KUKOSA KIBALI NA KUKATALIWA

Na Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Licha ya kwamba kanisani ni sehemu maalum kwaajili ya ibada, lakini pia ndiyo sehem pekee ya kutua mizigo yako inayokusumbua. Ndiyo maana Yesu anatoa mwaliko '' njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na mizigo nami nitawapumzisha '' Kinyume na matarajio hayo watu wanateswa na kuonewa na ibilisi japo wako kanisani :-
Zifuataizo ni sababu za kimaandiko. Biblia imeweka wazi na bayana. 

1. Madhabahu uliyopo. Uko uhusiano baina yako na madhabahu unayoitegemea. Ustawi wako wa kiroho unategemea uhalali wa madhabahu hiyo. 

~Kama madhabahu yako imetengenezwa katika misingi ya ki Mungu, lazima utakua na kibali. Kinyume na hapo, utajikuta uko kwenye adhabu ya Kiroho kwa maana BWANA amemwaga hasira yake juu ya madhabahu hiyo.

Somo la Kwanza :Ezekieli 22:30&31
"Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma (madhabahu), na kusimama mbele zangu....lakini sikuona mtu. Kwa sababu hiyo, nimemwaga ghadhabu yangu juu yao:nimewateketeza kwa hasira yangu...... asema BWANA MUNGU.

Ndugu mpendwa, nia ya Mungu si wewe kutaabika kwa magonjwa, ufugaji, madeni na ujinga. Unapaswa kutambua kuwa hapo ulipo si mahala pako, rudi kwenye njia sahihi. Ndiyo maana hata Mwana mpotevu alitafakari akaona bora arudi kwao, jipime mpendwa, jichunguze, pata maamuzi mapya. 

2 . Kaburi na kujiinua.
Katika dunia hii ya nyakati za mwisho, watu hujiinua sana. Wameingiwa na kiburi cha ibilisi. Wamemuasi Mungu, wamejipa utukufu wa Mungu. Lakini Bwana anamataka mtu huyu "mnyenyekevu, atetemekaye asikiapo Neno la Mungu" hivyo kwa viburi vyao, wamelaaniwa kama baba yao ibilisi.

Somo la pili. 2Nyakati 7:14.
"ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya :basi nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao"

Mpendwa, kama hujanyenyekea na kuomba, usitegemee kukutana na Mungu. Haijalishi wewe ni Askofu, mchungaji, muinjilist, Mzee wa kanisa au mshirika. Kama hauna unyenyekevu ndani yako, huwezi kukikaribia kiti cha neema ili upewe neema (Ebrania 4:14-16).Hivyo, unapswa kutambua kuwa kuna kuhani mkuu zaidi yako na mchungaji wako. Omba kwa kumaanisha huku ukiamini pasipo shaka yo yote (Yakobo1:6-8)
***Itaendelea ***
Mwl Sospeter SN
NEM Tanzania

Comments