MTU WA MUNGU AKISIMAMA TAIFA HUINUKA.

Na Mtume  Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Bwana Yesu asifiwe sana, ndugu za wapendwa leo Bwana anatukumbusha juu ya kutetea maisha yetu na taifa letu kwa ujumla. 

Kwa siku za hivi karibuni, kumetokea wimbi la huzuni, wasiwasi, mashaka na hali ngumu za kimaisha, pengine tunahisi ni utawala uliopo ama ni hali y kawaida lakini leo, Bwana amenipa ujumbe juu yako ndugu yangu, usione njaa, ukame, matetemeko ya nchi, maafa ya kila namna na maangamizi ya mvua ya mawe na vimbunga. Hayo ni matokeo ya ibada za kipepo....... 

Unaweza usielewa kwasasa, ila tafakari kwa kina, kama wanasayansi wanasema ni mabadiliko ya tabia ya nchi, kwanini hatukuyaona haya tangu mwaka jana na miaka iliyotangulia, na kama ndiyo mabadiliko yenyewe kwa hiyo hii hali itadumu kwa muda gani!!!na mbona yote yamekuja kwa mfululizo?
Ndugu mpendwa, Mungu anakutaka usimame utetee taifa lako kama Ibrahim, anakutaka uwe Lutu wa leo! Anataka uutafute uso wake, utubu kwaajili yako, nyumba yako na taifa lako ili aiponye nchi yako. 


***ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya :basi nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao (2Nyakati 7:14) ***
Ndugu mpendwa, toba yako si italeta ukombozi wa ardhi, bali pia uponyaji wa ardhi. 

Maombi yako yakifanyika kwa usahihi utashangazwa na hali itakavyobadilika! Mvua itarudi katika utaratibu wake, na itatosheleza mahitaji, haitazidi wala kupungua. Mazao yatapatikana ya kutosha, na wala hayataharibiwa na nzige wala viwavi(Yoeli 2:21-27). 


Ndugu yangu mpendwa, unalojukumu la kuiombea familia yako ili ipate neema ya mavuno, ukame usitawale wala mafuriko yasiharibu tena. Omba mvua inyeshe tena kwa kiwango wala si kwa uharibifu.
Ndugu mpendwa, Mungu amekukumbuka ndiyo maana anakutaka uombee mazingira uliyopo.
Sehemu ijayo, nitakujilisha maeneo ktk maisha yako yaliyoharibiwa.
Nakutakia Neema ya Kristo katika Maombi haya.
Ap Sospeter SN
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania

Comments