NAMNA WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.


Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Watu wengi sana huuliza sana kuhusu jinsi wanafunzi wa YESU wa wakati wa Biblia walivyokufa. Ngoja nikujuze.


=Mtume peke ambaye kifo chake kimeandikwa katika Biblia ni Yakobo (Matendo Ya Mitume 12:2). Mfalme Herode alimweka Yakobo “afe kwa kisu,” kuna uwezekano kuwa alikatwa kichwa. Hali ya kifo cha mitume wengine zimehusiana kutokana na historia ya Kanisa, kwa hivyo tusiweke uzito mwingi kwa tukio lo lote.
Katika historia ya Kanisa ya imekubalika kuhusiana na kifo cha mitume ni kuwa;


=Mtume Petro alisulubiwa kichwa chake kikiangalia chini kwa msalaba wa umbo la X huko Rumi kwa kutimiza unabii wa YESU (Yohana 21:18).
Ifuatayo ni historia inazojulikana sana kuhusu kifo cha Mitume wengine kulingana na historia ya kabisa;

=Mtume Mathayo aliteseka kwa ajili ya injili huko Ethiopia, aliuawa na donda la kisu. 

=Mtume Yohana alikumbana na mateso juu ya injili wakati alichomwa katika bakuli kubwa la mafuta yachomayo wakati wa uvumi wa mateso huko Rumi. Ingawa aliokolewa kimuujiza kutoka kwa kifo. Yohana alihukumiwa mateso katika kisiwa cha Patmo. Alikiandika kitabu chake cha unabii cha Ufunuo huko Patmo.
Mtume Yohana baadaye alifunguliwa na akarudishwa nchi hii leo yaitwa Uturuki. Alikufa akiwa mzee, Ni Mtume pekee aliyekufa kifo cha kawaida.


=Yakobo, nduguye YESU (si mtume halisi), alikuwa kiongozi wa Kanisa huko Yerusalemu. Alitupwa kutoka mnara wa juu sana wa Kusini-Mashariki wa Hekalu (takribani futi mia moja kwenda chini) wakati alikataa kumkana KRISTO. Wakati waligundua kwamba ameponea mwanguko huo, maadui wake walimpiga Yakobo kwa rungu hadi akafa. Hii imetuhumiwa kuwa mnara ambao Shetani alikuwa amempeleka YESU wakati wa majaribu baada ya kubatizwa.

=Bartholomayo, ambaye anaitwa Nathanaeli, alikuwa mmisionari huko Asia. Alishuhudia sehemu ambayo sasa inaitwa Uturuki na akauawa kwa sababu ya kuhubiri injili huko Armenia, kwa kupigwa hadi kifo na kijiti. 

=Andrea alisulubiwa kwa msalaba wa umbo la X huko Ugiriki. Baada ya kuchapwa kwa fimbo mara nyingi na walinzi saba, waliufunga mwili wake kwa msalaba kurefusha machungu yake. Wafuasi wake wakaripoti kuwa wakati aliongozwa kuelekea kwenye msalaba, Andrea akawapungia mkono wafuasi wake kwa maneno yafuatayo, “kwa muda mrefu nimengoja na kutamani saa kama hii ya furaha. Msalaba umekwisha takaswa kwa mwili wa KRISTO ulioangikwa juu yake.”
Aliendelea kuwahubiria watesi wake kwa siku mbili hadi wakati alikufa.


= Mtume Tomaso alichomelewa mkuki huko India wakati wa mojawapo ya safari zake kama mmisionari alipokuwa akilianzisha Kanisa huko. 

=Matia, mtume aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote, alipigwa mawe na kichwa chake kukatwa. 

=Mtume Pauo aliteswa na baadaye kichwa chake kikakatwa na mfalme mwovu Nero huko Rumi katika mwaka wa A.D 67. 

Si muhimu sana ni namna gani mitume walikufa. Cha maana ni kuwa walikuwa tayari kufa kwa sababu ya Imani yao.
Ikiwa YESU hakuwa amefufuka, mitume wangejua hivyo. Watu hawatakufa kwa kitu wanakijua kuwa uongo. Hoja kwamba mitume wote walikuwa tayari kufa kifo kibaya, walikataa kuikana Imani katika KRISTO ni uthibitisho mkubwa kuwa kwa kweli walishuhudia ufufuo wa YESU KRISTO.
MUNGU akubariki.

Comments