MLIKUSUDIA MABAYA

Na Askofu Dk Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

“Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. “Mwanzo 50: 20
Mambo makubwa yote ambayo yanaweza kumsababisha Mungu akatenda mambo makubwa Duniani yalisababishwa na mtu kuuchokoza Ufalme wa Mungu, kwenye Biblia mahala ambapo Ufalme wa Mungu haujachokozwa huwezi kuona mambo makubwa yakitokea.
DANELI NA BARAZA LA MAWAZIRI
”Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. .” Danieli 6:1- 1
Alikuwepo Mfalme aitwaye Dario alitawala nchi iliyoitwa Koresh ambayo sasa inayoitwa Iran kabla ya kristo, chini yake alikua na maliwali 120 wakimsaidia lakini Mfalme alipendezwa aweke maliwali watatu wakubwa ambao watafanya kazi karibu yake na mmoja wao alikuwepo Danieli.
Daniel 6:3 “Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote”.
Ulitokea uvumi hata kabla Mfalme hajawaapiza hao watu watatu kwamba Danieli ni mmoja wao, mtu ambaye sio raia wa nchi ya Koresh anakabidhiwa uongozi wapil kutoka kwa Mfalme. Cha kushangaza Danieli peke yake ndiye aliyetajwa jina kati ya hao watatu, kulikuwa na uvumi unaonekana kwamba Danieli atainuliwa. Shetani anaweza kunusa kwenye ulimwengu wa roho akajua utainuliwa baadaye kama wale mamajusi walivyonusa kwa namna yao ya kichawi wakajua Yesu kristo atazaliwa mashariki ya kati.
Daniel 6:4 “Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.”
Walikaa mawaziri na viongozi wengine wakapanga mchoro mbaya juu ya Danieli kwamba wamsingizie Danieli jambo litakalo mwangusha akose uteuzi wa nafasi tatu za Juu, lakini walishindwa kupata cha kusingizia mpaka wakaamua wamsingizie kwenye mambo ya Mungu wake.

Danieli 6:6 “Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.”
Watu hawa walipanga wamwangushe Danieli wakaamua kwenda kwa Mfalme, wakamwambia Mfalme tumeamua tukuenzi na kukuabudu wewe pekee asiabudiwe mtu mwingine, basi Mfalme Dario akaona jambo hilo ni jema akaamua kuweka amri kuanzia siku ile asiwepo mtu atakayeabudu isipokuwa kumwabudu yeye. Basi wale viongozi wakawa wameshaweka eneo ambalo mtu atakayeomba isipokuwa kwa Mfalme atupwe kwenye shimo la shamba, Danieli akasikia ule mpango naye akabadilisha namna ya kuomba akiwa amefunga mlango, akafungua milango yote na madirisha akawa anamwabudu Mungu wake kwa uwazi kila mtu asikie na aone “hapo ikawa Falme mbili zinapigana Ufalme wa Mungu Yehova na Ufalme wa Giza wa shetani” Danieli akafungua milango akazidisha kuomba akielekeza sauti yake Yerusalem.
Danieli 6: 15 “Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. 16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.”
Habari zikamfikia Mfalme watu wakakusanyika kwa Mfalme wakamweleza kwamba kuna mtu amevunja marufuku iliyowekwa naye Mfalme Dario akaamuru mtu huyo aitwe ndipo Daniel akaletwa mbele ya Mfalme, Mfalme alipomwona Daniel kafahamu kumbe ulikua ni mpango uliomlenga Danieli. Mfalme akataka kumwokoa Danieli lakini akashindwa. Danieli akatupwa ndani ya shimo la Simba na wale viongozi waliomsingizia wakasheherekea wakidhani mchoro wao umefanikiwa. Danieli aliwekewa jiwe juu ya shimo pamoja na mhuri wa Mfalme.
“Kumbe jambo linaweza kuandaliwa kumbe unalengwa wewe, usiogope yupe mfalme mahali anaona shida yako anaona umetumbukiwa kwenye shimo kwasababu ya wivu wa watu Fulani wewe simama Mungu unayemtumikia atakuokoa na utatoka salama kwa jina la Yesu”
Duniani kuna watu ambao wameitwa na Mungu kwaajili ya kuanguka chini na wengine kupanda juu, ukishindana na watu wa namna hii utaanguka chini lakini ukiambatana nao utainuliwa kwenda juu.
Daniel 6: 18 “Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.”
Asubuhi Mfalme akaondoka mapema mpaka kwenye shimo la Simba kwa huzuni akamlilia Danieli. Akasema Ee Danieli mtumishi wa Mungu aliye hai, (Mfalme alikua na imani kubwa mno kwa Mungu wa Danieli). Adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake, Miriam alimshambulia Musa ndugu yake, Daudi alishambuliwa na mwanaye, Yesu alishambuliwa na Mweka hazina wake na namna yao ya kuanguka ilikua moja ambao ni kifo, kila anayefanya vita na watu wa Mungu mwisho wake huishia kuanguka.
Daniel6: 20 “Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?”
Mfalme alipomkuta Danieli akamuuliza ee Danieli Mungu unayemtumikia amekuokoa?, Danieli akiwa bado anamheshimu Mfalme japo ndiye aliyetoa amri ili atupwe shimoni lakini kwa kulazimishwa na wasaidizi wake, Danieli akajibu Ee Mfalme Mungu ametuma malaika wake naye amefumba makanywa ya simba kwasababu mimi nalionekana sina hatia mbele zake na mbele zako ee Mfalme. Simba walikua wana njaa lakini hawakuweza kumla Danieli sababu hakuwa na hatia, wale waliomsingizia Danieli walikua wakifurahia wakidhani tayari ameshafariki kumbe bado yu hai.
Daniel6:23 “Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danielii katika lile tundu. Ndipo Danielii akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.”
Baraza la Mawaziri likashangaa kuona Danieli ametoka kwenye tundu la Simba wakajiuliza nini kitafuata baadaye. Basi Mfalme akaamuru wale waliomshtaki Danieli waletwe ili Simba wawe kipimo cha kumpata mwenye haki. Bilashaka waziri mkuu akaitisha baraza la mawaziri akawaambia Mfalme na wao wapelekwe kule shimoni siku moja kama Danieli alivyowekwa. Mfalme akaamuru mawaziri na wake zao na watoto wao waingizwe mle shimoni walidhani ni kusheherekea kumbe ni kuangamizwa. Wake zao na watoto hawakuwepo kwenye fitina ile lakini kama umezaliwa au jiungamanisha na mwovu yeyote nawe tegemea hayohayo yakupate kwa jina la Yesu.
“Ukipanga mabaya juu ya mtu wa Mungu siku moja mabaya hayo yatakujia kwako wewe na watoto wako na wanao, ndivyo ambavyo Mungu anavyotenda kazi.”
Sheria ya Mungu inasema kile walichopanga kwaajili yako kwa Ubaya baadaye kile kiwakurudia wao na familia zao na watoto wao kwa jina la Yesu.
Hapo ndipo mahala pokee kwenye historia ya Neno la Mungu liliangamizwa baraza lote la mawaziri wakiwa na wake zao na watoto wao. Biblia inasema nitayatimiza yale niliyosikia mnayasema, wana wa Israeli walinungunika wakiwa jangwani kwamba bora wafe jangwani kuliko kwenda kwenye nchi ya ahadi ndipo Mungu alipoamua kuwatendea kama alivyowasikia wanasema. Uongozi uliokuja ulikua ni unamwona Danieli kama mkuu na kumwogopa sababu alibaki yeye peke yake.
Daniel6: 25 “Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danielii; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.”
Yuleyule aliyetoa amri kwamba Danieli awekwe kwenye tundu la Simba yuleyule alitoa amri watu watetemeke na kuogopa mbele ya Mungu wa Danieli. Wakati ule Neno la Mfalme lilikuwa likitolewa linakua sheria tofauti na leo sheria zinatungwa na Bunge.
Daniel 6: 27 “Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danielii na nguvu za simba.”
“Usiwaone watu wamesimama ukawagusa sababu utapigwa na ukipigwa usione unapigwa kwasababu hao ni watakatifu sana hapana ni kwasababu Mungu ameweka kusudi ndani yao kwaajili ya Dunia, sasa unapowagusa hao unagusa kusudi la Mungu ukajikuta unapigwa”
YUSUFU NA NDUGU ZAKE 11
Yusufu amezaliwa kwenye Familia ya watu kumi na mbili akawa anapeleka taarifa kwa Baba yake pale ndugu zake walipokua wanafanya mabaya, kibinadamu walimwona kama mchonganishi hafai, jambo la pili alikua anapendwa na Baba yao kuliko wengine wakamchukia wala hawakuweza kuongea naye kwa amani/furaha, walimwona kama mchongezi, anapendwa na Baba yake kuliko wao, pia alikua ameshonewa kanzu nzuri na Baba yake huku wao wakiwa hawajashonewa, halafu kingine aliota ndoto kwamba atawatawala baadaye jambo ambalo lilipeleka wakataka kumuua.
Ndugu zake waliona wivu juu yake japo alikua ni mdogo wao. Walichukia kwasababu alikua ana ndoto ya siku moja kuwala. Ni watu wa familia moja Baba na Mama mmoja, wamepanga mipango ya kumuua ndugu yao.

Aliyekuwepo kaka yao anaitwa Ruben aliwashauri wasimwage damu ya ndugu yao ila wamfungie kwenye shimo (ili aje amtoe amrudishe kwa Baba yake).
Watu walisikia wivu kwamba anapendwa na Baba Mungu, amefunikwa na Mungu, ana maono,ana ndoto ya Utawala wakaona wivu juu yake. Sheria ya wivu ni kwamba kama mtu anakuonea wivu ni uthibitisho kuwa kuna kitu umemzidi anayekuonea wivu. “Biblia inasema mafarisayo na masadukayo waliojaa wivu wakawakamata Mitume wa Mungu wakawaweka ndani”
Yuda (ambaye Yesu alizaliwa kutoka kwake, Yesu ni Simba wa Yuda) alitoa wazo wasimuue mdogo wao bali wamuuze aende mbali kwenye taifa lingine. Walimuuza Yusufu kumbe walikua wanamwahisha kwenye ndoto yake. Mungu akamuandaa awe karibu na waziri mkuu aone anafanya nini ili baadaye aje achukue nafasi yake,Siku moja Yusufu akiwa nyumbani kwa Waziri mkuu wa Misri, waziri alitoka akabaki yeye na mke wa Waziri ambaye alimlazimisha awe naye kimahusihano lakini Yusufu akakimbia na kuacha shati yake, baadaye Waziri mkuu alivyokuja mke wake alimwambia Yusufu alitaka kumbaka na uthibithisho ni shati lake aliloliacha, kwa sababu hiyo Yusufu alifungwa maisha gerezani akiwa na ndoto yake.
“Usiogope mabaya yanayokuja mbele yako Mungu anakuandaa kwaajili ya baadae usiogope wala usiwe na wasiwasi Mungu ni Mungu wa mipango anaandaa mipango mema kwaajili yako kwa jina la Yesu.”
Yusufu akakaa gerezani akihangaika kwa miaka mingi, Kumbuka aliuzwa na ndugu zake akiwa na miaka 17 lakini alikuja kuwa waziri mkuu akiwa na miaka 40 na inamaana kuna miaka ishirini na iliyokua inamnoa mpaka kufikia uwaziri wake.
Yusufu alipoingia gerezani alikua kwenye level ya Uwaziri mkuu akasogea kwenye level ya Mfalme, Yusufu akakutana na wafanyakazi waliokua wakimwandalia Mfalme Farao chakula nao wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuharibu chakula na juisi ya Mfalme. Unaona Yusufu bado alikua na ndoto yake akiwa gerezani akatafsiri ndoto za wale waliokua watumishi wa Mfalme kwamba mmoja atanyongwa na mwingine atapona. Kipindi kile wamisri walikua wameweka haki kwenye kamba mtu ukinyongwa kwenye kamba ikatokea ikikatika unaitwa mwenye haki na isipokatika unakufa.
Yule mfanyakazi aliyepona Yusufu alimwomba akifika kwa Farao amtaje kwamba amesingiziwa kumbaka mke wa Waziri mkuu, Biblia inasema yule mtu alipofika kule kwa Farao akasahau kumkumbuka Yusufu, Imeandikwa (Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu amfanyaye kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Mungu). Basi aliposhindwa kumtaja Yusufu kwa farao, Mungu akatengeneza mlango mwingine na Yusufu akaonana na Mfalme.
Kuna mtu uliweka nguvu zako kwake ukamtegemea akusaidie akuvushe lakini hajafanya hivyo, usifadhaike maana Mungu atakufungulia mlango mwingine kwa jina la Yesu. Siku moja Yule mtu aliyekua anamwandalia Farao juisi akasikia Farao ameota ndoto ambayo hakuna mtu aliyeweza kuitafsiri, hapo akamkumbuka Yusufu na kumwambia Farao habari zake kule gerezani.
Yusufu akakumbukwa na yule kijana aliyemtafsiria ndoto akamwambia Farao kuna mtu yupo gerezani anaweza kukutafsiria ndoto yako sababu alinitafsiria ndoto yangu ikatimia. Muujiza wa kwanza ukampata Yusufu naye akaenda kunyolewa nywele ili aonane na Farao, Yusufu akafika kwa Farao akamtafsiria ndoto zile kipindi kuhusu cha miaka saba ya mavuno na miaka saba ya njaa, akamwambia mchague mtu mmoja mwenye hekima ambaye atafanikisha kazi hii. Yusufu akazitaja sifa anazotakiwa kuwa nazo mtu wa kazi ile naye akataja sifa zake mwenyewe. (Muujiza ukitokea taya sifa zako ili umiliki mwenyewe kwa jina la Yesu.)
Mfalme Farao akamtoa Yule waziri mkuu aliyemfunga gerezani nafasi yake ikachukuliwa na Yusufu. Biblia inasema yusuf akakusanya chakula na ile miaka Saba ya shibe ikaisha na njaa ikaingia katika nchi ya Misri kwenye miaka mingine Saba ya njaa. Baadaye njaa ilienea duniani kote mpaka wale ndugu zake wakaja kule Misri wakachukua chakula Yusufu akiwa waziri mkuu. Wao hawakumjua lakini yeye aliwajua kwasababu mtendaji wa mabaya huwa hakumbuki mabaya aliyotenda lakini mtendewa mabaya hukumbuka yote.

Yusufu aliweka kikombe cha mfalme kwenye mizigo yao halafu akawatuma askari kwenda kuwakagua, wale ndugu zake hawakua wamechukua kikombe kile wakajiamini wakakubali kusachiwa kumbe kikombe kimewekwa na Yusufu ili awakamate kwamba wametaka kukiiba lakinii lengo lake lilikua kuwakumbusha kwa habari za ndoto yake na mambo waliyomtendea, wakapatana naye na wakaishi pamoja.
SHADRACK MESHACK NA ABEDNEGO
Alikuwepo Mfalme aliyekuwa anatawala mashariki ya kati mpaka Asia yote, Mfalme huyu aliweka amri kila mtu aabudu sanamu ya mfano wake lakini kina Shadrack, Meshack na Abednego walisimama wakakataa kumwabudu mfalme wakisema wako tayari kufa kwenye moto kuliko kuabudu sanamu. (kila sanamu ni ushetani). Walisimia msimamo wao wakikataa kuabudu sanamu mpaka wakaingizwa kwenye moto.
USIOGOPE.
Mfalme aliandaa mjadala akawauliza Shadrack, Meshack na Abednego je ni kwamakusudi au bahati mbaya wamekataa kuabudu sanamu ile au kwa makusudi, lakini kina shadrack meshack na Abednego walikataa wakisema si kwa makusudi bali wamekataa kuabudu kisicho hai, Basi wakaandaliwa watupiaji wa kuwatupa kwenye moto uliokolezwa wakawanawatupia kina Shadrack, Meshack, na Abednego lakini wao ule moto ukawateketeza, maana yake wale waliojiandaa kukutupa kwenye moto wateketee wao kwanza kwa jina la Yesu.
Na baaaye akapita mtu mmoja akachungulia kwenye ule moto akaona wapo watu wanne badala ya watatu na mmoja wao anaonekana kama mwana wa miungu(alikua malaika). Mungu akawaponya na ule moto na tangu siku ile Mungu wa Shadrack, Meshack na Abednego akaabudiwa na watu wote.
Kila aliyesema jambo juu yako ikiwa hukulifanya mabaya hayatakupata wewe na yatampata yeye na familia yake na watoto wake kwa jina la Yesu. USIOGOPE

Comments