UPENDO WA KWANZA

Na  Dk Frank P. Seth

“Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.” UFU.‬ ‭2:2-7‬ ‭SUV‬‬

Hebu mwangalie tena huyu ndugu, "Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka". Kwa vigezo vya AKILI kwa kweli yuko vizuri. Hafanyi dhambi na hakubaliani na watumishi waliokaa vibaya...yuko sahihi...anakosoa sana ....yuko sahaihi...anaona makosa na udhaifu wa wengine....yuko sahihi...tena yuko vizuri...anasema kweli....ila UPENDO WA KWANZA! Upendo wa kwanza!

Huyu naye anaitwa aliyeanguka...anatakiwa kutubu...sio kwa sababu ya uzinzi...la! Hasha, kwa sababu ameacha upendo wa kwanza! Bado anamtumikia Mungu, bado ana subira, bado ana matendo mema, huyu hafanyi dhambi...ila atubu kwa sababu ameacha upendo wake wa kwanza! Naona changamoto...
Nini maana ya upendo wa kwanza? Angalia hapa, “Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu" (UFU.‬ ‭2:5‬ ‭SUV‬‬). Kuna matendo fulani ulikua unafanya mwanzo ulipokuwa unampenda BWANA, sasa hufanyi au umepunguza sana. KUMBUKA! Kilichopungua ni UPENDO sio mazingira wala hali halisi. Unaweza kusingizia watu, kazi, shule, nk. Ila kwa kweli ni shida kwenye upendo. Upendo wa kwanza umepoa na hicho kitu kinamsumbua Mungu.
Frank p. Seth

Comments