa namana mbalimbali ndivyo na Mungu  naye anavyozidi kukubariki zaidi.Ni kama mchezo wa kubarikiana,unabariki,nawewe unabarikiwa hivyo hivyo.
2 WAKORINTHO 9:8-13
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. Kama ilivyoandikwa: “Ametawanya huwapa maskini, haki yake yadumu milele.’’ Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, ambako kwa kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

  1. Kadiri tunavyo barikiwa zaidi na Mungu,Ndivyo Anavyo tutarajia kuwasaidia wengine zaidi.
Yesu amefundisha jambo hili  katika   
Luka 12:48
Lakini ye yote ambaye hakujua laini akafanya yale yastahilio kupigwa atapigwa kidogo.Ye yote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi na ye yote aliyekabidhiwa vingi kwake vitatakiwa vingi.  
Tumebarikiwa na tunabarikiwa kubariki wengine.Ni  muhimu kujiuliza kwa kuangalia Baraka zilizoko katika maisha yangu zinazonizunguka Mungu ananitarajia nifanye nini? Kuna mahitaji gani yanayonizunguka ambayo ninaweza kutumia kipawa au kipajichangu na kufanyika Baraka kwa wengine?
By  Rev. Meinrald A. Mtitu.
 Mkufunzi wa chuo cha Biblia cha ICM Seminary  Mapinga-Bagamoyo 
Pia ni Mchungaji  kanisa la International Pentecostal Holiness

Comments