SAFARI YA MAFANIKIO YENYE UPINZANI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Shalom wateule wa KRISTO.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Safari yeyote yenye mafanikio lazima kuwe na upinzani wakati mwingine.
Ukimuona mtu amefanikiwa ni kwasababu japokuwa alipitia upinzani lakini alivumilia.
2 Wafalme 2:1-15 '' Ikawa, hapo BWANA alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha. Eliya akamwambia Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Betheli.  Elisha akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni.  Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana BWANA amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko. Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni. Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili. Basi watu hamsini wa wale wana wa manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama karibu na Yordani. Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu. Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu. Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati. Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani. Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi BWANA, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.''

Eliya alikuwa nabii na Elisha alitaka kufanikiwa kupitia Eliya.
Katika maandiko hapo juu tunaona uvumulivu wa Elisha hadi akapata kitu cha ziada cha kumfanya afanye kazi yake vyema.
Walikuwepo wana wa manabii yaani wanafunzi wanaojifunza huduma ya unabii na hao waliona kitu rohoni kuhusu kuondoka kwa Eliya.
Ukiwa na macho ya rohoni utaona rohoni, wana wa manabii waliona rohoni kwamba Eliya ataondoka hivyo walijaribu kumweleza Elisha ili asiendelee kuambatana na Eliya.
Elisha alitambua kwamba kuna safari ndefu mbele yake ya utumishi na japokuwa muda mwingi ulikuwa umepita akiwa amepakwa mafuta kuwa nabii, lakini hakuona matendo ya MUNGU kupitia huduma hiyo na alihitaji kitu cha ziada kutoka kwa Eliya.
Safari yenye mafanikio ni lazima ikutane na upinzani.
Koti la Eliya lilikuwa muhimu sana kwa Elisha.
Kuna Vitu vya Ki-MUNGU ni muhimu sana kuving'ang'ania ili ufanikiwe katika safari yako.
Elisha kabla hajalipata lile vazi la Eliya hakukubali kwamwacha Eliya aende.
Elisha ilibidi tu avumilie ili asipoteze muujiza wake.
Inawezekana wewe wala huhitaji vazi lakini unahitaji Neno la ufunuo kutoka kwa MUNGU kupitia watumishi wake.
MUNGU anapokuwa ameandaa mujiza wako wakati mwingine maadui zako hujaribu kupeperusha muujiza wako.
Wana wa manabii walijaribu kumwambia Elisha  ili kumkatisha tamaa lakini Elisha aliwajibu kwamba ''Nyamazeni, mimi najua''
Elisha angemruhusu Eliya aende angebaki hivyo hivyo.
Kumbuka 1 Wafalme 19:15-16 Biblia inasema '' BWANA  akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.''
 Na baada ya Elisha kutiwa mafuta ulipita muda mwingi lakini hakufanya lolote kulingana na huduma yake.
Kuna kitu cha muhimu sana alikihitaji ndipo afanikiwe katika huduma yake.
Safari yenye mafanikio ni lazima iwe na upinzani.
Mteule wa KRISTO anayemjua MUNGU wake, huukemea upinzani huku akisonga mbele na kumfuata MUNGU wake katika mpango wake juu yake.
Eliya aliambiwa na MUNGU ampake mafuta Elisha ili awe nabii mahali pake kisha mungu hakusema kitu zaidi kwamba ni nini kinafuata. Elisha alijua kwamba kupakwa mafuta tu hakutoshi bali alitamani kupata kitu cha ziada ndani ya Eliya.
Elisha aling'ang'ania.
Kuna vitu ili uvipate ni lazima unganganie.
Kuna vitu ili uvipate ni lazima uvumilie sana.
Kung'ang'ania kwa Elisha ndiko kulikosababisha apate vazi la Eliya.
Kikwazo cha kwanza cha Elisha kilikuwa ni Betheli.
Kikwazo cha kukaa Betheli Elisha alikivunja na kuendelea kuifuata baraka yake.
Waswahili wanasema wengi wape lakini Elisha aliwaambia wana wa manabii walio wengi kwamba ''Nyamazeni, mimi najua''
Mtu wa MUNGU huwa hafanyii kazi maneno ya watu hata kama ni wengi sana, bali hufanyia kazi Neno la MUNGU.
Kikwazo cha pili kilikuwa Yeriko na kikwazo cha mwisho kilikwa Yordani.
Kikwazo cha Yordani kilivunjika na Elisha akapata baraka yake.
Alipomaliza kuvumilia Elisha alisikia sauti ikimwambia aombe lolote ili atendewe, lakini ni hadi alipovumilia hadi mwisho.
Sina uhakika kama safari za ghafla alizozipanga Eliya ili kumkwepa Elisha zilikuwa zinatoka kwa MUNGU.
MUNGU aangalie uvumilivu wako.
MUNGU aangalie juhudi yako.
Hata kama wasio upande wako ni wengi kiasi gani, wewe endelea kumtegemea MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi wetu.

Nehemia  4:1-6 ''Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe. Sikia, Ee MUNGU wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho; wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga. Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi. ''

 Katika safari yenye mafanikio huwa hawakosekani wapinzani.
Hawakukosekana wapinzani katika safari ya Nehemia kwenda kuujenga ukuta wa Yerusalemu.
Wakukupinga huwa hawakosekani hata wakati MUNGU amekufungulia mlango.
Akina Sanbalati na Tobia wako hata katika maisha yako.
Akina sanbalati na Tobia ndio wapinzani wako.
Hao siku zote hutaka wewe usifikie katika malengo yako, hutaka usifike katika lengo jema kutoka kwa MUNGU.
Wenye maneno ya kukatisha tamaa huwa hawakosekani.
Wapinzani wako hawakosagi neno la kusema.
Nehemia alimuomba MUNGU na alishinda.
Safari ya Nehemia ilikuwa ni safari ya mafanikio yenye upinzani lakini alishinda.
Safari ya Elisha ilikuwa ni safari ya mafanikio yenye upinzani lakini alishinda kwa kuvumilia.
Biblia inasema kwamba wakati mwingine akina Nehemia walikuwa wanajenga ukuta  huku wameshika silaha.
Ndugu yangu nakuomba fanya kazi ya MUNGU huku umeshika silaha.
Maombi ni silaha hivyo fanya kazi yako huku umeshika silaha.
Fanya jukumu lako jema huku ukiomba, maombi ni silaha yako kuu sana.
Ukisimama katika kusudi la MUNGU hakika MUNGU anaweza hata kukuandalia watu wa kukusemea.
Musa aliandaliwa Haruni kwa ajili ya kumsemea kwa farao ili afanikiwe katika safari yake.
MUNGU anaweza hata kukuandalia watu wa kukusemea.
Utaona watu wanabishana wao ili ufanikiwe wewe.
Kitu cha kwanza tulichokiona kwa Elisha ni uvumilivu na kwa njia hiyo Elisha alipata baraka za kiutumishi..
Baada tu ya Elisha kulipata vazi la Eliya miujiza mingi ilianza kuambatana na yeye.
Na ukisoma Biblia wakati mwingine unaweza ukaona miujiza aliyoifanya Elisha katika utumishi wake ilikuwa mingi na mikubwa kuliko hata miujiza ys Eliya.
Hebu oba Biblia inachosema mara tu baada ya Elisha kulipata vazi.
2 Wafalme 2:19-25 ''Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena. Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa! Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la BWANA. Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao. Akatoka huko akaenda mlima wa Karmeli, na toka huko akarudi mpaka Samaria.''

Kuvumilia kwako huku ukiomba ndiko kutaleta ushindi wako.
Kuvumilia kwako huku ukiishi maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO ndiko kutaleta baraka yako.
Ukishafanikiwa ni hao hao waliokupinga ndio watakutambulisha kwamba wewe ni mbarikiwa.
Elisha alipochukua vazi la Eliya hao hao wana wa manabii  waliomshawishi mwanzo ndio hao waliomsujudia wakisema kwamba Hakika roho ya Eliya iko juu ya Elisha.
Baada tu ya kulipata vazi la Eliya, Elisha alilitumia vazi lile kuyapiga maji na maji yakapisha akapita Elisha na huo ndio ukawa muujiza wa kwanza katika huduma yake japokuwa alikuwa amepakwa mafuta muda mrefu nyuma.
Elisha alihitaji vazi la Eliya ndipo huduma yake ianze kufanya kazi.
Inawezekana wewe vazi lako unalotakiwa kuwa nalo ili huduma yako ichanue ni utakatifu.
Kuna wengine wanahitaji tu kuomba sana ndipo watafanikiwa.
Elisha alihitaji vazi  lakini wewe unahitaji Neno la kinabii kutoka kwa ROHO wa MUNGU ndipo ukilifanyia kazi utafanikiwa katika safari yako.
Unahitaji kumtolea MUNGU sadaka na zaka  na kutunza muujiza wako.
Unahitaji kuipeleka injili mbele.
Kipo kitu kutoka kwa Bwana YESU unakihitaji ndipo safari yako itafanikiwa sana.
Somo hili najua ni gumu kulielewa katika usahihi wake ule niliokusudia lakini ROHO MTAKATIFU atakujulisha na simama imara katika Bwana YESU utashinda.

 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+ 2 5 5 7 1 4 2 5 2 2 9 2

Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako bila kubadili chochote, ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments