KUNA MAMBO/VITU LAZIMA VIFE AU UVIUE NDIPO UMUONE BWANA 2017! Sehemu ya Pili


Na Mtumishi Nickson Mabena
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu!
Karibu tuendelee na Mfululizo wa Pili wa Somo hili ambalo limekuwa baraka kwa wengi,
Somo hili linamtaka Mtu anayetaka kuwajibika katika Mungu, hasa yule mwenye kiu ya kumuona Mungu kwa viwango vingine!.
Kuna watu wamekuwa wanahitaji Kumuona Mungu kwenye Maisha yao, lakini ukiwaangalia kuna vitu wamevishikilia au wameshikiliwa na vitu, wakati mwingine wameshikiliwa na watu!.
Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu hao wanaomuhitaji Mungu basi somo hili linakuhusu!.
Roho Mtakatifu yupo kukusaidia pale utakapochukua atua ya kufanya maamuzi mapya!..
Leo, naanza na maandiko yafuatayo;
"Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho. *Neno la Bwana lakazidi na kuenea.*" MDO 12:21-24
Soma vizuri hayo maandiko, mimi nataka ule mstari wa 24 unaosomeka "NENO LA BWANA LIKAZIDI NA KUENEA"
Herode alipokuwa ameketi kwenye kiti chake cha Enzi, akauchukua Utukufu wa Mungu, na watu wakamuona kama Mungu-Mtu flani hivi!.
Malaika akaja, akampiga, akaliwa na Chango akatokwa na roho yaani AKAFA!
Alaipokufa nini kilitokea?, Biblia inasema NENO LA BWANA LIKAZIDI NA KUENEA!.
Kwa hiyo HERODE ALIKUWA KIKWAZO KWA NENO LA MUNGU KUKUA/KUZIDI NA KUENEA ndio maana ilibidi kwanza AULIWE ILI NENO LIZIDI NA KUENEA!.
Sikiliza, Biblia haijasema KANISA LIKAZIDI NA KUENEA, bali NENO LA BWANA LIKAZIDI NA KUENEA!
Kwa hiyo, Kama unataka kwenye Maisha yako NENO LA BWANA LIZIDI KWAKO, NA KUENEA KWA WINGI unatakiwa uingie gharama ya KUMTAFUTA HERODE WAKO NA KUMUUA!
Umenisikia nilichokisema?
Nimekwambia hivi, 'HERODE' wako LAZIMA AFE NDIO NENO LA MUNGU LITAZIDI KWAKO NA KUENEA.
Nakupa kazi moja, Mtafute HERODE wako na umfahamu kwamba huyu ndiye KIKWAZO!
Herode kawaida yake ni KUZIBA MASIKIO YAKO ILI NENO LA MUNGU LIKWAME KWAKO!
Kwenye somo la kwanza, nilikupa mfano wa kitu/vitu vya kuviua NDIPO UMUONE BWANA!.
Nataka nikupe mfano mwingine, nikuonyeshe HERODE WA WENGI!.
Nasoma, 1Korintho 15:33,
*"Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema"*
Nataka tusome andiko hilo kwenye biblia zingine kama mbili hivi, ili unielewe ninachomaanisha!.

Tafsiri ya Ulimwengu mpya inasema hivi;
*"Msiongozwe vibaya. MASHIRIKA MABAYA huharibu mazoea yenye kufaa"*

Biblia yangu REVISED STANDARD VERSION inasema hivi, *"Do not be deceived: BAD COMPANY ruins(corrupt) good morals*"
Ok, twende pamoja sasa!
Kuna maneno haya
*1.MAZUNGUMZO MABAYA (evil communications)*
*2.MASHIRIKA MABAYA,*
*3.BAD COMPANY*
[Namba 2 na 3 zinaweza zikawa na maana sawa!. ]
Umeyaona hayo maneno? Ni muhimu sana kwa WAKRISTO!
Wakristo wengi kikwazo chao katika maisha yao ya kiroho ni MASHIRIKA MABAYA,
Marafiki zako wengi ni waovu tu, mchumba wako muovu muovu tu, mazungumzo yenu ni maovu maovu maovu tu, Utafanikiwaje katika MUNGU?,
Usije kujidanganya eti UTAMBADILISHA HERODE,
Sikiliza ni rahisi sana DELILA KUMUANGUSHA SAMSONI kuliko SAMSONI KUMBADILISHA DELILA!
(Maamuzi ni yako)

Angalia, Chunguza aina ya Marafiki unaoshirikiana nao kwa karibu, pia angapia aina ya mazungumzo mliyonayo, na tena angalia aina ya mawasiliano mlionayo,
Ukija kugundua ni Mazungumzo mabaya, Mashirika Mabaya, Mawasiano mabaya basi bila shaka NDIVYO VINAVYOHARIBU VITU VYA KIMUNGU KWAKO,
Ndivyo, VIKWAZO VYAKO KWENYE MAISHA YAKO YA KOROHO,

Kama ni hivyo usitafute ushauri mwingine, bali UA HAYO MASHIRIKA, VUNJA NA KUHARIBU HAYO MAWASILIANO MABAYA, UA HUO URAFIKI NDIO KIKWAZO KWAKO!
Mwingine anaanza kuwaza, SASA ATANIELEWAJE?, angalia USIWAZE ATAKUELEWAJE MTU, Jiulize ANAKUELEWAJE MUNGU????.
Kumbuka, HERODE ALIPOKUFA NENO LA BWANA LIKAKUA NA KUENEA!
Hakika Neno la Mungu litaenea kwako, hakika neno litakua kwako FANYA MAAMUZI!.
Naomba nisiendelee sana, kwenye somo lijalo nitaingia ndani kidogo, Endelea kuyatafakari hayo!.
Nikupe tangazo la kitabu changu, ambacho kimekuwa Baraka kwa wengi sana, nisingetamani ukikose!
Kitabu kinaitwa MUNGU ANAYO NJIA KWA AJILI YAKO,
Kinapatikana kwa Tsh.5,000/= tu!.

Wasiliana nami ukipate kikusaidie!.

Mimi ni Kijana wako,
Naitwa,
Mwl. Nick
0712265856

(WhatsApp#)

Comments