![]() |
Na Mtumishi Dr. Frank P. Seth |
MWA. 18:1-15 SUV
Fikiri nyumbani mwako wanakuja wageni watatu, mume anawaita jina moja "Bwana" kwa sababu haoni watatu ila anamwona Bwana! Ghafla! Anawasujudia hata nchi...na kuanza kukimbia mbio huku na kule kuwahudumia. Ibrahim alifanya mwenyewe uchaguzi wa aina ya chakula na akaamuru waandaliwe hicho chakula halafu akawapa yeye...hiki ni kiwango kikubwa cha heshima!
Angalia mkewe. Muda wote mama anaona watu watatu na sio Bwana! Wala hakujua kwamba ni wakati wa kupokea muujiza wake. Anacheka moyoni mwake kwa sababu "hawa watu" wanazungumza mambo yasiyowezekana....Sara anajua siku zake zimekoka....hawa wageni hawajui chochote....maana Sara aliona watu sio Bwana! Hata hao wageni walipomjibu kama Bwana, bado hakuelewa, akajikuta anabishana na Mungu...Bwana anaona Sara amecheka, japo alicheka moyoni ...kwa sababu Sara hakucheka kwa sauti...Sara alijua hakuna "mtu" ameona hiyo...akabisha...Muda wote huu hakujau aliyekuja kwake ni Bwana!
Kwanini Sara hakujiuliza sababu za mumewe kuwa na mapokezi yasiyo ya kawaida? Gahfla mzee Ibrahim anakimbia hovyo, anawasujudia, anakuwa na adabu isiyo ya kawaida. Ibrahim Anajiita kwao "mtumwa"! Je! Macho ya Sara yaliluwa yanaona nini?

Mara nyingi kwenye maisha yetu tumedhani kwamba mambo yanayotuathiri ni yale ambayo watu wanajua! Kwa hiyo ukiweza kufuta mdomo vizuri unajifariji uko salama! Sara akabisha...swali ni Je! Unaona sawa sawa?
Frank P. Seth
Comments