MWAKA WA KUMTEGEMEA MUNGU NA KUSHINDA.

Na Mtu wa MUNGU, Mwinjilisti Peter Mabula.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
YESU KRISTO ni Mshindi, na ameshinda tena.
Nakutakia mwaka mzima wa ushindi na baraka za MUNGU Baba.
Nakutakia mwaka wa ushindi ndugu yangu na rafiki yangu.
Neno kuu la mwaka huu nililopewa Mimi ni Yeremia 10:6 ambapo Biblia inasema "Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee BWANA; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza. "
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU Baba.
Zingatia itakusaidia sana.


Kwanini umeingia mwaka huu mpya?
Je mwaka huu umebeba nini kwako?
"Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. - Mhubiri 3:1.

Kumbe kwa kila jambo kuna majira yake yaani kwa maana nyingine ni kwamba kila majira Fulani yamebeba mambo Fulani.
Je majira yako yanayoanza January mwaka huu  unatamani yabebe nini?
Wakati mwingine funga na kuomba ukiombea majira mapya yanayoanza january yabebe baraka kwako maana kwa kila jambo kuna majira yake.

Jiombee mwaka huu  uwe ni mwaka wa BWANA uliokubaliwa.
Omba ili uwe mwaka wa MUNGU kukubariki.
Inawezekana umejaribu kutafuta kazi miaka iliyopita ila hukufanikiwa, mwambie Bwana YESU kwamba majira haya  yaliyoanza january hii  basi asikupite.
Inawezekana umejaribu kutafuta mchumba lakini wala hukufanikiwa, mwambie MUNGU kwamba majira haya ya mwaka huu  ukafunge ndoa takatifu.
Ngoja nikupe ushuhuda mfupi.
Nilikuwa nimepanga kwamba mwaka 2010 nifunge ndoa lakini haikuwezekana. 2011 ndio hata dalili tu za kufunga ndoa hazikuwepo.
2013 ulikuwa mwaka mgumu lakini majira ya BWANA yaliyokubalika yalipofika nilifunga ndoa Sept 2014.

Hata wewe inawezekana majira yako ni mwaka huu. 
Ishi maisha matakatifu na omba maombi Mara kwa Mara maana inawezekana majira yako yamefika.
MUNGU Baba akakuonekanie mwaka huu wote.


Isaya 49:8 "BWANA asema hivi, wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa."

MUNGU akubariki mwaka huu  katika jina la YESU KRISTO.
Uwe mwaka wa ushindi wako na baraka zako
Ndugu Mtegemee MUNGU hakika utashinda.
Kila mwaka umebeba vitu vyake hivyo msihi MUNGU kwamba mwaka huu ukabebee baraka zao.

"MUNGU akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; - Mwanzo 1:14"

Kumbe kuna usiku na mchana, kuna majira na nyakati.
Kila siku katika maisha zimebeba mambo yake.
Kila majira kuna vitu yamebeba.
Kila miaka kuna vitu imebeba.

Nakuombea kwa MUNGU kwamba majira haya ya mwaka huu kwako yakabebe ushindi, kufunga ndoa, kufungua biashara nzuri, kupata kazi n.k.
Kama wachawi walikushinda katika majira ya mwaka ulipita basi kwa jina la YESU KRISTO mwaka huu wakapondwe na kuabika wao.
Ndugu jipange tu vizuri kwa YESU mwaka huu na wachawi hao wataharibiwa wao, watapondwa wao na wataangamizwa wao.
Kazi yako ni kuishi maisha matakatifu katika YESU KRISTO na kuomba kwa imani maana ushindi kwako ni lazima.


Zaburi 30:11 " Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, Ukanivika furaha"
Bwana YESU ageuze matanga yako kwa kukupa furaha juu mwaka 2017.
Misiba iondoke na mafanikio yaje kwako, kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Maombolezo kwako yaondoke kwa MUNGU kukupa furaha kuu.
Huu mwaka mpya ukawe mwaka wa ushindi wako.


" BWANA atawapa watu wake nguvu, BWANA atawabarikia watu wake kwa amani.- Zaburi 29:11"

MUNGU Baba akakutendee hayo mwaka huu, akakubariki na kukupa amani yake.
kwako mwaka huu uwe wa ushindi.
Mtegemee MUNGU Baba na hakika utashinda maana huu ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.

Ukabidhi kwa MUNGU mwaka wako na anza kuuishi mwaka kwa ushindi huku ukidumu sana katika utakatifu na maombi na kuhdhuria ibada kanisani

Wakati mwingine huwa kuna miaka ya tabu na miaka ya baraka.
Wewe ndiye unaweza kuamua mwaka huu kwako  uwe mwaka wa baraka au wa tabu.
Kama kuna mwaka ulianza shule basi pia kuna mwaka wa kumaliza shule.
Kama kuna mwaka wa mitihani tambua pia kwamba kuna mwaka wa furaha, vifijo na nderemo.
Kama kuna miaka ulikuwa single basi tambua kwamba kuna mwaka utafunga ndoa takatifu kanisani, kutegemea na utii wako kwa MUNGU.

Nakuombea mwaka huu uwe mwaka wako wa kufunga ndoa takatifu kanisani.
Umeshuhudia shela za wengine miaka mingi, MUNGU akupe kuna shela yako siku ukifunga ndoa mwaka huu  kwa jina la YESU KRISTO.

Unaweza ukalia ukikumbuka jinsi ulivyochangia harusi za wengine katika nyakati zao.
MUNGU Baba akupe majira yako mwaka huu na ukafanikiwe kufunga ndoa takatifu kwa jina la YESU.
Hakikisha tu unaishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO.
Usikubali uzinzi na uasherati uifute baraka yako ya mwaka huu.
Usikubali dhambi ziifute baraka yako ya mwaka huu.
Mtii KRISTO YESU na neno lake hakika utafanikiwa.

Nakushauri pia jambo hili; 
Naomba nikushauri mambo haya yafuatayo;
=Usikubali kuingia mpya  ukiwa huna Biblia yako binafsi na sio ya kuazima.
usikubali kwenda mwaka huu bila Biblia.
pia nakuomba katika mwaka mpya mzima huu hakikisha unaweka ratiba ya kusoma Biblia na kuielewa. Weka hata ratiba ya kuisoma Biblia nzima ili kuongeza ufahamu wa kiroho na hiyo itakusaidia kushinda.
Usiridhike na Biblia za kwenye simu tu Bali nunua Biblia.


=Wakati mwingine ni kwamba; Yale uliyoyapanda mwaka uliopita  ndio hayo utavuna mwaka huu.
Hatari ni kama umepanda mabaya mwaka ulipita basi unaweza kujikuta unavuna mabaya mwaka huu.
 Toba na utakatifu unahitajika sana kwako. 
 Umepanda nini mwaka uliopita?

 =Inawezekana kabisa imefika pahali ukajikataa na kujichukia, lakini mwaka wa MUNGU uliokubalika umekuja.
Nakuombea kwa MUNGU kwamba mwaka huu uwe mwaka wa baraka yako katika jina la YESU.

Katika mwaka fulani zamani kipindi cha Yusufu akiwa Misri ilianza njaa iliyodumu miaka 7, lakini Neema ya MUNGU ilikuwepo maana kulikuwa kumepita miaka 7 ya Neema na shibe na amani na utajiri mkuu, hiyo
 Mwanzo 41:29-31.'' Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana.''

Katika miaka ya baraka za MUNGU, Yusufu alikusanya utajiri wa Mali na vyakula vya kuwatosha taifa zima hata na majirani kwa miaka 7 iliyofuata.
Kupitia habari za Yusufu tunajifunza kwamba kumbe wakati mwingine huwa kuna miaka ya njaa na kuna miaka ya baraka.

Kama miaka ya maumivu imepita sasa MUNGU Baba akupe mwaka wa baraka yako.
MUNGU akupe mwaka wa furaha na ushindi.
Kama vilevile mwaka wa njaa kwako ulivyoanza ndivyo hivyo hivyo mwaka wa baraka nyingi uanze kwako katika jina la YESU KRISTO aliye hai milele.
Mtii tu MUNGU na ishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO YESU Mfalme wa uzima.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments