KUMILIKI KWA MTEULE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Shalom mtu wa MUNGU kokote uliko.
Nakusalimu katika jina kuu la YESU KRISTO Mfalme wa uzima.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.


Kumb 1:8 "Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao."

Kwa watu wa MUNGU kumiliki kupo kama tukiamua kumiliki.
Kumiliki katika ulimwengu wa roho kupo na ni jukumu letu kumiliki.
Katika maisha yako ya Ukristo hakikisha unamtii MUNGU na omba kwake ili upate kumiliki.
MUNGU akikupa kumiliki huo ndio ushindi wako mkuu.
Inawezekana kabisa kumiliki afya njema ya bila kusumbuliwa na magonjwa.
Inawezekana kabisa kumiliki ushindi dhidi ya kila nguvu za Giza.
Waliomiliki kwenye ulimwengu wa roho wala wahateswi na uchawi au mapepo.
Tunatakiwa sana kumiliki maana MUNGU Muumbaji ndio MUNGU wetu na sisi tu wateule wake Watakatifu tunaoishi katika kusudi lake.


Mteule wa KRISTO hakikisha una mamlaka ya kumiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho.

Jambo la kujua ni hili; Kumiliki katika taifa lolote ni lazima kwanza uwe na uraia wa taifa hilo.
Mfano huwezi kuwa waziri katika taifa ambalo wewe sio raia halali wa nchi ile, huwezi kuimiliki nafsi hiyo ya uwaziri hadi uwe raia wa nchi ile tena ukiwa na sifa za kuwa katika nafasi hiyo.
Hivyo hivyo hata kumiliki kiroho ni lazima kwanza uwe raia wa mbinguni ndipo utamiliki.


Kuwa raia wa mbinguni ni kumpokea YESU kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu katika yeye.
Kwa tuliookoka Biblia inasema kwamba wenyeji wetu ni mbinguni, yaani kwetu ni mbinguni au sisi ni raia halali wa mbinguni.


Wafilipi 3:20-21 "Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana YESU KRISTO; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake."


Ndugu tamani kumiliki baraka za MUNGU ukiwa tu na uraia wa mbinguni.
Lakini pia unatakiwa kuwa Mkristo asiyemuoga Bali aliye thabiti katika imani yake iliyo ya thamani sana.
Wanaomiliki ni mashujaa.
Wanaomiliki ni waombaji na wanaishi maisha matakatifu katika YESU KRISTO.


Wanaomiliki ni wale wenye imani kubwa kwa MUNGU.
Wanaomiliki ni wale wanaopambana kwenye ulimwengu wa roho na kushinda kwa kutumia jina la YESU KRISTO na damu ya YESU KRISTO.
Wanaoshinda ni wale walio na nguvu za ROHO MTAKATIFU na wanamtii yeye.
Wanaomiliki ni wale wanaotumia neno la KRISTO na jina la YESU KRISTO katika maombi yao.
Wanaomiliki ni wale mashujaa wanaoendelea mbele na Wokovu wa KRISTO bila kurudi nyuma wala kusitasita.
Ndugu yangu ni wakati wako wa kumiliki.
Miliki afya, uchumba, ndoa, biashara, Kufaulu mitihani.
Miliki hitaji lako kwa maombi ya imani katika jina la YESU.
YESU KRISTO ni mshindi na atakushindia hakika.
Yeye akikuweka huru hakika utakuwa huru kweli kweli.


Yohana 8:36 "Basi Mwana( YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. "


Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments