UBATIZO WA MAJI NI ISHARA YA NJE INAYOONYESHA BADILIKO LA NDANI YA MTU.

Mchungaji Elly Botto akiomba kabla ya kuanza kubatiza.
Jumamosi ilikuwa ni siku ya ibada ya ubatizo katika Kanisa la P A G Kawe chini ya Mchungaji Kiongozi Elly Botto.
Ubatizo huo ulifanyika katika Bahari ya Hindi katika Eneo la Kawe.
Mchungaji Botto kabla ya kubatiza alifundisha umuhimu wa ubatizo.
Ubatizo wa maji ni jambo la muhimu kwa kila mteule wa MUNGU.
Ubatizo wa Maji ni ishara ya nje inayoonyesha badiliko la ndani kimatendo, kimtazamo na kimaisha ya kiroho katika Wokovu wa YESU KRISTO..
Yohana 3:5-6 '' YESU akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa MUNGU.Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa ROHO ni roho.''

Waliobatizwa kutoka P A G Kawe walikuwa wote wamefaulu mtihani wa ubatizo baada ya kufundishwa na Mwalimu Peter Mabula kisha kufanya mitihani chini ya usimamizi wa Mtumishi wa MUNGU Scholar Mabula.
 wote walifaulu kisha Mchungaji Kiongozi Elly Botto akawabatiza katika Bahari ya Hindi.
Hizi ni baadhi ya picha katika tukio hilo la ubatizo.
Baadae nitawaletea Mitihani ya Ubatizo ambayo niliowafundisha wote walifaulu. 
Katika Mtihani huo unaweza kujipima na wewe hata kama ulishabatizwa au hata kama hujabatizwa.
Waefeso 4:4-6 '' Mwili mmoja, na ROHO mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.BWANA mmoja, imani moja, UBATIZO mmoja.MUNGU mmoja, naye ni BABA wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.''

MUNGU akubariki.
By Mwinjilisti Peter Mabula.
Kubatizwa kwa maji ni Ishara ya kufa na kufufuka na Yesu Kristo (Wakolosai 2:12)

Mchungaji Elly Botto akiomba

Dada huyu baada tu ya kubatizwa alijawa na nguvu za ROHO MTAKATIFU na kuanza Kunena kwa lugha Mpya.
Alipata double double yaani kubatizwa kwa maji na kubatizwa kwa ROHO MTAKATIFU.

Mchungaji Emmanuel Akiomba wakati wa ibada ya ubatizo.

Ubatizo wa maji ni
Ni Ishara ya ondoleo la dhambi
Ni Ishara ya kufa na kufufuka na Kristo
Ni Ishara ya kuachana na ya dunia ili uambatane na Yesu Kristo.

Anayebatizwa lazima amwamini Yesu Kristo kama  Bwana  na Mwokozi wake

 Kubatizwa Ni kutii ushauri wa Mungu (Luka 7:29 – 30)

Dada huyu akinena kwa lugha baada ya kubatizwa.



Watu 11 waliobatizwa jumamosi iliyopita wakiwa pamoja na wachungaji

Dada huyu akifurahi pamoja na wachungaji baada ya kubatizwa. Dada huyu alikuwa mganga wa kienyeji na MUNGU alimfungua baada tu ya kubatizwa mapepo yalimwacha.



Scholar Mabula  akiwa na baadhi ya waliobatizwa siku hiyo.

Comments