UBAGUZI WA MATUMIZI YA NEMBO YA KIISLAMU YA HALAL.

Na Mwalimu wa Neno la MUNGU, Daniel Mwankemwa

Nembo ya Kiislamu ya Halal (حلالا) inaonekana kwenye bidhaa mbali mbali zinazozalishwa hapa Tanzania.

Nembo hiyo kwa sasa hutolewa na Taasisi za Kiislamu hapa nchini. Taasisi hizo ni Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Baraza Kuu na Taasisi zake. Taasisi hizo zinapotoa nembo hiyo kwa wazalishaji hutoza kiasi fulani cha kodi ambazo huenda kutunisha mfuko wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Suleiman Lolila, akiongelea kuhusu nembo hiyo, alisema, "kupitia uwepo wa nembo hii katika bidhaa itasaidia kuweka uhalali wa bidhaa na kuweza kuuza bidhaa zetu nchi za nje kama Malaysia lakini pia tutakuwa tumetekeleza ibada ya Waislamu kwa kula vyakula halali."

Nembo hiyo inapotolewa, haihusiani na ubora au thamani yoyote ya bidhaa hiyo, bali ni kuitambulisha bidhaa hiyo kwamba imeandaliwa kwa kufuata misingi ya Sharia ya Kiislamu.

  Ubaguzi ninaouongelea hapa ni kwamba nembo hiyo inaihusisha jamii moja tu ya kiimani, ambayo ni ya Kiislamu.

   Hoja inayojitokeza hapa ni kwamba, je, jamii zingine za kiimani zinaruhusiwa na mamlaka  ya nchi kutumia nembo zao katika biashara wanazozizalisha ili kukidhi hitaji lao la kiimani kama ilivyo kwa Waislamu?

  Kwa kuwa hili ni suala linalohusisha uchumi, uzoefu kwa hapa Tanzania umeonesha kwamba, kumekuwa na upendeleo mkubwa sana wa kibiashara kutoka mamlaka kuu kuipendelea zaidi dini ya Kiislamu kuliko dini zingine.

Maana yake jamii moja inalazimishwa kwa nguvu kufuata mfumo wa imani usio wao.

Kwa mfano, mpaka leo kuna mgogoro mkubwa kwa Wakristo wanaomiliki bucha za kuuzia nyama, ambao, wasingependa kuchinjiwa wanyama wao na Muislamu.

 Hili limeonekana zaidi hasa  kipindi ulipoibuka mgogoro wa uchinjaji wa wanyama. Kwamba, je, ni nani anayeruhusiwa kisheria kuchinja wanyama ambao nyama yao itatumiwa na jamii nzima?

 Mgogoro huo, mbali na kusababisha baadhi ya Wakristo kutishiwa maisha na kufungwa, ulisababisha kifo kwa Mchungaji Mathayo Kachila wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of Tanzania (P.A.G) Buseresere, mkoa wa Geita aliyechinjwa hadi kufa.

     Sharia ya Kiislamu pamoja na mambo mengine imekusudia kuwabana wasio Waislamu kwenye mambo mbali mbali.

Vitabu vya sharia za Kiislamu vinalielezea suala hilo. Moja ya kauli ya Mtume Mohammad s.a.w kama ilivyonukuliwa katika kitabu kilichoandikwa na Sheikh Abdubakar Jabir al- Jazair kiitwacho,  Minhaj il Muslim, juzuu ya 3, uk.22 kuhusu kuwabana Wakristo, inasema, “Msiwaanze Mayahudi na Manasara (Wakristo) kwa kuwasalimia, mkikutana na mmoja wao njiani mbaneni asipate nafasi pana ya kupata. “(Ameipokea Muslim).”

 Tena Mtume Mohammad (s.a.w) amenukuliwa  katika kitabu kiitwachoTafsiri ya Bulugh Al-Maram, uk.499 Hadithi na 1126 akisema: “Msianze kuwaamkia Mayahudi wala Manasara mtakapokutana na mmoja wao njiani msogezeni upande wenye dhiki.” Manaswara ndiyo Wakristo.

   Katika dini ya Kiislamu, kuna Jihad mbili; Jihad Saghir, yaani, Jihad ndogo, ambayo, hii huhusika na kueneza Uislamu kwa njia ya mapambano ya silaha na huisha tu pale vita vinapokoma. 
     
  Jihadi nyingine inaitwa Jihad Kabir, yaani, Jihadi Kubwa. Hii huhusisha harakati zisizo tumia silaha zikiwemo za kiuchumi, kisiasa au kijamii kama ndoa na uenezi wa maandiko n.k.                   
     
 Jihad Kabir, yaani, Jihadi Kubwa ndiyo  inayosababisha mateso ya kiuchumi (economic persecution) kwa wasio Waislamu. Jihad hii Kubwa ni ya milele haina kikomo

   Utekelezaji wa Jihad kubwa ndiyo chimbuko la shinikizo la matumizi ya nembo ya Kiislamu ya Halal kwenye bidhaa mbali mbali ili kuuendeleza Uislamu. Na shinikizo hili, halifanyiki kwenye nchi za Kiislamu tu, bali hufanyika pia hata kwenye nchi zisizo za Kiislamu, ambako, kuna Waislamu wanaharakati walioko kwenye vyombo vya maamuzi, na wafanyabiashara wanaosimamia utekelezwaji wa Jihadi hii.

Mgogoro huo wa uchinjaji wa wanyama ili kuipa nguvu nembo ya Halal, uliwahi kupelekwa na kujadiliwa na bunge letu la Jamhuri.

 Katika HANSARD ya Bunge: Mkutano wa Tano, Kikao cha Tano kilichoketi tarehe 6 Nov, 2006, swali la uchinjaji wa wanyama liliulizwa na Mh.Hafidh Ali Twahir, Mbunge wa Dimani, (CCM), Zanzibar, aliyeitaka Serikali itunge sheria ya uchinjaji wa wanyama kwa kufuata imani za kidini.

Katika ukurasa wa 55 wa HANSARD hiyo, Mh. Twahir alisema, “sasa wenzetu kwa sababu ya kuweka tofauti pale ambapo kunachinjwa nyama halali, basi unapokwenda katika ranchi yao ya kuchinjia  kile kisu kimeandikwa Bismillah na kule alikoelekea ndiko kunakokubalika.” 

Mh. Twahir alitaka wanyama wanapochinjwa wachinjwe kwa kuelekezwa Qibla, uelekeo ambao Waislamu huelekea wakati wa kufanya ibada zao, yaani Makka.

Aliyekuwa Waziri wa Mifugo wa kipindi hicho Mh. Anthony Diallo (MB) (CCM) alitoa msimamo wa Serikali kuhusiana na suala hilo la uchinjaji. Katika uk.88 wa HANSARD hiyo ya Bunge, Mh. Dialo alisema,  "Kwa hiyo, muuzaji nyama yeyote ni lazima atazingatia kitu ambacho ni desturi na mila na matakwa ya wanunuzi wa nyama hiyo. Kwa  hiyo, hatuhitaji kuweka kwenye sheria kwa sababu tunafahamu Serikali yetu haina dini na hatuwezi kuanza kuingiza vifungu vya kutamka mahitajio ya dini moja au dhehebu  moja ndani ya sheria tunakiuka Katiba ambayo inatukataza Serikali isijihusishe na uhuru wa dini ni wa kila mtu sio wa Serikali.”


Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza usawa wa watu wote mbele ya sheria na inakataza ubaguzi wa aina yoyote.

     13.-(1)  Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. 

     (2)  Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.       
 17
      (4)  Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.

       (5)  Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.

Katiba inakataza ubaguzi wowote ukiwemo ule wa kidini. Matumizi ya nembo ya Halal ya Kiislamu kwenye bidhaa zote zinazotumiwa na jamii yote, huku wasio Waislamu wakizuiliwa kutumia imani yao katika masuala ya kibiashara, ni ubaguzi na kinyume cha Katiba.

Baada ya miaka kadhaa chini ya nembo hiyo ya Halal, jamii isiyo ya Kiislamu itajikuta haimiliki uchumi wa aina yoyote na hivyo kukandamizwa na kupoteza imani yao.


Daniel Mwankemwa
dmwankemwa@gmail.com
Dar es Salaam,

Comments